Tafuta

2023.09.16 Papa amekutana na maafisa na Askali Polisi mjini Vatican. 2023.09.16 Papa amekutana na maafisa na Askali Polisi mjini Vatican.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa Francisko kwa Polisi:Fanyeni jamii iwe ya haki na ya ubinadamu zaidi

Papa Francisko mekutana na maafisa na Askari Polisi wa Italia katika Uwanja wa Mtakatifu Petro katika kukumbuka shujaa Makamu Bregedia Salvo D'Acquisto aliyeuawa kwa kutetea wengine.Papa amesema bado hata leo hii kuna umuhimu wa kupamana dhidi ya uhalifu na mawazo ya mafia.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Maafisa na Askari Polisi wa Italia wakiwa na familia zao, Jumamosi tarehe 16 Septemba 2023 katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican uliopambwa na karibu na watu elfu sita. Papa katika fursa hiyo kwenye hotuba yake amekuwa na furaha ya kuwakarisha na kuwashuru kukutana nao. Wamekuwa hapo katika fursa ya kumbukizi ya  Makamu Brigedia Salvo D'Acquisto, ambaye mama kanisa amemtambua kama ni Mtumishi wa Mungu na shujaa wa Nchi ya Italia ambaye alilipa ahadi yake kama polisi  kwa sadaka  ya maisha yake na ambapo  miaka themanini iliyopita, mnamo tarehe 23 Septemba 1943, alijitolea mwenyewe kuokoa mateka wasio na hatia waliotekwa na kundi la wanajeshi wa kinazi. Papa amewaeleza polisi hao kuwa inafaa  kumtazama mwenzao huyo, kwa utume alioufanya kwa roho ya kujinyima, kwa ushuhuda uliokithiri ambao aliwaachia. Kutokana na muktadha huo, Papa amependa kukumbuka kwa pamoja lakini sio kubaki tu katika siku za nyuma badala yake, kupata motisha thabiti wa kujenga siku zijazo. Kukumbuka mwenzao huyo, haimaanishi kubaki katika ukumbusho usio na uhai ambao unabaki nyuma, bali kujifunza, kutokana na sadaka hiyo na ukarimu huo, kufanya upya ahadi yao  kwa Jeshi leo, katika huduma ya wema na ukweli, wa  taasisi ya  huduma.

Papa amekutana na Polisi Italia
Papa amekutana na Polisi Italia

Baba Mtakatifu ameeleza kuwa Salvo D'Aquisto aliishi katika miaka ya kutisha ambapo ulimwengu ulikuwa vitani, mateso ya ubaguzi wa rangi yalikuwa yakiendelea huko Ulaya na mantiki ya chuki ilionekana kutawala. Katika kitongoji kidogo cha Torrimpietra, ambako alikuwa ametumwa kufuatia ombi lake la kujisikia kuwa muhimu kwa watu maskini, vijana ishirini na wawili walihatarisha kupigwa risasi na  Kikundi cha Kinazi.  Uongo wa shutuma zilizotolewa dhidi yao, hasira ya upofu iliyolenga kulipiza kisasi ambacho wao walikuwa waathrika, nguvu ya chuki iliyotawala juu ya huruma, ilidhoofishwa na ukarimu wa yule Makamu Brigedia kijana, ambaye alijishtaki mara moja badala ya wengine na kuwasadikisha wale waliohusika kuwa yeye ndiye pekee aliyepaswa kunyongwa.

Tukio la Papa na Polisi wa Italia

Katika mantiki hiyo Papa Francisko ameongeza kusema je inawezakanaje kushindwa kuona, chini ya historia hii yenye kustaajabisha na yenye kugusa moyo, kuiga mfano wa Yesu ambaye, alitumwa na Baba ili kutuonesha upendo wake, alitoa uhai wake ili kutuweka huru kutoka katika nguvu za kifo, alichukua dhambi zetu juu yake mwenyewe kama asemavyo nabii kuwa: “aliyachukua mateso yetu, alichukua maumivu yetu na kwa usahihi "kwa kupigwa kwake sisi tuliponywa” (Isa 53,4-5). Hata leo hii, Papa amebainisha kuwa historia ya sadaka ya , historia ya Makamu  Brigedia D'Acquisto inawakilisha onyo la wakati unaofaa sana, yaani wakati tunaishi katika wakati uliochafuliwa na ubinafsi na kutovumiliana kwa wengine, na pia kwa kukithiri kwa aina nyingi za vurugu na chuki ambazo tunaona katika miji yetu, ushuhuda wake unatupatia ujumbe uliojaa nguvu ya upendo.

Kama kawaidia upendeleo kwa watoto
Kama kawaidia upendeleo kwa watoto

Kwao ambao kila siku wanajitolea kutumikia haki na uhalali  na ni hitaji kiasi gani la uhalali leo! , Papa ameongeza: Ningependa kusema kwamba yote haya hupata sababu yake na lengo lake kuu katika upendo. Haki, kiukweli, haielekei tu kutoa adhabu kwa wale ambao wamefanya makosa, lakini kurejesha watu kwa jina la heshima na manufaa ya wote.”  Kwa maana hiyo, dhamira yao ni kubwa.” Aidha Papa amesema “Ningependa kusema kwamba ninyi polisi mnaitwa  sio tu kufanya wajibu wenu", kutumia kanuni na taratibu, lakini ni kufanya  zaidi ili jamii  iwe na haki na ya kibinadamu. Kwa hiyo ni vizuri kwamba wao kama polisi ni watu wenye shauku, kama Salvo D'Acquisto; watumishi wa Serikali na manufaa ya wote, wanaopambana na udhalimu, kutetea wanyonge, kutoa hisia ya ulinzi kwa miji yetu. Mapenzi ya Waitaliano kwao yanashuhudia kwamba haya si maneno tu bali, shukrani kwa mfano wa wengi wao  ni ukweli!” Bila shaka, haya yote Papa amesisitiza yanahitaji sadaka na kujitolea, nidhamu na upatikanaji, hisia ya wajibu na kujitolea.

Papa na Polisi na familia zao
Papa na Polisi na familia zao

KBaba Mtakatifu kwa hiyo amewafikiria wao wanaojikuta wamezama katika mazingira magumu, ambayo haki mara nyingi hukanyagwa, na ambao wanaitwa kupambana dhidi ya kila aina ya uharamu, dhidi ya uhalifu uliopangwa na dhidi ya hisia ya kutokujali ambayo wakati mwingine kwa bahati mbaya ina mizizi, dhidi ya mawazo ya mafia. Amewafikiria  wao wanaotekeleza kazi za uchunguzi, wakiweka teknolojia za hali ya juu katika huduma ya utafiti wenye subira, makini na wenye uwezo, ili uwongo ufichuliwe. Bado Papa amewafikiria wao  ambao, katika maeneo yenye migogoro na katika mazingira ya kimataifa, wanajua jinsi ya kufikia wakazi wa eneo hilo, na kuwa mafundi wa amani kwa njia ya upatanisho, kukuza watu na ujenzi wa kimya wa mema. Na pia amewafikiria wale wanaofanya huduma ya kila siku yenye thamani katika mitaa ya miji yetu na katika pembe za vitongoji vyetu.

Zawadi kwa Papa kutoka kikosi cha Polisi Italia
Zawadi kwa Papa kutoka kikosi cha Polisi Italia

Kwa njia hiyo Papa Francisko amewashuruku kaka na dada hao na kusema asante kwa kwa kila kitu wanachofanya. Kadhalika amewaomba wasivunjike moyo kamwe, wasijitoe kwenye jaribu la kufikiri kwamba uovu una nguvu zaidi, na kwamba ubaya zaidi hautaisha na kwamba kujitolea kwao ni bure. Wakimtazama Salvo d'Acquisto, waache wauhuishwe na shauku ya kufanya mema. Amewaomba pia waendelea kuonesha ukaribu na watu, ambao wamegundua tabia yao hiyo nzuri kila wakati. Amewabariki, wanafamilia wao,  wapendwa wao zaidi, ambao nao pia amesema  wanashiriki katika Utume wao. Na amewaomba waache Bikira Amini anawasindikize na wanapomuomba wasisahau pia  kutoa sala kwa niaba ya Papa Francisko. Amehitimisha.

Papa na Polisi Italia tarehe 16 Septemba 2023
16 September 2023, 12:39