Papa Francisko atoa shukrani kwa Marsiglia na kumbukizi ya wahanga wa Nice
Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi tarehe 23 Septemba 2023 mara baada Ibada ya Misa Takatifu katika uwanja wa Velodrome huko Marsiglia, amependa kutoa shukrani zake. Akianza amesema “Ninakushukuru, mwadhama, kwa maneno yake amewashukuru wote kaka na dada , kwa uwepo wao na kwa maombi yao. Papa amebainisha alivyofikia mwisho wa ziara yake ambapo ametaka kutoka shukrani zake kwa mapokezi mazuri aliyopokea, pamoja na kazi na maandalizi yote ambayo yamefanyika. Amemshukuru Rais wa Jamhuri na kupitia kwake, ametoa salamu za matashi mema kwa wanaume na wanawake wote wa Ufaransa. Amemsalimia Waziri Mkuu aliyekuja kumkaribisha katika uwanja wa ndege na pia aliwasalimia viongozi waliokuwapo, hasa Meya wa Marsiglia.
Papa Francisko ameonesha kukumbatia Kanisa zima la Marsiglia, pamoja na parokia zake na jumuiya za kitawa, taasisi zake nyingi za elimu na mashirika yake ya upendo. Jimbo kuu hilo lilikuwa la kwanza ulimwenguni kuwekwa wakfu kwa Moyo Mtakatifu wa Yesu, wakati wa mlipuko wa tauni mnamo mwaka 1720. Kwa hiyo Papa ameongeza kusema “mioyoni mwenu muwe ishara za upendo mwororo wa Mungu, pia katikati ya janga la leo hii la kutojali”. Asante kwa huduma yao ya upole na ya kujitolea, ambayo inashuhudia ukaribu na huruma ya Bwana! Baadhi yao walifika hapo kutoka sehemu mbalimbali za Ufaransa: waliwashukuru kwa kifarasa merci à vous!
Pia Baba Mtakatifu alipenda kuwasalimu kaka na dada kutoka Nice, wakisindikizwa na Askofu na Meya wao. Amekumbuka shambulio baya la tarehe 14 Julai 2016, ambalo walikuwa ni manusura. Kwa hiyo ameomba “Wakumbukwe katika sala wale wote waliopoteza maisha katika mkasa huo, pamoja na vitendo vyote vya kigaidi ambavyo vimekuwa vikifanyika nchini Ufaransa na kila sehemu ya dunia. Ugaidi ni woga. Tusichoke kuombea amani katika maeneo yenye vita, na hasa kwa watu waliokumbwa na vita wa Ukraine.”
Ni matumanini ya Papa kuwa salamu zake za dhati zitafika kwa wagonjwa, kwa watoto na wazee, ambao ni kumbukumbu ya ustaarabu. Amewafikiria hasa wale walio katika matatizo na wafanyakazi wote katika jiji hilo: Jacques Loew, Padre wa kwanza mfanyakazi wa Ufaransa, aliyefanya kazi kwenye bandari ya Marsirglia alisema kuwa “Heshima ya wafanyakazi iheshimiwe, ikuzwe na kulindwa! Papa kwa kuhitimisha amewahakikishia kubeba moyoni mwake matukio ya siku hizi Na kwamba Mama Yeru wa Ulinzi alitazame jiji hilo, ambalo ni jiwe la matumaini, juu ya familia zao zote, na juu ya kila mmoja wao amembariki huku akimbwa wamuombee. Sio kazi rahisi na ameshukuru.