Papa alikutana na Chiara Amirante kuhusu mkutano wa vijana wa Roma
Vatican News.
Utume wa matumaini na msaada kwa watu wasiojiweza katika njia ya imani katika mitaa ya mji mkuu, ndiyo ilikuwa moja ya mada ya mkutano kati ya Papa Francisko na Chiara Amirante, uliofanyika alasiri tarehe 14 Septemba 2023. Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habati Vatican ni kwamba "Kuanzia tarehe 15 - 22 Oktoba hadi 2023 jumuiya ya “Nuova Orizzonte” pamoja na Jimbo la Roma na zaidi ya vijana 200 kutoka katika hali halisi na harakati tofauti za kikanisa, watakwenda mchana na usiku mahali ambapo vijana hukusanyika katika makanisa, mitaani, mahospitalini, magerezani, katika maeneo yaliyo motomoto ya madawa ya kulevya, katika shule kwa ajili ya programu za kuzuia matatizo ya vijana, maskini wanaoishi mitaani, kuvunja ukuta wa kutojali na kuleta msaada wa kusikiliza na thabiti, pamoja na kupeleka ujumbe wa matumaini”.
Baba Mtakatifu kwa mujibu Chiara Amirante mwanzilishi wa Harakati ya Nuova Orizonte alibainisha kuwa anaunga mkono utume huo mpya katika moyo wa Roma na anafurahi kwamba utume huo unaishi kwa ajili ya vijana kwa kusikiliza kilio cha wengi. “Tunataka kuleta nuru ya matumaini na furaha kamili mahali penye giza na giza zaidi.”, Aliongeza kusema Chiara Amirante.