Papa Francisko akumbuka mashahidi familia na watoto 7
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Ma baada ya sala ya Malaika wa Bwan, Dominika tarehe 9 Septemba 2023 pamoja na mengine Baba Mtakatifu alihamia sehemu nyingine ya Ulaya ambapo amebainisha jinsi ambavyo Dominika tarehe 10 Septemba “huko Markowa, nchini Poland, mashahidi Joseph na Victoria Ulma wametangazwa kuwa wenyeheri pamoja na watoto wao 7 ambayo ni familia nzima iliyoangamizwa na Wanazi mnamo 24 Machi 1944 kwa kuwapatia kimbilio baadhi ya Wayahudi walioteswa."
Baba Mtakatifu amesisitiza kuwa "Walipinga chuki na jeuri ambayo wakati huo ilikuwa inapinga upendo wa kiinjili. Familia hiyo ya Poland, ambayo iliwakilisha miale ya nuru katika giza la Vita vya Pili vya Ulimwengu,” Papa Francisko amebainisha kuwa: “iwe kielelezo kwetu sisi sote cha kuiga katika shauku yetu ya mema na katika huduma ya wale wanaohitaji;” na hatimaye ameomba kuwapatia pongezi kwa kuwapigia makofu familia hiyo ya Wenyeheri wapya!...
Na kwa kufuata mfano wao, Papa amesema tujisikie kuitwa kupinga nguvu ya silaha na ile ya upendo, ukakamavu wa maombi dhidi ya maneno ya vurugu. Hebu tufanye hivyo juu ya yote kwa ajili ya nchi nyingi ambazo zinakabiliwa na vita; hapa ninadhani kwa namna ya pekee, tuzidishe maombi kwa ajili ya Ukraine inayoteswa! Kuna bendera huko Ukraine, ambayo inateseka sana, sana! Papa Francisko amesisitiza hayo akitazama waamini na mahujaji katika Uwanja wa Mtakatifu petro ambamo kulikuwa na bendera za Ukraine.