Papa anawapongeza wafanyakazi wa Famasi,Vatican kutimiza miaka 150
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko Jumatatu tarehe 18 Septemba 2023, amekutana na Wafanyakazi wa Famasi ya Vatican katika fursa ya Miaka 150 tangu kuundwa kwake. Akianza hotuba yake, amemsalimu Kardinali Vérgez, Rais wa Utawa na Sr. Raffaella Petrini, Katibu Mkuu tawala, Padre Jesús Etayo Arrondo Mkuu wa Shirika la Fatebene Fratelli,Baraza zima, Mkurugenzi Ndugu Thomas Binish, pamoja na Watawa wa Shirika la Hospitali la Mtakatifu Yohane wa Mungu na wote wapendwa wahudumu na wafanyakazi wa Famasi. Papa amesema ni vizuri kukutana nao wakati maadhimisho ya miaka 150 tangu kuanzishwa kwa famasi yakiwa yanakaribia. Papa akitazama mizizi ya historia ya famasi hiyo, amependa kukumbusha kuwa taasisi ilitimiza ndoto ya Papa Gregory XVI, mtawa wa Camaldoli ambaye alifahamu vyema umuhimu wa duka la dawa lililowekwa kwenye monasteri. Wakati huo Mwenyeheri Pio IX ndiye aliyefanikisha ndoto hiyo, akimkabidhi Mkuuwa Shirika la Hospitali la Mtakatifu Yohane wa Mungu kazi ya kuunda duka la dawa mjini Vatican. Amri hiyo, kiukweli, ilijivunia tamaduni ndefu katika eneo hilo, na duka la dawa la nyumba ya kitawa ambalo katika sehemu nyingi pia ilifanya huduma kwa watu wa nje. Eusebio Frommer, Mtawa wa shirika la Fatebene fratelli, kwa hivyo alichaguliwa kama mfamasia wa kwanza na historia yao mara moja ilianza. Kwa hiyo ni miaka 150 iliyopita!
Daima kukumbuka, kwa karibu huacha pamoja albamu ya picha na ni vizuri kukumbuka wakati muhimu, yaani, huduma ya Shirika lao wakati wa Mtaguso wa II wa Vatican. Kila siku asubuhi, kabla ya kuanza vikao vya baraza shughuli, chumba cha Famasia kilikuwa kimejaa Maaskofu wa mataifa yote kwa ajili ya kununua dawa na, wakati huo kikundi kidogo cha watu waliowekwa wakfu wakijaribu kukidhi haja ya maombi hayo kwa lugha tofauti, wauguzi wengine wawili watawa walikuwepo katika vituo vya huduma ya kwanza vilivyowekwa pamoja na daktari na wabeba machela wawili, kwa hitaji jingine lolote. Na kwa kujikita katika nyakati zetu kwa sasa, Baba Mtakatifu amesema kuwa na Duka lao la Dawa ambalo halitofautiani na maduka mengine kwa sababu tu limejitolea kwa ajili ya huduma ya moja kwa moja ya Mrithi wa Petro na wa Curia Romana, lakini pia ni kwa sababu linaitwa kuwa na nyongeza ya upendo inayotekeleza huduma ambayo, pamoja na uuzaji wa dawa, inahitajika kujitokeza kwa umakini wake kwa watu dhaifu na kwa utunzaji wa wagonjwa. Ni ahadi inayolenga sio tu kwa wafanyakazi wa Vatican na wakaazi wa Jiji la Vatican, lakini pia kwa wale wanaohitaji dawa fulani, ambazo mara nyingi ni ngumu kupatatikana mahali pengine.
Papa Francisko kwa njia hiyo amependa kusema asante kwa hilo: asante kwa Shirika la Fatebenefratelli; kwa wanashirika wa kawaida, kwa wafamasia na wafanyakazi, kwa wale wanaofanya kazi kwenye ghala na kwa wale wote wanaoshirikiana katika kazi hiyo. Asante kwa taaluma yao na kujitolea, lakini pia kwa moyo wa kukaribishwa na kupatikana ambao unafanya kazi yao, ambayo kwa wakati mwingine inahitaji juhudi na kama ilivyotokea hasa wakati wa janga la Uviko utayari wa kujitoa sadaka. Baba Mtakatifu amebainisha kwamba sio rahisi kwao, na sio rahisi kwa wafamasia kwa ujumla, ambao amewafikiria wakati huu na ambao amependa kutoa wazo. Watu wengi wanakuja kwao hasa wazee, ambao mara nyingi, katika kasi ya ha hali ya sasa , hawana haja ya dawa tu, bali pia tahadhari na tabasamu; maana wao wanahitaji sikio na neno la faraja. Papa amekazia kusema wasisahau kuwa na utume wa masikio. ‘Kusikiliza, kusikiliza’ amerudia Papa mara mbili... Ndiyo!, ameongeza inaonekana kuwa ya kuchosha wakati mwingine, lakini kwa mtu anayezungumza ni bembelezo kutoka kwa Mungu kupitia wao. Na wafamasia ni mkono huu wa karibu, unaonyooshwa ambao sio tu hupitisha dawa, lakini hupitisha ujasiri na ukaribu. Papa amewashukuru sana.
Baba Mtakatifu amewambia wasonge mbele wakiwa na jumuiya ya Fatebenefratelli, wafamasia, washirika na wafanyakazi, kwa ukarimu, kwa sababu kila siku wanaweza kufanya mengi mazuri, ili kufanya huduma ya Famasia ya Vatican izidi kuwa ya ufanisi na ya kisasa,na kuonesha kwamba utunzaji makini na ukarimu kwa kufikiria ambayo ni ushuhuda wa Injili kwa wale wanaokutana nao. Papa amewaomba wawe na subira nyingi, wakikumbuka kuwa uvumilivu ni mtihani wa hatua za upendo. Na hatimaye, ushauri mdogo wa kiroho ambao Papa amewapatia ni kuwa kila mara na kisha wainue machao yao kuelekeza kuelekeza Msalabani, wakigeuza macho yao kwa Mungu kwa wale waliojeruhiwa. Utumishi wanaowafanyia wagonjwa ni utumishi unaofanyiwa Yeye. Na ni vizuri kuteka subira na ukarimu kutoka kwa Daktari wa mbinguni na nguvu ya kupenda, bila kuchoka. Shuleni yao Papa amesema, inaanzia katika dawati la msalaba hadi kaunta ya maduka ya dawa, kwa hiyo nao pia wawe wasambazaji wa huruma kila siku. Papa amewabariki na kuwaomba, tafadhali wamwombee.