Papa amekwenda Seneti kutoa heshima kwa Giorgio Napolitano
Vatican News
Domininka tarehe 24 Septemba 2023 muda mfupi baada ya saa saba na robo hivi kama ilivyotangazwa na Ofisi ya Vyombo vya Habari Vatican kwamba: Papa Francisko alikwenda kwenye Jumba la serikali lililowekwa geneza la Rais Mstaafu Giorgio Napolitano, kutoa heshima yake pamoja na uwepo wake kwa sala, mapenzi yake ya kibinafsi kwake na familia yake na kuheshimu huduma kuu iliyotolewa kwa nchi yake ya Italia."
Ikumbukwe mnamo tarehe 20 Septemba iliyopita, katika salamu zake mwishoni mwa katekesi yake, Baba Mtakatifu alikuwa ameelekeza mawazo yake kwa Rais Mstaafu huyo Napolitano, ambaye alikuwa amelazwa hospitalini kwa miezi 4 katika kliniki ya Roma iitwayo 'Salvatorian Mundi,' na ambaye hali yake ya kiafya ilikuwa mbaya zaidi, akimfafanua kama “mtumishi wa nchi". Siku ya kifo chake, tarehe 22 Septemba, katika telegramu kwa mke wake Baba Mtakatifu alikumbuka “mtazamo wake katika uchaguzi muhimu kwa ajili ya maisha ya nchi.”