Papa amekwenda marsiglia kwa tafakari ya changamoto ya uhamiaji
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Baada ya karibu miaka 500 tangu wakati wa Papa Clement VII, Papa anakwenda Marsiglia. Baba Mtakatifu Francisko aliondoka saa 8.45 mchana , Ijumaa tarehe 22 Septemba 2023, kutoka uwanja wa ndege wa Rome-Fiumicino kuelekea mji wa wa kusini mwa Ufaransa, ambapo atabaki huko hadi Jumamosi tarehe 23 Septemba 2023 ili kufunga tukio linalohusu Mikutano ya Mediteranea “Rencontres Méditerranéennes”, kwa mada ya changamoto za uhamiaji. Hili ni tukio ambalo, baada ya Mikutano ya Mediterania ya Bari (2020) na Firenze (2022), inawaleta pamoja maaskofu wa Makanisa yanayotazamana na Mare Nostrum,yaani Bahari yetu ambayo imekuwa kaburi la wazi baada ya ajali nyingi za meli na majanga ya baharini kama ambavyp Papa Francisko mwenyewe alivyoshutumu mara kadhaa.
Papa Francisko akiwa safari ya kuelekea Marsiglia katika kuhitimisha Mkutano ametuma telegramu kwa Rais wa Jamhuri ya Italia, Bwana Sergio Mattarella, ambapo katika telegram hiyo ameandika kwamba: “ Katika muda ambao ninaacha Roma kueleza siara ya Marsiglia,mahali mabapo nitashiki Mkutano ambao unaunganisha makani na mji wa mediteranea kwa lengo la kutafakari juu ya changamoto za ukarimu, ufungamanishwaji na udugu, kwa namna ya kusaidia mazungumza ya kiutamaduni na kuhamasisha njia ya amani, ninayo furaha ya kukelekea wewe, Bwana Rais, salumu zangu, ambazo zinasindikizwa na mtashi mema kwa ajili ya wema wa kiroho na kijamii kwa watu wa Italia, ambao kwa upendo ninatumia baraka zangu.”
Ni katika Mkutano ambao unawaona maaskofu 70 kutoka katika nchi zinazopakana na Bahari ya Mediteranea, ukiwa ni mkutano wa toleo la tatu wa aina hiyo. Mkutano huo unawaona hata vijana wapatao 120. Akiwa ndani ya Ndege hiyo Papa Francisko amesalimia waandishi wa Habari wanaoongozana kwenye ziara hii ya 44 ya kitume kusini mwa Ufaransa, mji ambao unapakana na Bahari ya Mediterranea ambao kwa hakika ni sehemu iliyojaa wahamiaji.
Hata hivyo kabla ya kuondoka katika nyumba ya Mtakatifu Marta mjini Vatican, Papa Francisko kama kawaida sasa kwa mara nyingine tena amekutana na kundi la wanawake 20 hivi ambao wanatunzwa katika Nyumba ya Huruma kwa kuhudumiwa na watawa wa Upendo wa mama Teresa wa Kalkuta. Pamoja nao walikuwepo baadhi ya Masista wa Shirika la Upendo, ambao wamekabidhiwa uangalizi huo. Kisha aliwasili Roma-Fiumicino kwa gari, akilakiwa na Askofu wa Jimbo la Porto-Santa Rufina, ambaye katika mamlaka yake kulikuwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa, na Monsinyo Gianrico Ruzza.