Sala ya Papa mbele ya Mama Maria wa Fatima:fuata anayokuelekeza Mama

Baba Mtakatifu katika ziara yake ya kitume,tarehe 5 Agosti amekwenda katika Madhabahu ya Mama Maria wa Fatima na kusali rozari na mahujaji.Ni ziara yake ya pili ambapo ya kwanza ilikuwa 2017.Mama Maria anatuelekeza ishara mbili ya kukaribisha na kufanya yale ambayo Yesu anatwambia.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Kutoka kwenye kilele cha Madhabahu ya Fatima, moyo wa ibada ya Maria, barani Ulaya, chini ya anga ambalo moto uliozukasiku ya  Ijumaa 4 Agosti  katika eneo karibu na Leira, Helikopta iliyombeba Papa Francisko ilionekana karibu saa 3.40 asubuhi. Alizunguka mara mbili na ukimya uliodumishwa hadi wakati huo na takriban waamini 200,000 waliokusanyika hapo tangu alfajiri (wengine hata kutoka usiku uliopita) umevunjwa kwa makofi ya kishindo. Papa Francisko baada ya kuondoka jijini Lisbon kwa saa chache ambapo amekuwepo huko tangu tarehe  2 Agosti kwa ajili ya Siku ya Vijana duniani (WYD) alichungulia  nje ya dirisha kwenye nafasi ya wazi iliyojaa waamini wakimsubiri. Kutoka juu Kikanisa cha Tokeo alisimama mbele ya sanamu ya Mama Yetu ambaye aliwatokea watoto Francis, Jacinta na Lucia;  kwa hiyo ikawa ndiyo ziara ya Pili ya Baba Mtakatifu Francisko ambapo ya kwanza ilikuwa mnamo tarehe 13 Mei 2017 wakati wa tukio la Maadhimisho ya Miaka 100 tangu alipotokea  Mama Maria wa Fatima kwa watoto hao.

Papa amekaribishwa na umati mkubwa huko Fatima 5 Agosti 2023
Papa amekaribishwa na umati mkubwa huko Fatima 5 Agosti 2023

Kwa njia hiyo wafungwa sita walikaa ndani, pamoja na kundi la vijana wagonjwa ambapo Papa Francisko alisali nao Rozari kwa ajili ya amani.  Hata hivyo wakati wa maombi ulitanguliwa na safari ndefu katika ya Kigari cha Kipapa kutoka kituo cha heliporta, ambapo Papa alitua mapema. Na kwa kilomita 4.5 nzima kwa gari lililo wazi hadi kwenye Madhabahu huku akiwasalimu na kuwabariki watu, zaidi wakiwa wanampungia mikono, bendera na leso nyeupe. Hapakukosekana kuona hata maua ya mawaridi, wengine wakilia kwa hisia kali. Kila mara alioonekana Baba Mtakatifu akisimama kuwasalimia baadhi ya watoto  wakubwa, wadogo na wachanga sana ambao wazazi wao walimpatia awabusu. Wakati huo wote, wimbo wa 'Ave Maria' ulisindikiza pole pole maandamao hayo ya Papa kuelekea kikanisa. Katika kiti cha magurudumu, akiwa na taji la mawaridi meupe Papa Francisko alifika mbele ya Mama na kuomba kwa dakika chake peke yake akiwa ameinamisha kichwa chini na macho yake yamefumba. Kwanza makofi mafupi yalisikika kutoka katika umati. Hatimaye ukimya ulirudi kwenye uwanja mzima. Takriban ikuwa ni ukimya usio wa kawaida kutokana na wingi wa watu.

Sala ya Ukimya
Sala ya Ukimya

Baba Mtakatifu mara baada ya kusali ametoa tafakari yake ambapo amependa kutazama sura ya Maria ​​na kila mtu afikiri kuwa Maria anamwambia nini kama Mama, "ananinonyoshea nini kwa kidole chake. Anatuonesha Yesu, wakati mwingine anatuonesha hata jambo dogo ambalohalifanyi kazi vizuri moyoni. Lakini daima anaashiria. Mama, unanielekeza nini? Tukae kimya kidogo kila mtu moyoni mwake aseme: 'Mama unanionesha nini? “Ni nini kinachonisumbua katika maisha yangu? Je, ni nini kuhusu maisha yangu kinachonisukuma? Kuna nini katika maisha yangu ambacho kinakuvutia na wewe uoneshe hivyo”. Na hapo anatuonesha moyo wa Yesu. Na kama vile Yesu anavyotuonesha, na anaonesha moyo wa kila mmoja wetu." Papa Francisko emesema.

Wazee kwa vijana na watoto walimlaki Papa
Wazee kwa vijana na watoto walimlaki Papa

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na tafakari yake bila kusoma alisema "Ndugu wapendwa, leo tunahisi uwepo wa Maria Mama, Mama ambaye daima anasema: “fanya yale Yesu akuambiayo” Yesu anatuonyesha. Lakini Mama anayemwambia Yesu kuwa fanya utakalo kwako”. Huyu ni Maria. Huyu ndiye Mama yetu, Mama yetu aliye karibu nasi. Na awabariki nyote! Kwa uwepo wenu na kwa maombi yenu. Tulisali Rozari, sala nzuri na muhimu, kwa sababu inatuweka katika uhusiano na maisha ya Yesu na Maria. Na tulitafakari juu ya mafumbo ya furaha, ambayo yanatukumbusha kwamba Kanisa linaweza kuwa nyumba ya furaha. Kanisa ambalo ndani yake tunajikuta ni sura nzuri ya Kanisa yaani ya kukaribisha na bila  kuwa na milango. Kanisa halina milango kwa hiyo kila mtu anaingia. Na hapa tunaweza pia kusisitiza ukweli kwamba kila mtu anaweza kuingia, kwa sababu hii ni nyumba ya Mama na mama daima ana moyo ulio wazi kwa watoto wake wote, bila kutengwa yoyote", Papa alirudia neno "WOTE", neno ambalo lilisika tena wakati wa hotuba kwa vijana.

Aliwasalimia wagonjwa huko Fatima
Aliwasalimia wagonjwa huko Fatima

“Tuko hapa, chini ya uangalizi wa kimama wa Maria, tuko hapa kama Kanisa, Mama Kanisa. Hija kiukweli ni sifa ya Maria kwa sababu kwanza kuhiji baada ya kutangazwa kwa Yesu alikuwa Maria. Mara tu alipojua kwamba binamu yake ni mjamzito, binamu yake alikuwa amezeeka, alitoka mbio. Ni tafsiri ya bure kwa kiasi fulani, lakini Injili inasema “alikwenda upesi”, tungesema “alitoka mbio”, alitoka mbio akiwa na hamu hiyo ya kusaidia, ili awepo. Majina ya Maria yapo mengi, lakini moja ambalo tunaweza kusema hata kuyafikiria ni haya: Bikira anayetoka mbio, kila likitokea tatizo, kila tukimwomba hakawii, anakuja, na anaharakisha. Mama yetu ambaye ni wa haraka", mnaipenda? Hebu sote tuseme pamoja: 'Mama yetu wa haraka. Anaharakisha kuwa karibu nasi, anaharakisha kwa sababu ni Mama.' Papa Francisko alisisitiza.

Papa ameombea amani duniani huko Fatima
Papa ameombea amani duniani huko Fatima

Baba Mtakatifu akiendelea na tafakari yake alisema "Kwa Kireno inasemekana “apressada. Mama yetu ‘apressada’. Na hivyo inaambatana na maisha ya Yesu, na hajifichi baada ya ufufuko, anawasindikiza wanafunzi, wakimngojea Roho Mtakatifu, na anaambatana na Kanisa linaloanza kukua baada ya Pentekoste. Mama yetu ambaye ni wa  haraka na Mama Yetu anayetusindikiza. Daima husindikiza. Ishara ya Mama Maria ya kukaribisha ni mbili: kwanza anakaribisha na kisha anafanya anaelekeza. Kwa nini hii? Kuelekeza kwa Yesu. Maria katika maisha yake hafanyi chochote ila kumwelekeza Yesu. “Fanyeni lolote atakalowambia”. Kufuata Yesu. Hizi ndizo ishara mbili za Maria. Hebu tufikirie juu yake. Anatukaribisha sisi sote na kuelekeza kwa Yesu. Na anafanya hivyo kwa haraka kidogo, “Mama yetu "apressada" ambaye anatukaribisha sote na kutuelekeza kwa Yesu."

Baba Mtakatifu amekazia kusema kuwa "Na kila tunapokuja hapa tukumbuke hilo. Hapa Maria alijifanya kuwapo kwa namna ya pekee, ili kutokuamini kwa mioyo mingi kumfungulie Yesu. Kwa uwepo wake anamnyooshea Yesu, daima kwa hili anamuonesha Yesu. Na leo yuko hapa, kati yetu, yeye yuko kati  yetu kila wakati, lakini leo tunahisi yuko karibu zaidi. Maria aliye na haraka. Baba Mtakatifu amewambia waamini wote hapo kuwa: "Yesu anatupenda hadi kujitambulisha kwetu na anatuomba tushirikiane naye. Na Maria anatuonysha kile ambacho Yesu anatuomba. Kutembea kupitia maisha na tukishirikiana naye". Papa kwa kuhitimisha amesema: "Leo tunahisi uwepo wa Mama Maria, Mama ambaye daima atasema: 'fanya yale Yesu akuambiayo'.  Yesu anatuonesha. Lakini Mama ni anayemwambia Yesu “fanya utakalo kwako”. Huyu ni Maria. Huyu ndiye Mama yetu, Mama yetu "apressada", kuwa karibu nasi. Na awabariki nyote! Amina.”

Tafakari ya papa huko Fatima katika madhabahu ya Mama Maria
05 August 2023, 11:26