Tafuta

Papa:Maria ni mfano wa huduma na sifa kwa Mungu!

Tafakari ya Papa katika Siku Kuu ya Kupalizwa Mbinguni Maria,kwa mantiki mbili:kuhudumia na kutoa sifa kama Maria.Maria alitembea kutoka Nazaret karibu kilomita 150 ili kufika nyumbani kwa Elizabeth:“Kusaidia kuna gharama!Hii tunaifanyia uzoefu hata sisi,katika ugumu,kuvumilivu na wasiwasi unajionesha wakati wa kusaidia wengine.”

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Mama Kanisa kila tarehe 15 Agosti ya kila mwaka anaadhimisha siku kuu ya Kupalizwa Mama Maria mbinguni na thibitisho hakika la imani yetu kikatoliki  ambamo mnamo tarehe Mosi Novemba 1950, Papa Pio XII alitoa Dogma ya Munificentissimus Deus (kwa kiitaliano Il munificentissimo Dio) yaani, ‘Mungu Mkarimu’ ikifafanua utubitisho wa ‘Kupalizwa Mbinguni kwa Maria, Mwili na Roho.’ Kwa hiyo Waamini na mahujaji wengi wakiwa wameunganika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican, kupitia dirisha la kawaida la nyumba ya kitume, Baba Mtakatifu ametoa tafakari yake katika Siku kuu hii ya Bikira Mpalizwa Mbinguni.

Waamini wakisali sala ya Malaika wa Bwana
Waamini wakisali sala ya Malaika wa Bwana

Baba Mtakatifu amesema “Leo hii ni sikukuu ya Bikira Maria, tunamtafakari Yeye ambaye anapanda mbinguni mwili na roho katika utukufu wa Mbingu. Hata Injili ya siku inasimulia  wakati anapanda, lakini kwa hili kuelekea katika eneo la mlima (Lk 1,39), anapanda kwa nini? ili kumsaidia binadamu yake Elizabeti na anamsifu kwa wimbo wa furaha wa kutukuza. Maria anapanda na Neno la Mungu linatuonesha kile ambacho kinamtofautisha wakati anapanda kuelekea juu. Je ni kitu gani kinamtofautisha? Huduma kwa jirani na sifa kwa Mungu; yote mawili. Maria ni mwanamke wa huduma kwa jirani na Maria ni mwanamke anayesifu Mungu

Injili ya Luka na kama nyingine, inasimulia maisha yenyewe ya Kristo kama kupanda kuelekea kilele; yaani kuelekea Yerusalemu, eneo la zawadi yake juu ya msalaba na wakati huo huo, inaeleza  hata safari ya  Maria. Yesu na Maria wanatembea katika njia sawa, yaani maisha mawili ambayo yanapanda juu, wakimtukuza Mungu na kuhudumia ndugu. Yesu kama Mkombozi, mtu anayetoa uhai wake kwa ajili yetu, kwa ajili yetu kuhesabiwa haki; Maria kama mtumishi anayekwenda kuhudumu; maisha mawili yanayoshinda kifo na kufufuka tena; maisha mawili ambayo siri zake ni huduma na sifa. Hebu tuzingatie vipengele hivi viwili: huduma na sifa” Papa amesisitiza.

Papa kwa hiyo amependa kujikita kwa kina katika mantiki hizo mbili na akianza na huduma, amesema: “Ni pale tunapoinama kuhudumia ndugu  ndipo tunakwenda juu; ni upendo ambao unainua maisha”.  Kwa hiyo tupokwenda kuwahudumia ndugu zetu na kwa hudumia ndiyo  tunakwenda kileleni. Lakini kuhudumia siyo rahisi; Maria ambaye mapema alikuwa amechukua mimba, alitembea kutoka Nazaret karibu kilomita 150 ili kufika nyumbani kwa Elizabeth. Papa ameongeza “Kusaidia kuna gharama! Kwetu sote, kuhudumia ni gharama. Hii daima tunaifanyia uzoefu, katika ugumu, katika uvumilivu na katika wasiwasi ambao unajionesha wakati wa kusaidia wengine.”

Watawa wanaonekana wa Poland wakishiriki sala ya Malaika 15 Agosti
Watawa wanaonekana wa Poland wakishiriki sala ya Malaika 15 Agosti

Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu amesema kuwa tufikirie kwa mfano, kilomita ngapi ambazo wengi wanafanya kila siku ili kwenda na kurudi kutoka kazini na wanajikita na  kazi nyingi kwa ajili ya kusaidia jirani; tufikirie ni safari ngapi za wakati na usingizi kwa sababu ya kumsadia mtoto mchanga au mzee; na jitihada katika kuhudumia ambaye hawezi kurudisha, katika Kanisa kama ilivyo wa kujitolea. Papa amebainisha anavyoshangazwa na kujitolea. Ni ngumu, lakini ni kupanda kuelekea kilele; ni kupata Mbingu! Hii ni huduma ya kweli. Hata hivyo huduma ina hatari ya kuwa tasa ikiwa haina sifa kwa Mungu. Kwa hakika wakati Maria alipoinga katika nyumba ya binamu yake alisifu Bwana.  Hakuzungumza juu ya uchovu wake wa safari ,lakini kutoka moyo wake ukatoa wimbo wa furaha. Kwa sababu anayempenda Mungu anatambua sifa.

 Na Injili ya siku inatuonesha“maporomoko ya sifa”: kitoto kilicheza kwa furaha katika umbu la Elizabeti ambaye alitamka maneno ya baraka na kutamka: “heri ya kwanza”: “Heri yeye aliyeamini” (Lk 1:45);na kila kitu kinaishia kwa Maria, ambaye anatangaza sifa kuu (rej. Lk 1:46-55). Sifa huongeza furaha. Sifa ni kama ngazi: huinua mioyo juu. Sifa huinua roho na kushinda jaribu la kukata tamaa. Papa ameuliza swali: “Je mmewahi kuona watu wanaokera, wale wanaoishi kwa porojo, hawana uwezo wa kusifu? Mjiulize: Je, mimi nina uwezo wa kusifu?” Ni jinsi gani ilivyo nzuri kumsifu Mungu kila siku na wengine pia!  Ni jinsi gani  ilivyo nzuri kuishi kwa shukrani na baraka badala ya majuto na malalamiko, kutazama juu, badala ya kukunja uso juu! Papa amesema kuhusu malalamiko kwamba  kuna watu ambao wanalalamika kila siku. Lakini tazameni kuwa  Mungu yuko karibu nawe, tazama kwamba  alikuumba, na tazama vitu alivyokupatia, vyote hivyo ni vya ni Sifa tu. Na hiyo ndiyo afya ya kiroho.” Papa Francisko ameshauri.

Uwanja wa Mtakatifu Petro wakati wa sala ya Malaika wa Bwana 15 Agosti 2023
Uwanja wa Mtakatifu Petro wakati wa sala ya Malaika wa Bwana 15 Agosti 2023

Baba Mtakatifu katika  hilo ameomba kujiuliza maswali kuhusu Kuhudumia na sifa. Je mmni ninaishi kazi na wasiwasi ya kila siku kwa roho ya huduma au ubinafsi? Je ninajikita kumsaidia mtu, bila kutafuta mafao ya haraka? Kimsingi ninafanya huduma ya haraka na shauku katika maisha yangu? Na kwa kufikiria sifa, Baba Mtakatifi amesema je ninatambua kama Maria kumtukuza Mungu (Lk 1,47)? Ninasali na kumsifu Bwana. Na baada ya kusifu ninaeneza furaha kati ya watu ambao ninakutana nao?  Na kila mmoja atafute kujibu maswali haya. Mama Yesu Mpalizwa Mbinguni, atusaidie kupanda kila siku juu zaidi kwa njia ya huduma na sifa. Baba Mtakatifu amehitimisha.

Tafakari ya Papa ya Injili ya Siku Kuu ya Kupalizwa Mbinguni na baada ya sala
15 August 2023, 16:21