Papa:tuwaombee Waukraine wanaoteseka sana,vita ni ukatili
Na Angella Rwezaula, - Vatican
Mawazo ya Baba Mtakatifu yamegeukia nchini wakati mapigano yamekuwa yakiendelea kwa siku 546. Kw amata nyingine tena mwishoni mwa katekesi yake Jumatano, tarehe 23 Agosti 2023 akihitimisha salamu kwa lugha ya Kiitaliano, Papa Francisko ameikabidhi nchini hyo kwa “maombezi ya Mtakatifu Bartholomayo nchi iliyojaribiwa vikali na vita”; kwa kuhuzunishwa na maisha mengi ya binadamu yaliyofifishwa na migogoro hiyo, ameomba kila mmoja asali bila kukoma, siku ambayo bendera ya taifa inaadhimishwa, mkesha wa siku ya uhuru uliopatikana mnamo tartehe 24 Agosti 1991.
“Tuwaombee ndugu zetu wa Kiukraine, wanateseka sana, vita ni ukatili, watoto wengi wamepotea, watu wengi waliokufa, tuombe, tafadhali, tusiwasahau Ukraine wanaoteswa, leo ni tarehe muhimu kwa nchi yao.”
Hapo awali, pia katika salamu zake kwa waamini walitoka Poland, Papa alitaja nchi ya Ukraine na hasa akikumbuka Sikukuu inayokuja ya Mama Yetu wa Czestochowa, tarehe 26 Agosti, kuadhimisha siku kuu nchini Poland kutokana na ibada kubwa kwake, ambayo huleta kwa pamoja idadi kubwa ya watu kwenye madhabahu yake, Papa aliomba kwamba ibada hii izidi kuwasha upendo wa watu wa Poland kwa ajili ya jirani zao Ukrainiane, wanaoteseka kutokana na vita" na kuwabariki kutoka moyoni mwake.