Papa:tuache kuwafanya wapembezoni mwa jamii wasionekane
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko ameomba kuombea watu wanaoishi pembezoni mwa jamii, katika hali ya maisha isiyo ya kibinadamu. Ameeleza hayo katika nia ya mwezi Septemba 2023, ili wasisahauliwe na taasisi na kamwe wasichukuliwe kama takataka. Katika video iliyochapishwa na Mtandao wa Kimataifa wa Nia za Maombi ya Sala ya Papa, anaonesha uchungu kwamba mtu asiye na makao anayekufa barabarani hatatokea kwenye ukurasa wa mbele wa Injini za utafutaji katika mtandao au habari. Na swali lililoelekezwa kwa kila mtu kutoka kwa Papa ni kwamba Je: Tufanyeje? kufikia kiwango hiki cha kutojali?"
Maneno ya Baba Mtakatifu Francisko katika lugha ya Kihispania yana ambatana na picha zinazoonesha watu wasio na makazi kwenye barabara za Canada, Marekani, Kenya, Cameroon na India, watoto wa mitaani ambao hutumia siku zao kuosha madirisha ya magari yaliyoegeshwa kwenye taa za trafiki huko Mtakatifu Salvador, na bado walemavu nchini Hispania, Ufilipino na Amerika ya Kati. Na pia kuna makazi duni karibu na skyscrapers huko Vancouver, Buenos Aires na Rio de Janeiro. Ni ubinadamu wa aina mbalimbali ambao wanaishi pembezoni, kulingana na Ripoti ya Umoja wa Mataifa (UN) asilimia 10% ya idadi ya watu duniani, zaidi ya watu milioni 700. Mbele ya ukweli huu, ndiyo mwaliko wa Papa Francisko ili kutafakari.
Tunawezaje kuruhusu utamaduni wa kutupa ambapo mamilioni ya wanaume na wanawake hawana thamani ikilinganishwa na faida ya kiuchumi; tunawezaje kuruhusu utamaduni huu kutawala maisha yetu, miji yetu, njia yetu ya maisha? Tunakuwa na shingo ngumu, kwa kuangalia pembeni ili tusione hali hiyo. Idadi iliyotolewa na Umoja wa Mataifa inawahusu watu walio katika hali ya umaskini uliokithiri, ambao wanatatizika kukidhi mahitaji ya kimsingi, kama vile afya, elimu na upatikanaji wa maji na usafi wa mazingira, wakati kuna takriban watu bilioni 1.6 wanaoishi katika mazingira duni ya makazi. Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) linafichua, hata hivyo, kwamba mtu mmoja kati ya wanane duniani ana shida ya matatizo ya akili na kwamba 16% ya idadi ya watu ulimwenguni wana ulemavu mkubwa. Jibu la haya yote ni kukukaribisha, kama alivyo sema Baba Mtakatifu Francisko.
“Tafadhali acheni kuwafanya wasioonekana walioko pembezoni mwa jamii, iwe kwa sababu ya umaskini, mada ya kulevya, magonjwa ya akili au ulemavu. Hebu tuzingatie mapokezi. Juu ya kuwakaribisha watu wote wanaohitaji. Kwani utamaduni wa kukaribisha, ukarimu, kuwezesha paa, kutoa makazi, kutoa upendo, kutoa joto la kibinadamu." Papa anatoa onyo hilo.
Ombi la Baba Mtakatifu ni kuhamasisha na sala, ambayo inaleta kile kilichofichwa moyoni kama alivyosisitiza Kardinali Michael Czerny, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kuhamasisha Maendeleo Fungamani ya Binadamu. Kwa sababu hii wale wanaoishi pembezoni, kama wasioonekana, lazima wapate nafasi katika maombi yetu: wako ndani ya moyo wa Kanisa: moyo wa nyama na si wa jiwe. Moyo wa jiwe hutupa; moyo wa nyama unakaribisha”. Kuhusu video ya Papa ya mwezi wa Septemba, Kardinali Czerny anabainisha kwamba “ Papa Francisko anajua nguvu ya kielimu ya sala na kwa njia hiyo anatualika kuendeleza utamaduni wa ukarimu”.
Na akinukuu mstari wa Biblia "Jiwe lililokataliwa na waashi limekuwa jiwe kuu la msingi" Kardinali liongeza kuwa "ujumbe huu unabaki kuwa na nguvu na wa kuaminika ikiwa hata leo hii tunatoa nafasi kwa wale waliokataliwa, ikiwa tunatambua utu usiofutika wa wale ambao alisulubishwa na uchumi usio na huruma, kutoka kwa kiburi au kutojali”. Kadinali Czerny pia alibainisha kwamba “kukaribisha ni zaidi ya kusaidia: ina maana ya kumleta mwingine kwenye kiwango chetu, kutafuta dada au kaka tuliyempoteza” na alieleza kwamba “katika maombi tunakuwa washiriki wa Mwili mmoja”.
Kwa upande wake Padre Frédéric Fornos, mkurugenzi wa kimataifa wa Mtandao wa Maombi ya Papa Ulimwenguni kote amebainisha kwamba, ili kutoa suluhisho dhahiri kwa mamilioni ya watu waliokataliwa ambao mara nyingi hupata tu kutojali, au hata kuudhika anachomba Papa ni mtazamo tofauti wa umaskini na kutengwa. Hii pia inamaanisha kusali, kwa sababu maombi hubadilisha mioyo yetu, kubadilisha macho yetu na kutufungua kwa wengine, hasa walio hatarini zaidi. Kwa hivyo tunahitaji kuomba, pamoja na Papa Fransisko, kwa ajili ya 'utamaduni wa kukaribisha yenye uwezo wa kuwakaribisha wale wote wanaohitaji, kutoa paa, nyumba, upendo na joto la kibinadamu, alihitimisha kueleza.