Tafuta

Papa na wawakilishi wa vituo vya usaidizi na Caritas:ni mikono inayogusa ukweli na shida za wengine

Katika siku yake ya tatu ya ziara ya Kitume nchini Ureno,Papa Francisko amewasifu wahudumu wa kujitolea kwa kuishi upendo kwa vitendo na kuwakumbusha thamani hata ya ishara ndogo kabisa za fadhili.Tabia yao ya kujitolea kwao,kwa kuchafua mikono yao kugusa ukweli na taabu za wengine,wanazalisha msukumo na maisha,

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko katika siku yake ya tatu nchini Ureno kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya 37 ya Vijana Duniani tarehe 4 Agosti, asubuhi amekutana na wawakilishi wa baadhi ya vituo vya misaada  na huduma (Caritasi) katika Kituo cha Parokia ya Serafina mjini Lisbon. Akiwahutubia watu wa kujitolea amesisitizia upendo kwa vitendo, huku akiwataka kuendelea kufanya maisha kuwa zawadi ya upendo na furaha. Papa alisema hakuna kitu kama upendo wa kufikirika. Upendo halisi, ule unaochafua mikono na kila mmoja wetu anaweza kujiuliza: je, upendo ninaohisi kwa kila mtu hapa, kile ninachohisi kwa wengine, ni halisi au cha kufikirika? Ninapopeana mikono na mtu mwenye shida na mgonjwa, pamoja na mtu aliyetengwa, baada ya kupeana mikono, je, ninafanya hivyo mara moja, ili wasiniambukize?

Papa amekutana na wawakilishi wa vituo vya kutoa msaada na Caritas
Papa amekutana na wawakilishi wa vituo vya kutoa msaada na Caritas

Papa kwa hiyo alitoa wito kwa watu binafsi kujiuliza ikiwa wanachukizwa na umaskini na akaonya dhidi ya kuishi, kile alichoelezea kama, maisha yaliyochujwa ambayo yapo tu katika mawazo yetu, lakini si katika hali halisi. "Ni maisha mangapi yasiyo na maana, ambayo hupitia maisha bila kuacha alama yoyote... badala ya kuishi kwa njia ambayo inaacha alama na inaweza kuwa msukumo kwa wengine"?. Papa ameendelea kusema kuwa kwa tabia yao, ya  kujitolea kwao, kwa kuchafua mikono yao kwa kugusa ukweli na taabu za wengine, wanazalisha msukumo na wnazalisha maisha, hivyo Papa aliwashukuru kwa hilo. Papa aliwashukuru kutoka ndani ya moyo wake, akiwaambia waendelee mbele na wasivunjike moyo. Na ikiwa watavunjika moyo, wanywe glasi ya maji na waendelee mbele.  Papa alitoa maoni haya bila kusoma hotuba iliyotayarishwa. Lakini katika hotuba iliyotayarishwa, alisema upendo ni chimbuko na lengo la safari yetu ya Kikristo na uwepo wa wahudumu wa upendo ni ukumbusho halisi wa upendo kwa vitendo.

Papa alikutana na wawakilishi wa huduma na Caritas
Papa alikutana na wawakilishi wa huduma na Caritas

Baba Mtakatifu alisema inatusaidia kukumbuka maana ya kile tunachofanya na jinsi tunavyopaswa kukifanya. Upendo, hutufanya tuwe na furaha si mbinguni tu, bali hapa duniani pia, kwa sababu hupanua mioyo yetu na huturuhusu kukumbatia maana ya maisha. Ikiwa tunataka kuwa na furaha ya kweli, basi, na tujifunze kubadilisha kila kitu kuwa upendo, kuwatolea wengine kazi yetu na wakati wetu, kusema maneno ya fadhili na kufanya matendo mema kwa tabasamu, kukumbatia, kwa kusikiliza, au hata tazama, aliwahimiza vijana  na wale waliokusanyika mbele yake, kuishi kwa njia hiyo. "Sote tunaweza kuifanya, na kila mtu anaihitaji, hapa na ulimwenguni kote. Papa kwa wahudumu hawa wa upendo alitoa wito wa kuishi, kusaidia na kupendana pamoja, miongoni mwa vijana na wazee, wenye afya na wagonjwa, wote pamoja".

Akizungumzia ugonjwa, Papa Francisko alisema tusijiruhusu kufafanuliwa na ugonjwa wetu, lakini badala yake tuufanye kuwa sehemu ya kujenga  mchango wetu kwa jamii iliyo pana. “Hatupaswi kujiruhusu kufafanuliwa na ugonjwa au ugumu, kwa maana hakuna hata mmoja wetu hasiye na  ugonjwa au tatizo: kila mmoja wetu ni zawadi, zawadi ya kipekee, pamoja na mapungufu yetu wenyewe, zawadi yenye thamani na takatifu kwa Mungu na kwa jumuiya ya Kikristo na ya kibinadamu.” Akisisitiza hitaji la kutenda kwa uthabiti, Papa Francisko aidha alisema, hii inahitaji kuzingatia hapa na sasa, kama wanavyofanya tayari, kwa jicho la undani na akili ya vitendo, ni fadhila nzuri za kawaida za watu wa Ureno. Ikiwa hatupotezi wakati wa kulalamika juu ya mambo, lakini badala yake tutazingatia kukidhi mahitaji halisi ya watu, kwa furaha na kuamini katika usimamizi wa Mungu, basi mambo ya ajabu yanaweza kutokea.

Watu wa kujitolea wawakilishi wa vituo vya huduma nchini Ureno
Watu wa kujitolea wawakilishi wa vituo vya huduma nchini Ureno

Kwa hiyo “endeleeni, kwa upole na wema, kuchukua changamoto, na aina  za zamani na mpya za umaskini, na kujibu kwa njia thabiti, kwa ubunifu na ujasiri,” aliwasihi Baba Mtakatifu. Papa alitoa wito kwa kuwa karibu na walio hatarini zaidi. Ingawa sisi sote ni dhaifu na tunahitaji, mtazamo wa huruma wa Injili hutuongoza kuona mahitaji ya walio hatarini zaidi. Vile vile inatusukuma kuwatumikia maskini, waliotengwa, waliopembeni  watoto wadogo, wasio na ulinzi  wale wanaopendwa zaidi na Mungu, ambao alijifanya kuwa maskini kwa ajili yao, wao ni hazina halisi ya Kanisa, Papa alikumbusha. Kwa hiyo “Kupenda ni zawadi kwa wote! Tukumbuke: o amor é um presente para todos!". Wacha tuyarudie pamoja: o amor é um presente for todos!” Wacha tupendane kwa njia hiyo! Papa alisema, Tafadhali, endelea kufanya maisha kuwa zawadi ya upendo na furaha." alihitimisha.

Papa na wawakilishi wa vituo vya kutoa huduma na Caritas
04 August 2023, 12:22