Tafuta

2023.08.27 Vidonge vya dawa za kulevya. 2023.08.27 Vidonge vya dawa za kulevya. 

Papa,Kongamano la 60 Kimataifa la uchunguzi wa dawa za kulevya:sikiliza kilio cha wadhaifu

Papa Francisko katika ujumbe wake kwa washiriki hao walioanza Agosti 27-31,Roma,anaeleza wasiwasi wa ongezeko la matumizi ya dawa za kulevya miongoni mwa barbaru na vijana.'Mtu hawezi kubaki kutojali,nyuma ya ulevi kuna uzoefu halisi,historia za upweke,ukosefu wa usawa,kutengwa na ukosefu wa ushirikiano.'

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Dominika tarehe 27 Agosti 2023, ametuma ujumbe wake kwa washiriki wa Kongamano la 60 Kimataifa la Madaktari  wa Uchunguzi wa Madawa ya kulevya linaolendelea Roma kuanzia tarehe 27 Agosti na litafungwa  tahere 31 Agosti 2023. Katika ujumbe huo Baba Mtakatifu amewashukuru kwa jitihada, muda na nguvu wanayoiweka katika kuzuia na kupambana dhidhi ya madawa ya kulevya, hata kwa njia ya siku za mafunzo na uhamasishaji wa utamaduni kuhusu mada hiyo ambayo inaona kuwahusisha idadi kubwa ya sura za kitaaluma na baadhi wakiwa vijana watafiti. Hali ya matumizi mabaya ya madawa ya kulevya na kisaikolojia inaendelea kuamsha wasiwasi na duku duku hasa kutokana na ukuaji wa matumizi uliorekodiwa kati ya vijana barubaru na rika la vijana na  kwa hiyo, kutokana na ongezeko la mauzo ya madawa ya kulevya kwenye viwanja vya kidigital" vya mtandao wa giza. Barubaru na vijana, kama tunavyojua, Papa amesema ni hatua dhaifu sana katika maisha ya kila mtu, inayooneshwa na mabadiliko makubwa katika kiwango cha mwili, kihemko na kijamii. Kinachoongezwa na hilo ni ukweli kwamba jamii zetu za sasa ni dhaifu katika mambo mengi na zinaoneshwa na ukosefu wa usalama wa kimsingi.

Ni muhimu kuendeleza uchambuzi na kutafuta mbinu ya kuzuia

Kutokana na  hilo  Baba Mtakatifu anabainisha kwamba mtu anaweza baadaye kuvutwa kwenye utaftaji wa kulazimishwa wa uzoefu mpya,  kwa sababu ya hitaji la kujipima na mpya, hamu ya kuchunguza haijulikani, lakini pia kuna kunyamazisha hofu ya kuhisi kutengwa na hitaji la kushirikiana na wenzao. Haya ni mambo hatari sana, ambayo yanaweza kusababisha vijana kufanya uchaguzi na tabia hatari, kama vile matumizi ya vitu vinavyoathiri akili na matumizi mabaya ya pombe, au uwezekano wa kukimbilia katika hali mbaya, zote mbili na halisi. Yote hii inawakilisha ardhi yenye rutuba kwa matumizi ya vitu vya sumu. Kati ya hizi, ni dawa mpya za kitoksini(NPS) na ambazo ni hatari zaidi, zinazowakilisha shida kubwa na ngumu katika mazingira ya sasa kwenye mzuko wa madawa na soko linalokua kwa kasi na athari zisizo na uhakika za kitoksini na athari mbaya kwa afya ya umma. Urahisi wa kurekebisha dawa hizi kuwa kemikali basi huruhusu uhalifu uliopangwa, kukwepa udhibiti wa kisheria, na kufanya iwe vigumu zaidi kutambua misombo haramu.

Vijana wengi wanatumia NPS dawa hizi bila kujua hatari yake

Vijana wengi hutumia hizi (NPS) bila kujua jinsi ilivyo hatari sana. Kwa hiyo, ni muhimu sana kuendeleza mbinu za uchambuzi, pamoja na hatua za kuzuia zinazolenga kudhibiti  kuenea kwake na kuhimiza mipango ya kutosha ya matibabu. Pia tunashuhudia ongezeko la usambaaji wa dawa za kusisimua misuli, hasa katika nyanja za ushindani na michezo. Utumiaji wa vitu vya kuimarisha utendaji katika michezo hudhihirisha shauku ya kufikia malengo muhimu na matokeo ya utendaji wa juu kwa gharama zote. Kwa wazi, jambo hilo ni kiashiria cha kitu ambacho kina mizizi zaidi, ambayo ina maana umuhimu wa kutafakari juu ya jamii yetu leo hii, iliyojaa utamaduni wa ufanisi na tija, ambayo hairuhusu kusita na kushindwa. Haja ya kuonekana kila wakati kulingana na matarajio, kuonesha kwa nje taswira ya mtu mzuri na aliyefanikiwa, ambaye udhaifu zaidi ya yote katika kutaka kuondoa inakuwa kikwazo kisichoweza kushindwa kwa utafutaji wa maendeleo kamili ya mwanadamu.

Kusikiliza kilio cha walio dhaifu

Kwa hivyo, wakiwa wamechanganyikiwa Baba Mtakatifu anabainisha na mara nyingi bila mahali pa kukimbilia vijana wengi hufuata udanganyifu wa kupata matumizi ya madawa ya kulevya  kwa mawazo ya kusimamisha uchungu na ukosefu wa maana: yaani matumaini ya bure ambalo huondoa uchovu wa kuwa na huwepo, mara nyingi hujificha chini ya kivuli cha tamaa ya kutoroka na kujifurahisha. Zaidi ya hayo, hatuwezi kusahau kwamba nyuma ya kila mlevi kuna uzoefu halisi, wa historia za upweke, ukosefu wa usawa, kutengwa, ukosefu wa ushirikiano na ufungamanishwaji. Baba Mtakatifu amesisitiza kuwa “Hatuwezi kuwa tofauti na hali hizi. Bwana Yesu alisimama, akakaribia, akaponya majeraha. Sisi pia tunaitwa kutenda katika mtindo wa ukaribu wake, kusimama mbele ya hali ya udhaifu na maumivu na kujua jinsi ya kusikiliza kilio cha upweke na uchungu”. Ni matumaini ya Baba Mtakatifu  kuwa watakuwa na matokeo ya kazi yao yanayochangia utambuzi wa njia za elimu, matibabu na urekebishaji zenye uwezo wa kuzuia na kupambana na janga la dawa za kulevya, kukuza mifano mbadala ya kiutamaduni na kuhimiza utafutaji wa sababu za kuishi katika wale hasa vijana ambao wamewapoteza. Baba Mtakatifu akiwatakia kazi yao ya kisayansi na kiutamaduni iweze kuzaa matokeo wanayotaka, amewakabidhi kwa maombezi ya Maria, Mama anayejali na amewabariki  kutoka moyoni  mwake na kuhitimisha.

Ujumbe wa Papa kwa watalam wa masuala ya Madawa ya Kulevya
27 August 2023, 18:15