Papa atia saini katika kitabu cha heshima:Nchi iendelee na upeo wa udugu
Vatican News.
Katika ziara ya Papa Francisko nchini Ureno, akiwa amefika kumtembelea Rais kwa faragha katika Jumba la Taifa la Belém nchini Ureno, Baba Mtakatifu, Jumatano tarehe 2 Agosti 2023 e ameandika katika kitabu cha Heshima. Katika maneno hayo yanasomeka kuwa: “Kama mujaji wa matumaini nchini Ureno, ninasali na kutumaini kwamba nchi hii yenye moyo kijana itaendelea kuelekeza katika upeo wa udugu; Lisbon, ni jiji la kukutana, huhamasisha njia za kushughulikia maswala makubwa ya Ulaya na ulimwengu kwa pamoja."
Na katika fursa hiyo ya ziara ya heshima katika ukumbi wa Ikulu ya Taifa Belém, Papa Francisko kwa kubailishana zawadi alikabidhi picha ya nishani ya kumbukumbu ya safari hiyo na medali ya dhahabu ya Upapa kwa Rais wa Jamhuri ya Ureno.