Papa,Mongolia,safari kati ya nyika na Ger ili kukumbatia kundi dogo la Kikatoliki!
Na Salvatore Cernuzio na Angella Rwezaula, - Vatican.
Safari kati ya nyika kubwa na (Ger) nyumba ya kiutamaduni ndogo, ambayo ni kama hema za kawaida zilizo na nguzo za mbao na kuta, ikiwa ni ishara ya maisha ya kuhamahama ya idadi ya watu. Kwa hiyo ni shauku na amani ya idadi ya watu, na wito kwa watu wengine na kwa ajili ya kutunza mazingira baada ya maporomoko ya madini hatari. Ni idadi ya watu ambao 0.02% yao wanadai kuwa Wakatoliki, kutoka katika kundi dogo waliozaliwa upya baada ya kuanguka kwa ukomunisti mnamo 1992. Kwa hivyo mkurugenzi wa Ofisi ya Vyombo vya Habari, Dk. Matteo Bruni, alielezea hija ya Kitume ya Baba Mtakatifu Francisko huko Mongolia, ambapo ataondoka tarehe 31 Agosti na atabaki hadi Septemba 4, akitembelea mji mkuu tu Ulanbaatar nchini humo. Kwa hiyo hii ni ziara ya 43 ya kitume ya Papa wa Argentina, na Upapa wa 61 wa Papa wa kwanza katika Nchi hii ya Asia kati ya Urussi na China, nchi ya mwisho ambayo Jorge Mario Bergoglio(Papa Francisko) atavuka kwa ndege ya nje na kurudi na ambayo telegram kwa Rais Xi Jinping inatarajiwa, kama ilivyoripotiwa na Dk Bruni.
Kwa njia hiyo eneo la Mongolia ni ishara ya kijiografia katika wakati wa kihistoria ulioadhimishwa na vita vya Ukraine ambavyo pengine vitakuwa na athari katika hotuba ya Papa mnamo tarehe Mosi Septemba kwa mamlaka ya kiraia, mojawapo ya hotuba tano zote katika Kiitaliano, ambazo Papa Francisko atatoa katika siku tatu za kusafiri, zenye sifa ya kukutana na hali halisi mbalimbali za kitaasisi na kijamii za nchi. Hata hivyo, moyo wa safari nzima utakuwa mkutano na jumuiya ndogo ya Wakatoliki, waamini wapatao 1500. Kwa hiyo, “Papa anakwenda Mongolia kuzungumza nao hasa, atashughulikia maneno ya kutia moyo na matumaini kwa ukweli huu mzuri ambao hutoa muhimu wa mchango katika nyanja za maisha ya binadamu,” kwa mujibu wa Dk. Bruni.
Na pia kukumbuka mizizi ya Kanisa hili ambalo, kiukweli, linaishi asili yake leo hii hata kama kuna mawasiliano na ulimwengu wa Kilatino mapema kama 1200 na pia kubadilishana barua kati ya mtoto wa Genghis Khan na Papa Innocent IV. Uteuzi wa Askofu wa kwanza ulianza mwanzoni mwa karne ya nne, wakati ufalme wa Mongolia ulijumuisha sehemu ya China; kisha kwa karne nyingi uwepo wa Wakristo katika eneo hilo ulikaribia kupungua, hadi ulipotoweka kabisa wakati wa miaka ya utawala wa kikomunisti. Tangu mwaka 1992, Kanisa “lilirejeshwa tena na kualikwa kwenye uwepo, ambapo limetiwa nguvu tena katika miaka thelathini iliyopita na kazi kubwa ya wamisionari, kwanza kabisa Wamisionari wa Consolata, Shirika ambalo lina Kardinali wa kwanza na wa pekee wa Mongolia Giorgio Marengo, ambaye ni Msimamizi wa kitume wa Ulanbaatar, ambaye alipokea Kofia ya ukardinali mnamo 2022.
Kwa kuzingatia historia hii, lakini pia sasa ya Kanisa hili dogo lililoenea sana katika jamii kiasi kwamba makubaliano kati ya Vatican na Mongolia juu ya kazi ya Wakristo yanasomwa katika miezi ya hivi karibuni, Misa itaadhimisha mchan tarehe 3 Septemba katika Steppe Arena. Kwa waamini1,500 wanaoishi Mongolia, 90% katika mji mkuu, pia kutakuwa na waamini elfu nyingine kutoka nchi mbalimbali jirani. Miongoni mwao: Urussi,China, Thailand, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Azerbaijan, Vietnam. Pia siku ya Dominika tarehe 3, Papa ataongoza tukio la kiekumeni na la kidini katika ukumbi wa michezo wa Hun: wawakilishi wa shamanism, Shintoism, Buddhism, Uislamu, Uyahudi, Uhindu na madhehebu mengine watashiriki. Ishara ya wito wa kuishi pamoja kwa amani ambayo, alisisitiza Dk Bruni, ina sifa ya watu wa Kimongolia kwa miongo kadhaa. Waangalizi wa serikali na wawakilishi wa ulimwengu wa vyuo vikuu pia watakuwepo katika mkutano huo, alisema msemaji wa Vatican, ambaye alijibu maswali kutoka kwa baadhi ya waandishi wa habari juu ya uwezekano wa mvutano kati ya China juu ya mkutano na wawakilishi wa Ubuddha wa Tibet, ikiwa ni pamoja na mtoto aliyezingatiwa kuzaliwa upya akiwa wa kumi wa Buddha, pamoja na uwezekano wa mkutano wa faragha na waamini wa Kirusi na Kichina baada ya Misa.
Matteo Bruni, akifafanua kuwa kwa sasa hakuna mikutano iliyotengwa,ya kifaragha alielezea kuwa vikundi vyote vya kidini vitakuwepo kwenye hafla ya kiekumeni na ya kidini. Kuhusu marejeo yanayowezekana kwa China iliyo karibu, mkurugenzi wa Ofisi ya Vyombo vya Habari alikumbuka maneno ya Papa katika sala ya Malaika ya mwisho Dominika tarehe 27 Agosti 2023 ambapo “Papa alikuwa wazi sana Doniminia kwamba ‘ninakwenda Mongolia, ninataka mkutano huo ambao nimeutarajia kwa furaha na heshima kubwa, nina hamu ya kukutana na watu”. Kwa hisyo “Nisingeongeza kitu kingine chochote. Safari iko Mongolia”. Akionesha mpango huo kwa undani, aliripoti kwamba Papa ataondoka uwanja wa ndege wa Fiumicino mnamo tarehe 31 Agosti saa 12.30 jioni na kwa masaa 9 na nusu ya kuruka juu, miongoni mwa mengine atapitia juu ya Georgia, Azerbaijan na China. Njia iliyoanzishwa haijumuishi Urussi. “Kwa kawaida njia huchaguliwa kulingana na ile ambayo ni rahisi zaidi kwa wakati kama huo. Sifahamu sababu nyingine zozote,” msemaji wa Vatican alisema. Papa atatua Ulanbaatar katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Chinggis Khaan, akikaribishwa na waziri wa mambo ya nje na mwanamke kijana ambaye atampatia kikombe cha mtindi mkavu, zawadi ya kawaida ya nchi hiyo. Siku ya kwanza itawekwa kwa uteuzi wa taasisi: asubuhi na mamlaka ya kiraia, ikiwa ni pamoja na Rais Ukhnaagiin Khürelsükh na Waziri Mkuu; mchana na maaskofu, mapadre, wamisionari watawa wa kike na kiume.
Mkutano huu wa mwisho utafanyika katika Kanisa kuu, lililojengwa katika karne ya 20 na muundo unaofanana na Ger, ambapo kuna sanamu ya Maria iliyopatikana kwa mwanamke mmoja kwenye takataka miaka iliyopita, kisha akatawazwa na kuheshimiwa kama Mama wa Mbingu. Kardinali Marengo aliiweka wakfu Mongolia kwake mnamo 2022. Mwanamke aliyepata sanamu hiyo kwenye takataka atamkaribisha Papa katika Kanisa kuu, lililogawanywa katika sakafu mbili, pamoja na mwanamke wa Kimongolia ambaye atatoa jagi la maziwa lililofunikwa kwa kitambaa cha bluu, zawadi nyingine ya kawaida. Mbali na mikutano ambayo tayari imetajwa, ambapo Papa atapanda gari la gofu, katika siku ya mwisho Papa Francisko atabariki na kuzindua Nyumba ya Huruma, jumba la shule lililotelekezwa la watawa ambalo sasa limeanzishwa ili kuwapa masikini makazi, wasio na makazi, wahamiaji na waathiriwa wa unyanyasaji wa nyumbani. “Ni vyema kwamba Papa atahitimisha safari yake katika mahali hapo pa upendo” alifafanua Dk. Bruni.
Tarehe 4 Septemba 2023, katika siku ya mwisho ya Ziara ya kitume, Papa Fransisko atazindua muundo uliozaliwa kutokana na hisia za viongozi wa Kanisa mahalia na pia kuungwa mkono na usaidizi ... Katika safu ya upapa, Kadinali Luis Antonio Tagle, Mwenyekiti shirikishi wa sehemu ya Uinjilishaji wa kwanza na Makanisa mapya na kwa ajili ya Uinjilishaji; Kardinali Kurt Koch, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la luhamaisha Umoja wa Wakristo; Kardinali Miguel Angel Ayuso, Mwenyekiti wa Baraza la kipapa la kwa ajili ya mazungumzo ya kidini. Pia katika ujumbe huo alikuwa Silvina Peréz, mwanamke wa kawaida, mratibu wa toleo la Kihispania la Osservatore Romano.