Tafuta

Papa huko Fatima,Comastri:Vijana fungueni mioyo !

Mkuu wa Mstaafu wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro,Kadinali Comastri ametoa tafakari kuhusu hatua ya Baba Mtakatifu katika Madhabahu ya Maria mnamo tarehe 5 Agosti 2023 na kuwaeleza vijana kuwa “Sikilizeni Bikira na mrudi nyumbani mkisema “sasa ninataka kuanza maisha yenye upatano na zaidi ya Kikristo."

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Rozari ni sala ya ajabu anashangaa Mkuu Mstaafu wa  Kanisa kuu la Mtakatifu Petro, Kardinali Angelo Comastri, wakati akitafakari kwenye Tevesheni ya “ Telepace” kuhusu umuhimu wa ziara ya Papa  Francisko kwenda kwenye Madhabahu ya Fatima Jumamosi tarehe 5 Agosti 2023, ikiwa ni sehemu ya Siku ya Vijana Duniani huko  Lisbon.  Kwa mujibu wa Mwandishi wa habari wa Vatican, Eugenio Bonanata alibainisha kwamba Kardinali Comastri alisema “Ni jambo zuri kwamba Fransisko na vijana wa ulimwengu watakusanyika hapo kusali rozari, ambayo inaunda hija katika maisha ya Yesu akifuatana na Maria. Wakati huo huo, kusali rozari pia ni ubora tunaoupata wa historia na nafasi ambayo tunamfungulia Mungu ili aweze kunyoosha mapito yetu.” Na hii ndiyo sehemu ya kuanzia ya kuwashughulikia wale wote ambao wamechagua kwenda mahali palipojaa imani iliyo na alama za kuonekana kwa Bikira katika siku za hivi karibuni.

Siri ya Ujumbe wa Maria 

Ushauri huu bilashaka unahusiana na kumbukumbu za kibinafsi za Kadinali ambaye aliibua kwa hisia ya ziara ya mahali Patakatifu aliyoifanya  mnamo tarehe 13 Mei  2000 pamoja na Mtakatifu Yohane Paulo II wakati wa sehemu ya tatu ya siri ya Fatima iliposomwa. Kando ya hafla hiyo, Kardinali Comastri alikuwa mikononi mwake nakala ya ujumbe ambao Mama Yetu alimpatia Sr. Lucia na hivyo  mnamo 1987 kuhusu ushindi wa moyo safi wa Maria. Kweli, Bikira aliomba mchango wa kila mtu kando yake kwa kusudi hili. “Ikiwa tunataka kucheza nafasi ya watoto lazima tumsikilize Mama” alielezea kardinali 

Mpango wa Mungu

Ndiyo maana katika kukabiliana na uhamasishaji wa vijana kwa ajili ya mkutano wa ulimwengu huko Lisbon, Kardinali Comastri alirudia kusema kwamba haitoshi kukusanyika na labda kufanya hija kwenye Madhabahu ya Maria. “Tunahitaji kusikiliza, kukusanya na kutafakari ujumbe wa Mama Yetu wa Fatima”. Hatimaye hii ina maana ya kutafakari Maandiko na kuelewa kwamba uhuru kinyume na vile wengine wanavyofikiri si kufanya kile mtu anataka. “Unajumuisha kusema ndiyo, kama Maria, na kufafanua hasa kwa kuwalenga vizazi vipua tena “Tazama, kuna mpango wa Mungu kwa ajili yenu nyote pia. Tunahitaji kujua kwa sababu hii ndiyo njia ya kuwa na furaha na tuache nyuma yetu mtaro wa kheri”.

Maneno ya Mama Teresa

Kulingana na kuhani mkuu aliyestaafu, kinachohitajika zaidi kwa wale wanaoshiriki katika Siku ya Vijana Duniani(WYD) ni ufunguzi wa moyo wa kuanza na Yesu kwenye njia ya furaha. “Lazima turudi nyumbani tukisema: sasa ninataka kuanza maisha madhubuti na zaidi ya Kikristo. kwa kurejea y kwa Mama Teresa wa Calcutta  Kardinali hawezi kuepukika kusisitiza haja ya kuchukua Injili kwa uzito.  kwa hiyo alisema “Mtakatifu  Teresa mara nyingi alisema kwamba Injili inaweza kuishi na ni kwa kuishi tu maisha yanapata nuru. Bila moyo wazi ni vigumu. Ikiwa moyo umefungwa tunaweza hata kuwasha taa elfu, lakini hatutaona chochote.” alihitimisha.

01 August 2023, 16:44