Tafuta

Papa:Ulaya ina jukumu la amani mashariki,Mediteranea,Afrika&Mashariki ya Kati

Katika hotuba ya I nchini Ureno,katika mkutano na mamlaka,mashirika ya kiraia na ya kidiplomasia,Papa ameomba amani na kutumaini kuwa WYD itakuwa msukumo kwa bara la Ulaya katika jukumu la kuleta amani katika sehemu ya mashariki.Sera za siasa lazima zirekebishe usawa wa kiuchumi,kuwekeza katika familia na kutunza mazingira.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu baada ya kufika Nchini Ureno, tarehe 2 Agosti 2023 na kupokelewa kwa afla ya heshima  katika Jumba la Kitaifa la  Belem, alimtembelea kwa faragha Rais wa Jamhuri ya Ureno na baadaye kufuatia mkutano kwa Serikali, vyama vya kiraia pamoja na wanadiplomasia wanaoziwakilisha nchi na mashirika ya Kimataifa katika nchi ya Ureno.  Katika hotuba yake ameanza  salamu na kumshukuru Rais kwa makaribisho na kwa maneno ya hotuba yake. Ni furaha yake kuwa Lisbon, mji wa kukutana ambao unawakumbatia watu mbali mbali na tamaduni ambazo zinageuka kwa siku hii kuwa za uliwemgu zaidi; zinageuka kwa  maana nyingine mji mkuu wa ulimwengu. Mjuu nkuu wa wakati ujao kwa sababi vijana ni wa wakati ujao.

Siku ya vijan Ureno
Siku ya vijan Ureno

Kile kinachofaa katika tabia ya wingi wa watu na wingi wa tamaduni, kwa kufikiria  mtaa mmoja wa Mauraria mahali ambapo  wanaishi kwa maelewano watu kutoka zidi ya nchi sitini, na kuonesha sura ya Mji Mkuu wa Ureno ambayo inajenga mizizi juu ya  shauku ya kijifungulia ulimwengu na kuigunduaa kuelekea upeo mpana zaidi. Baba Mtakatifu ameeleza juu ya eneo hilo kwamba sio mbali na  Cabo ya Rocca ambayo imechongwa sentesi ya mshairi maarufu wa mji huo. Kwa miongo mingi ilikuwa inaaminika kuwa ndio mwisho wa dunia, na kwa namna nyingine ni kweli: Kwani amesema “Tunajikuta mpakani mwa ulimwengu kwa sababu katika Nchi hii inapakana na Bahari  ambayo inatengenisha mabara. Lisbon inakumbatia na ina manukato. Bahari ambayo ni kitu kikubwa cha eneo ni mwaliko katika roho ya kila mreno. Mbele ya bahari, wareno wanatafakari juu ya nafasi kubwa ya roho na juu ya maana ya maisha katika ulimwengu. Hata hivyo  Baba Mtakatifu kwa kuacha ashangazwe na alipenda  kutoa baadhi ya mawazo.

Papa amesema kwa mujibu wa imani za kale, Bahari ni mwana wa mbingu ukubwa wake unapelekea wafu kutazama juu na kuinuka kuelekea yasiyo isha. Lakini wakati huo huo, Bahari ni mwana wa ardhi (Gea) ambaye anakumbatia na anaalika hivyo  kuelekeza huruma ndani ya ulimwengu tunaoushi; kwa hiyo Lisbon ni mji wa  wa maji,  ambao unaalika umuhimu wa upamoja kufikiria mipaka kama sehemu za kukutana. Na sio kama mipaka ambayo inagawanya. Papa amesema inavyotambuliwa kuwa leo hii masuala makubwa ni ya kiulimwengu na zaidi mara nyingi tunafanya uzoefu wa dhati  katika kujibu hasa kwa sababu mbele ya matatizo ya pamoja ya ulimwengu yamegawanywa au kidogo hayatoshi, kutokuwa na uwezo wa kukabiliana pamoja kile ambacho kinaweza kuleta mgogoro kwa wote. Utafikiria kuwa haki za sayari, vita, migogoro ya tabianchi, na uhamiaji vinakimbia zaidi ya uwezo na mara nyingi kwa utashi, wa kukabiliana pamoja hizi changamoto.

Hotuba ya Papa kwa viongozi wa Nchi ya Ureno
Hotuba ya Papa kwa viongozi wa Nchi ya Ureno

Papa amesema, Lisbon inaweza kushauri   kubadili hatua. Hii ni kwa sababu mnamo 2007 ilitiwa saini Mkataba wa mapinduzi ya Umoja wa Ulaya. Huo ulikuwa unathibitisha kuwa Umoja unapaswa kuhamasisha amani, thamani zake na ustawi wa watu ( Mkataba wa Ulaya ibara. 1,4/2.1); Lakini unakwenda zaidi yake.  Kwa kuwa katika uhusiano na ulimwengu, unachangia kwa amani, kwa usalama, kwa maendeleo endelevu ya ardhi, ya mshikamano na kulingana na upamoja, kati ya watu, biashara uria, na sawa, kuondoa umaskini, na kulinda haki za binadamu. Sio kwa maneno, lakini hatua muhimu kwa ajili ya safari ya jumuiya ya Ulaya, iliyochongwa katika kumbukumbu ya mji huu. Hapa kuna roho ya jumla, iliyohuishwa na ndoto ya Ulaya ya umoja wa pande nyingi zaidi kuliko muktadha wa Magharibi tu.”

Neno la pili lililojadiliwa kwamba jina la Ulaya linatokana hasa na neno ambalo linaelekeza mwelekeo wa magharibi. Ni hakika kinyume kwamba Lisbon ni mji mkuu zaidi wa magharibi ya bara la Ulaya. Wenyewe unatualika kwa hili  kwa ulazima wa kufungua njia za kukutana zaidi kama Ureno inavyofanya tayari, hasa na Nchi nyingine zinazopakana nazo kwa lugha yenyewe. Ni matumaini kwamba Siku ya vijana duniani iwe kwa “bara la kale  msukumo wa ufunguzi wa ulimwengu wote." Kwa sababu Ulaya, ya Ulaya ya kweli, ulimwengu unahitaji: unahitaji jukumu lake la kuwa daraja, la amani katika sehemu yake ya mashariki. Katika Mediterrania, katika Afrika na katika Mashariki ya Kati. Kwa njia hiyo Ulaya itaweza kupelekea ndani mwake mambo ya kimataifa, umuhimu wake asili, msimamo katika karne iliyopita wakati kutika katika mgogoro mkubwa wa kidunia, ulifanya kuwacha cheche za upatanisho, kwa kuibua ndoto ya kujenga ya kesho na adui wa jana, kwa kuanzisha michakato ya mazungumzo  na ya ujumuishi,  kwa kukuza diplomasia ya amani ambayo inazima migoro na kupunguza mivutano, kuweza kufahamu dalili hafifu za kustarehesha na kusoma kati ya mistari iliyopotoka zaidi.

Kuna maaskofu na makardinali wengi Ureno katika WYD
Kuna maaskofu na makardinali wengi Ureno katika WYD

Baba Mtakatifu Francisko amekazia kusema kuwa "Katika bahari ya historia, tunasafiri katika hali ya dhoruba na kuna ukosefu wa njia za ujasiri za amani. Kuangalia kwa upendo wa dhati kwa Ulaya, katika roho ya mazungumzo ambayo ni tabia, mtu anaweza kuuliza: unasafiri kuelekea wapi, ikiwa hautoi njia za amani, njia za ubunifu za kumaliza vita huko Ukraine na mizozo mingi ambayo inamwaga damu duniani? Na tena, kupanua uwanja: ni njia gani unayofuata, Magharibi? Teknolojia yako, ambayo imeashiria maendeleo na utandawazi wa dunia, haitoshi yenyewe; hata kidogo zaidi silaha za kisasa hazitoshi ambazo haziwakilishi uwekezaji kwa siku zijazo, lakini umaskini wa mtaji wa kweli wa kibinadamu, ni ule wa elimu, huduma za afya, hali ya ustawi. Inatia wasi wasi hasa tunaposoma kuwa katika maeneo mengi wanaendelea kuwekeza fedha katika silaha badala ya wakati ujao wa watoto. Mimi ninaota ndoto ya Ulaya, moyo wa Magharibi, ambao unaweka ustadi wake kwa matumizi mazuri katika kuzima milipuko ya vita na taa za matumaini; Ulaya ambayo inajua jinsi ya kugundua upya nafsi yake ya ujana, inaota juu ya ukuu wa yote na kwenda zaidi ya mahitaji ya haraka; Ulaya ambayo inajumuisha watu na watu binafsi, bila kufukuza nadharia na ukoloni wa kiitikadi.

Bahari kubwa iliyotanda ya maisha inaalika asili za maisha. Katika ulimwengu ulionendelea wa leo, imekuwa muhimu kipaumbele cha kutetea maisha ya binadamu ambayo yamekuwa hatarini kutikana kile kiitwacho kutumia ambao hutumiwa na kubaguliwa. Papa amefikiria watoto wengi wasio zaliwa na wazee walioacha peke yao, ugumu wa kukaribisha, kulinda na kuhamasisha na kufungamanisha yule anayekuja kutoka mbali na kubisha milango, upweke wa familia nyingi zenye matatizo katika kuweka katika dunia na kukuza watoto. Vile vile Papa amesema hapa pia mtu angelazimika kusema: unasafiri kuelekea wapi, Ulaya na Magharibi, na taka za zamani, kuta za waya ya miiba, mauaji ya baharini na vitanda vya watoto tupu? Unakwenda wapi ikiwa, unakabiliwa na ubaya wa kuishi, unatoa tiba za haraka na zisizo sahihi, kama vile ufikiaji rahisi wa kifo, suluhisho rahisi ambalo linaonekana tamu, lakini kwa kweli ni chungu zaidi kuliko maji ya bahari?

Lisbon iliyokumbatiwa bahari lakini inatupatiasababu za kutumaini. Bahari ya vijana ambayo wamefika katika makaribisho ya mji huu. Hivyo  Papa amependa kuwashukuru kwa kazi kubwa na ukaribu wa jitihada za Ureno kwa kukaribisha tukio hili kubwa mno,  lakini lenye matunda ya matumaini. Kama misemo ya sehemu hiyo isemavyo: “ Karibu na vijana huzeeki”. Vijana wamekuja  kutoka ulimwengu mzima ambao wanakuza shauku ya umoja, yaani ya  udugu, wanatuchangamotisha kutimiza ndoto zao za wema. Hawapo njiani wakipaz sauti  kwa hasira, lakini kwa kushirikishana tumaini ya Injili. Na ikiwa leo kuna hali ya maandamano na kutoridhika katika sehemu nyingi, kuna ardhi yenye rutuba ya nadharia za utaifa na njama. Kwa hiyo  Siku ya Vijana Duniani ni fursa ya kujenga pamoja. Inafufua hamu ya kuunda mambo mapya, kwenda baharini na kusafiri pamoja kuelekea siku zijazo. Baadhi ya maneno ya ujasiri ya Pessoa yanakuja akilini: "Kusafiri ni muhimu, kuishi sio lazima [...]; kinachohitajika ni kuunda" (Navegar). Kwa hivyo wacha tujishughulishe na ubunifu ili tujenge pamoja! Ninafikiria maeneo matatu ya ujenzi ya matumaini ambayo sote tunaweza kufanya kazi pamoja: mazingira, siku zijazo, udugu, Papa amesema.

Papa ameanza na  Mazingira. Ureno inashiriki na Ulaya juhudi nyingi za mfano kwa ajili ya ulinzi wa kazi ya uumbaji. Lakini tatizo la kimataifa linasalia kuwa kubwa sana: kwani bahari zina joto kupita kiasi na vilindi vyake vinadhihirisha ubaya ambao tumechafua makazi yetu ya pamoja. Tunageuza hifadhi kubwa ya maisha kuwa dampo za plastiki. Bahari inatukumbusha kuwa maisha ya mwanadamu yameitwa kuoanisha mazingira makubwa kuliko sisi, ambayo lazima yatunzwe kwa uangalifu, tukifikiria vizazi vichanga. Je, tunawezaje kusema tunawaamini vijana tusipowapa nafasi nzuri ya kujenga maisha yao ya baadaye?

Furaha ya vijana kumuona Papa
Furaha ya vijana kumuona Papa

Wakati ujao ni uwanja wa pili wa ujenzi. Na siku zijazo ni vijana.  baba Mtakatifu amesisitiza kuwa "Lakini mambo mengi yanawakatisha tamaa, kama vile ukosefu wa kazi, kasi ya kuzamishwa kwao, kuongezeka kwa gharama ya maisha, ugumu wa kupata nyumba na, wasiwasi zaidi, woga wa kuanzisha familia na kuzaa watoto. Katika Ulaya na, kwa ujumla zaidi, katika nchi za Magharibi, tunashuhudia awamu ya kushuka ya mzunguko wa idadi ya watu: maendeleo inaonekana kuwa swali kuhusu maendeleo ya teknolojia na starehe za watu binafsi, wakati ujao unahitaji kukabiliana na kupungua kwa kiwango cha kuzaliwa na kupungua kwa hamu ya kuishi. Siasa nzuri inaweza kufanya mengi katika hili, inaweza kuzalisha matumaini. Kiukweli, haijaitwa kushika madaraka, bali kuwapa watu uwezo wa kutumaini. Inaitwa, leo kuliko wakati mwingine wowote, kusahihisha kukosekana kwa usawa wa kiuchumi wa soko linalozalisha mali lakini haligawi, na kuzitia umaskini roho kwa rasilimali na uhakika. Inaitwa kujigundua tena kama jenereta ya maisha na utunzaji, kuwekeza kwa mtazamo wa mbali katika siku zijazo, katika familia na kwa watoto, kukuza miungano ya vizazi, ambapo siku za nyuma hazifutikani kwa swipe katika sifongo, lakini vifungo kati ya vijana. watu na wazee. Lazima tuchukue hili tena: mazungumzo kati ya vijana na wazee".

Baba Mtakatifu amsema kuwa hisia ya Kireno inakumbuka hili, ambalo linaonesha kujutia, kukata tamaa ya kutokuwepo vizuri, ambayo huzaliwa upya ikia  katika kuwasiliana na mizizi ya mtu. Vijana lazima wapate mizizi yao kutoka kwa wazee. Kwa maana hii, elimu ni muhimu,ambayo haiwezi kutoa mawazo tu  ya kiufundi ili kuwepo maendeleo ya kiuchumi, lakini imekusudiwa kuanzisha historia, kukabidhi mila, kuthamini mahitaji ya kidini ya mwanadamu na kukuza urafiki wa kijamii. Sehemu ya mwisho ya matumaini ni ile ya Udugu ambao sisi kama wakristo tunajifunza kwa Bwana Yesu Kristo. Katika sehemu nyingi za Ureno kuna maana ya ukaribu na mshikamano hai sana. Lakini katika muktadha wa ulimwengu ambao unatukaribia japokuwa hautupatii ukaribu wa kidugu, sisi sote tunaitwa kukuza maana ya Jumuiya, kuanzia na utafiti wa anayeishi karibu nasi. Kwa sababu, kama msema maarufu Swa aramago “Kile kinachotoa maana ya Mkutano ni utafiki na hitaji la kutengeneza njia ili kufikia kile kilicho karibu (Todos os nomes, 1997).

Vijana huko Lisbon
Vijana huko Lisbon

Ni jinsi gani ilivyo vizuri kujigundua kama kaka na dada, kufanya kazi kwa ajili ya wema wa pamoja kwa kuacha nyuma ya mabega kinzani na utofauti. Hata hapa kuna mfano wa vijana ambao kwa kilio chao cha amani na utashi wao wa maisha, wanatupelekea kupandan kwa ugumu …. Papa amependa kuwashukuru tena na kuwatia moyo, ukaribu na wengi ambao katika jamii ya Ureno wanaangaikia wengine, Kanisa mahalia ambalo linafanya vizuri, mbali na mengi yanayo shamiri. Kuhisi wote tunaalikwa kidugu ili kutoa tumaini katika ulimwengu mahali ambamo tunaishi na katika Nchi hii nzuri. Deus abençoe Portugal! amehitimishwa.

02 August 2023, 16:37