Papa Francisko na vijana wa Urussi:muwe mafundi wa amani katikati ya migogoro!
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Takriban kilomita 2500 za kuruka angani, lakini hazikuwa kikwazo cha kutumia muda kidogo wa kuwa pamoja. Kwa hiyo kwa zaidi ya saa moja, Baba Mtakatifu Francisko alizungumza kwa njia ya mtandao tarehe 25 Agosti 2023 na Vijana wavulana na wasichana wapatao 400 ambao wanafanya mkutano wa Kumi wa Vijana Katoliki wa Urussi hadi Agosti 27 huko Mtakatifu Peterburg. Siku hizi zimekuwa kubwa na za aina yake ambazo zimefanyika tangu mwaka 2000, ambazo kwa mwaka 2023 zimeandaliwa kwa mara ya kwanza huko Mtakatifu Peterburg, ambapo baadhi ya washiriki wamekabiliana hata kilomita 9000 kufika hapo.
Kiukweli, kuwa hapo wamekutana miji 54 ya Shirikisho, kuanzia na Kaliningrad hadi Vladivostok lakini, shukrani kwa teknolojia inawezekana kukumbatiana katika Roho waliyopewa, kama mkumbatio wa Maria na Elizabeth, alisema hayo Askofu Mkuu Paolo Pezzi, wa Kanisa Kuu la Mama wa Mungu huko Moscow, katika salamu ya utangulizi. Mkutano huo ni mojawapo ya fursa chache za kufahamiana, kushiriki ushuhuda wa imani; mawasiliano na Papa yanapata furaha fulani, ni maalum katika mwanzo, kwa sababu mtu anaweza kuwa na uzoefu sio tu umoja ndani ya Kanisa la mahalia lakini pia umoja na Kanisa zima.
Akiwahutubia vijana wa Urussi, baada ya kusikiliza shuhuda mbili za Alexander na Varvara, Papa alichukua mawazo matatu kuhusu kauli mbiu ya Siku ya Vijana Duniani (WYD) ya Lisbon, iliyoongozwa na kauli mbiu: “Maria alisimama na kwenda kwa haraka" (Lk 1:39), na hivyo ili waweze kufanya hivyo lazima kuifanyia kazi zaidi: "Nawatakia nyinyi, Vijana Warusi wito wa kuwa mafundi wa amani katikati ya mizozo mingi, katikati ya migawanyiko mingi ambayo inatesa ulimwengu wetu pande zote. Ninawaalika kuwa wapandaji, kupanda mbegu za upatanisho, mbegu ndogo ambazo katika majira ya baridi ya vita hazitaota kwa sasa katika ardhi iliyohifadhiwa, lakini ambayo itachanua katika chemchemi ya baadaye. Kama nilivyosema huko Lisbon: kuwa na ujasiri wa kubadilisha hofu na ndoto. Badilisha hofu na ndoto. Msiwe wasimamizi wa hofu bali wajasiriamali wa ndoto. Jipatie amasa ya kuota ndoto kubwa!”
Baba Mtakatifu Francisko akinukuu tukio la mkutano kati ya Maria na Elizabeth alikumbuka kwamba Bwana huita kwa jina, kabla ya talanta tuliyo nayo, kabla ya sifa zetu, kabla ya giza na majeraha yetu. Kumbuka wanawake hawa wawili waliokuwa mashahidi wa uweza wa Mungu ubadilishao, kumbuka ile haraka ya Maria katika kumwambukiza furaha yake. “Mungu anapoita, hatuwezi kubaki tumekaa tuli. Tunainuka na upesi, kwa sababu ulimwengu, ndugu, mgonjwa, ambaye yuko karibu naye na hajui tumaini la Mungu anahitaji kupokea furaha ya Mungu. Ninainuka haraka ili kupeleka furaha ya Mungu.”
Papa alisisitiza kwamba “Upendo wa Mungu ni kwa kila mtu na Kanisa ni la kila mtu na alishauri kukumbuka Injili mahali inaposimulia mwaliko wa Bwana katika karamu kwenye njia panda kupeleka Injili kwa kila mtu: "Hapa ndivyo Yesu anavyomaanisha kwa wote, Papa alisisitza tena neno “WOTE”. “Kanisa ni mama mwenye moyo wazi, anayejua kukaribisha na kupokea, hasa wale wanaohitaji uangalizi zaidi. Kanisa ni mama mwenye upendo, kwani ni nyumba ya wapendwao na nyumba ya wale walioitwa. Je ni majeraha mangapi, ni kiasi gani cha kukata tamaa kinaweza kuponywa pale ambapo mtu anahisi kukaribishwa. Na Kanisa linatukaribisha. Ndio maana ninaota Kanisa ambalo halina mtu wa ziada, ambapo hakuna mtu wa ziada. Tafadhali, Kanisa sio desturi ya kuchagua nani aingie na asiyeingia. Hapana, kila mtu, na kwa kila mtu. Kiingilio ni bure. Na baadaye kila mtu asikie mwaliko wa Yesu wa kumfuata, kuona jinsi anavyosimama mbele za Mungu; na kwa njia hiyo kuna mchakato wa mafundisho na Sakramenti.”
Pia katika hali hii, Baba Mtakatifu Francisko amechukua wazo ambalo liko karibu na moyo wake wa mazungumzo kati ya vijana na wazee na umuhimu wa uhamasisho wa uzoefu unaopaswa kujitokeza kutokana nayo. Kwa kurudi kwenye mkutano kati ya Maria na Elizabeti, ambayo ni ndoto Baba Mtakatifu aliwambia kuwa anatualika kuwa: “wajenzi wa madaraja kati ya vizazi, kutambua ndoto za watangulizi wetu na babu na Bibi. “Muungano kati ya vizazi huweka historia na utamaduni wa watu hai. Papa alisisitiza juu ya umuhimu wa kuwa "shara ya matumaini, ishara ya amani na furaha, kama Maria. Kwa kuiga unyenyekevu wake, wao pia wanaweza kubadilisha historia ambayo wanaishi. Kwa hivyo wazee huota mambo mengi: demokrasia, umoja wa mataifa…; na vijana wanatabiri, wanaitwa kuwa mafundi wa mazingira na amani. Elizabeth, kwa hekima ya miaka kwa kuwa alikuwa mzee , aliimarisha Maria, ambaye alikuwa kijana na alikuwa amejaa neema, huku akiongozwa na Roho.”