Papa Francisko:Je Yesu ni Bwana wa maisha yangu?
Na Angella Rwezaula, Vatican.
Katika Dominika ya 21 ya Mwaka A, tarehe 27 Agosti 2023, Baba Mtakatifu ametoa tafakari yake kwa waamini na mahujaji waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican ambapo akianza tafakari hiyo amesema: “Leo katika Injili (Mt 16,13-20) Yesu anawauliza wanafunzi swali moja zuri: Je “watu wanasema nini juu ya mwana wa binadamu”. Ni swali ambalo tunaweza kujiuliza hata sisi, kwamba watu wanasemaje Yesu? Kwa ujumla mambo mazuri: wengine wanaona kama mwalimu mkuu, kama mtu maalum: mwema, mwenye haki, makini na jasiri… Lakini je hiyo inatosha kuelewa ni nani na hasa inamtosha Yesu? Baba Mtakatifu akiendelea amesema “Nafikiri hapana. Ikiwa Yeye angekuwa tu mhusika wa wakati uliopita wa zamani, kama takwimu zilizotajwa katika Injili hiyo hiyo zilivyokuwa kwa watu wa wakati huo kama vile Yohane Mbatizaji, Musa, Eliya na manabii wakuu, ingekuwa kumbukumbu nzuri ya wakati ule uliopita. Lakini hii haifanyi kazi kwa Yesu. Kwa hiyo, mara moja baadaye, Bwana anauliza wanafunzi swali stahiki: “Lakini je ninyi Mnasemaje kuhusu mimi ni nani?” (rej. Mt 16, 15). Mimi ni nani kwenu sasa hivi?"
Kwa kuongezea, Papa amesema "Yesu hataki kuwa mhusika mkuu wa historia, lakini anata kuwa muhusika mkuu wa leo yako, wa leo yangu; na siyo nabii wa mbali, bali Yesu anataka kuwa Mungu wa karibu! Papa amekazia kusema. Kristo sio kumbu kumbu ya wakati uliopita, lakini ni Mungu wa wakati wa leo hii. Ikiwa angekuwa mtu wa kihistoria tu, kumuiga leo hii ingekuwa ngumu: tutajikuta mbele ya shimo kubwa la wakati na hasa mbele ya mtindo wake, na ambao ni kama mlima mkubwa na usiofikiwa; tunataka kuupanda, lakini usio na uwezo na wa zana za lazima. Kinyume chake Yesu ni hai na tukumbuke haya, kuwa Yesu yu hai, Yesu anaishi Kanisani, anaishi duniani, Yesu anatusindikiza, Yesu yu upande wetu, na anatutolea Neno lake, anatupatia neema yake, inayotuangazia na kuturudishia maisha yetu na katika njia, Yeye,ni mtaalamu kiongozi na mwenye hekima, anafurahi kuongozana nasi kwenye njia ngumu zaidi na kwenye milima isiyoweza kupandwa."
Baba Mtakatifu Francisko, amefafanua kuwa katika njia za maisha sisi hatuko peke yetu, kwa sababu Kristo yuko nasi na anatusaidia kutembea, kama alivyofanya na Petro na kwa wanafunzi wengine. Kwa hiyo kwa dhati Petro, katika Injli ya leo, anamtangaza na kwa neema ya kumjua katika Yesu, “ Kristo Mwana wa Mungu aliye hai” (rej. Mt 16,16): Yesu anakwambia wewe unasemaje kuhusu mimi? Kwa hiyo Papa ameshauri kwamba “tuhisi sauti ya Yesu ambayo inatuuliza swali hilo”. Kwa maneno mengine: Yesu ni nani kwangu? Ni mtu mkubwa, mtu wa kukimbilia, mfano usioweza kufikiwa au Mwana Mungu, anayetembea kando yangu, ambaye anaweza kunipeleka kwenye kilele cha utakatifu, mahali ambapo siwezi kufika peke yangu? Je, kweli Yesu yu hai katika maisha yangu, na Yesu anaishi na mimi? Ni Bwana wangu? Je, mimi ninamtegemea Yeye wakati wa shida? Je, ninakuza uwepo wake kupitia Neno kwa njia ya Sakramenti? Kupitia Yeye mimi ninajiruhusu kuongozwa naye, pamoja na kaka na dada zangu, katika jumuiya? Maria, Mama wa safari, atusaidie kuhisi Mwanae aliye hai na yupo kando yetu.” Papa amehitimisha.