Papa Francisko ameondoka kwenda Mongolia katika hija ya 43 ya Kitume!
Vatican News.
Baba Mtakatifu Francisko ameanza ziara yake ya 43 Kitume ambapo ameondoka saa 12.41 jioni ya tarehe 31 Agosti 2023 kutoka katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa Fiumicino, Roma, kuelekea Ulaanbataar, mji mkuu wa Mongolia. Ni safari ya ndege ya kilomita elfu saba ili kutembelea pembe nyingine ya dunia, ambayo ni jumuiya ndogo lakini yenye bidii ya Wakatoliki wanaoishi hapo, yaani waamini wapatao 1,500, wanamngoja kwa shauku kubwa.
Njia, ambayo pia inaweza kubadilika, inajumuisha safari za ndege kupitia Italia, Kroatia, Bosnia Herzegovina, Serbia/Montenegro, Bulgaria, Uturuki, Georgia, Azerbaijan, Kazakhstan, China. Kuwasili nchini Mongolia kunatarajiwa saa 10 (saa za ndani), nchini Italia itakuwa usiku kamili (maana kuna tofauti ya masaa 6). Katika msafara wa Papa, waandishi wa habari karibu sabini wanamsindikiza na Papa.
Telegram kwa Rais Matarella
Katika telegramu aliyoelekezwa kwa Rais wa Jamhuri ya Italia Sergio Mattarella, Papa anathibitisha kwamba yuko karibu kukutana na wale anaowaita “watu mashuhuri". Papa atatembelea, jumuiya ndogo lakini iliyo hai ya Kikatoliki; anatuma salamu zake za raha kwa Waitaliano, ambazo anaandamana nazo kwa matumaini ya kujitolea kwa manufaa kwa wote na kwa sala kwa Mungu ili kusaidia wale wanaofanya kazi kwa ajili ya mipango ya mshikamano".
Papa wa kwanza kukanyaga ardhi ya Mongolia
Papa Francisko ni papa wa kwanza kukanyaga ardhi ya Mongolia, na ubalozi wa Vatican huko Gerelmaa Davaasuren. Akizungumza na waandishi wa habari wa Vatican, alisisitiza juu ya matunda ya mahusiano baina ya dini na heshima kwa utofauti unaodhihirishwa na uwepo wake. Ni "matarajio makubwa kwa safari hii ya kihistoria, ambayo anaiona kuwa mchango mkubwa katika kudumisha amani na utulivu katika eneo letu na duniani kote". Huko Kazakhstan, Papa Francisko alikuwa amesema kwamba kuna neema katika kuwa kwenye kundi dogo kama Kanisa. Huko Mongolia kundi ni dogo kiidadi lakini katika hali hii ya upendeleo na kutokuwa na umuhimu, kuna thamani na uzito maalum ambao Papa Francisko anataka kuwekea nuru katika ziara hii.
Tarehe 31 Agosti 2023 Mchana kabla ya kuondoka Nyumba ya Mtakatifu Marta kuelekea uwanja wa Ndege wa Kimataifa, Baba Mtakatifu Francisko, alisalimiana na vijana 12 wa mataifa mbalimbali, ambao ni wageni wa bweni la “Dono di Misericordia” yaani 'zawadi ya Huruma' , ambao katika siku za hivi karibuni wamesaidia Kanisa katika maandalizi ya kupeleka chakula knchini Ukraine. Kadinali Konrad Krajewski pia alikuwepo. Kwa hiyo ishara ya ukaribu, ile ya Mrithi wa Petro, kwa wale wanaoishi katika hali ya umaskini, kwa wale wanaopata aina mbalimbali za kunyimwa, ambayo sasa inarudiwa kabla ya kila safari ya upapa, karibu ni aina ya muhuri ambayo daima huweka huduma ya Kipetro hasa katika kuungana na wa pembezoni, wanaoishi barabarni na maskini.