Papa amemteua Amarante kuwa Mkuu mpya wa Chuo Kikuu cha Laterano
Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko, Jumanne tarehe Mosi Agosti 2023 amemwandikia barua Mkuu mpya wa Chuo Kikuu cha Kipapa la Laterano, Padre Alfonso V. Amarante, C.SS.R.,. Katika barua yake, Baba Mtakatifu anabainisha kuwa “ kutokana na kuchauguliwa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kipapa, ninakukabidhi jukumu gumu na kwa tumaini tabiti. Unapaswa kupeleka katika utimilizo wa kazi namna hiyo vizuri kama alivyofanya mtangulizi wako, Profesa Vincenzo Buonomo. Hii ni kufanya Chuo Kikuu cha Laterano kuwa imara zaidi na mwepesi wa kuheshimu vyema kazi yake ya kwanza ya kutangaza ukweli na furaha ya Injili kwa njia ya mafunzo, tafakari na kazi ya kielimu”. Papa anasisitiza kuwa “ Chuo kikuu “ cha Papa kinapaswa kuzama katika utume huu, kwa utambuzi wa maalum wa ukakaribu na Mfuasi wa Petro na kazi yake ya kuimarisha ndugu na katika kipindi hiki cha kihistoria, kikanisa na kiutamaduni ambamo Bwana alituita kuishi.”
Mkurugenzi wa Usimamizi katika utawala wa Chuo Kikuu
Baba Mtakatifu Francisko katika barua hiyo anabainisha kwamba “Katika muktadha huo, nimeamua kumteua Mkurugenzi wa Usimamizi, kukusaidia katika usimamizi wa utawala na uchumi na katika kushirikiana kwa dhati kwa maendeleo ambayo yanafanya Chuo Kikuu cha Latenano kuwa mstari wa mbele wa Mfumo wa Chuo Kikuu Kikanisa na kiraia”. Baba Mtakatifu ameandika kuwa: “ Katika kupanga mtaala na utawala, katika kusikiliza ishara za nyakati, kwa kufanya kuwa tunu msingi ya ushirikiano na Taasisi za Kipapa zilizomo katika Vitivo cya Chuo Kikuu, utatumia mihimili ya vyuo viku vyenye uwezo, kwa kuvihusisha ili kusaidiana na mabadiliko ya kielimu na kiusimamizi ambayo yataonekana kuwa ya lazima.”
Kuwa sauti ya kuchangia kwa akili,busara,ubunifu na ujasiri
Papa amempatia maelekezo menginge kwamba atasaidiana hata na Baraza Kuu la Uratibu ambao uliundwa na Papa Mwenyewe mnamo tarehe 21 Agosti 2021 mahali ambapo zaidi ya sura ambazo zilikuwa zinatarajiwa, watajumuishwa wengine waliohitimu kutoka Curia Romana na katika ulimwengu wa chuo kikuu, ili kufafanya hata kitaasisi juu ya dhamana ya kipekee ya uhusiano kati ya Chuo Kikuu Laterano na Makao makuu ya Kitume. Kwa njia hiyo, kazi yake inajumuishwa kuingizwa kwenye Chuo Kikuu cha Laterano mchakato, ambao aliutaka Papa mwenyewe na Uratibu wa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu kwa kuzingatia upangaji mpya wa Taasisi za Kielimu za Kipapa Roma. Kwa kuhitimisha barua hiyo Baba Mtakatifu anaandika kuwa: “Ninaamini kwamba, kwa kuwa sauti nzima ya Chuo Kikuu, utachangia kwa akili, busara, ubunifu na ujasiri katika mchakato huo ambao utauanza mnamo tarehe 12 Septemba Ijayo. Roho wa Kristo Mfufuka awe juu yako na Mwenyeheri Bikira Maria Salus Populi Romani, akusindikize. Tafadhali uniombee”.
Tamko na uteuzi wa Baraza Kuu la Utaribu wa Chuo Kikuu cha Kipapa la Laterano
Baba Mtakatifu Francisko kufuatia na hiyo bara hata hivyo Jumanne tarehe Mosi Agosti 2023 ametoa Tamko la uteuzi wa Baraza Kuu la Uratibu wa Chuo Kikuu cha Kipapa cha Laterano, akikumbusha hati ya tarehe 21 Agosti 2021 ambayo kwayo yeye aliunda ndani ya Chuo Kikuu cha Kipapa cha Latenano Baraza Kuu la Uratibu. Kwa hiyo Baba Mtakatifu anaandika kuwa:“Mbali na sura zilizotajwa tayari, ninateua wajumbe wafuatao: Dk. Sabrina Di Maio, Mkurugenzi wa Usimamizi; Dk. Stefano Fralleoni, Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usimamizi - Utawala wa Urithi wa mali za Kitume; Dk. Marina Roveraro, Mtaalam wa Udhibiti na Usimamizi - Sekretarieti ya Uchumi; Dk. Paolo Nusiner, Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Masuala ya Jumla ya Baraza la Kipapa la Mawasiliano; Mons. Luigi Michele De Palma, Katibu wa Baraza la Uratibu Mkuu. Wajumbe wapia wataanza majukumu yao mnamo tarehe 11 Septemba 2023
Uteuzi wa Mshauri Mkuu wa Mji wa Vatican, Bonomo
Hata hivyo huyo aliyerithiwa Profesa Vincenzo Buonomo ndiye alikuwa Mkuu wa Chuo kikuu cha Kipapa Laterano, ambapo Jumanne tarehe Mosi Agosti 2023, Baba Mtakatifu amemteua kuwa Mshauri Mkuu wa Mji wa Vatican na ambaye ambaye hadi uteuzi huo alikuwa tayari ni mshauri wa serikali.