Papa ameungamisha baadhi ya vijana katika bustani ya Vasco da Gama,Lisbon
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Akiwa katika siku yake ya tatu kwenye Ziara yake ya 42 ya Kitume Kimataifa katika Siku ya 37 ya Vijana duniani (WYD) ambayo inaongozwa na Kauli mbiu: “Maria aliondoka akaenda kwa haraka.” Lk. 1:39, Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa tarehe 4 Agosti 2023, amepata fursa ya kuungamisha vijana katika sakramenti ya kitubio. Yesu aliweka Kitubio na Mpako wa Wagonjwa kwa sababu alijua udhaifu wa binadamu hauishi mara anapopokea uzima wa Mungu! Sakramenti ya Upatanisho ni muhimu sana katika safari ya maisha ya kiroho na uwongofu wa ndani unaodai toba kila wakati na malipizi ya dhambi ya mwanadamu.
Ni kwa njia hiyo ambapo kwa kukaribishwa na kwaya iitwayo Esta es la juventud del Baba Mtakatifu Francisko aliwasili katika bustani ya Vasco da Gama, huko Lisbon. Katika nafasi hiyo kubwa ya kijani moja ya wakati muhimu zaidi wa Siku nzima ya Vijana Ulimwenguni (WYD), yaani kupokea sakramenti ya upatanisho kwa vijana wa kike na kiume ilitendekea
Kwa hakika, watu wapato 150 waliungamana dhambi zao katika bustani hiyo kubwa, iliyotengenezwa na wafungwa vijana wa gereza la Pasos de Ferreira, ambayo imejengwa kwa kutumia nyenzo zilizosindikwa na kutumika tena na kufanywa ambapo hata walemavu wanaweza kwenda. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu Francisko kabla ya kwenda katika Kituo cha Mtakatifu Vinsenti wa Paulo kukutana na wawakilishi wa baadhi ya vituo vya usaidizi na wahudumu alifika katika sehemu hii kwa kiti cha magurudumu na kuwaungamisha vijana ambao ni mvulana wa Kihispania mwenye umri wa miaka 21, mwenye umri wa miaka 33 na Mzee wa Guatemala na Mwitaliano wa miaka 19.