Papa Francisko amelaani vurugu zisizo na msingi nchini Equador
Vatican News
Vikosi vya kisiasa na raia wa Ecuador viungane katika juhudi za pamoja kwa ajili ya amani. Huu ndio wito uliozinduliwa na Baba Mtakatifu Francisko tarehe 12 Agosti 2023 katika telegramu, iliyotiwa saini na Kardinali, Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, iliyotumwa kwa Askofu Mkuu Alfredo José Espinoza Mateus, wa Jimbo kuu katoliki la Quito,Equador ambapo, Baba Mtakatifu Francisko anaelezea masikitiko yake kuhusu mauaji ya mgombea urais wa nchi hiyo, Fernando Villavicencio na wakati huo huo analaani vurugu zisizo na msingi zinazosababisha mateso kwa watu.
Juhudi za pamoja za kuleta amani
Papa Francisko aidha ametoa rambirambi zake kwa Askofu, kwa familia za marehemu na watu wote wapendwa wa Ecuador huku akiwaalika raia na nguvu za kisiasa kuunganisha juhudi zao pamoja kwa ajili ya amani. Baba Mtakatifu Francisko, akikabidhi sehemu iliyobaki ya Villavicencio kwa maombezi ya kimama ya Mama Yetu wa El Quinche, ametoa baraka zake kama ishara ya imani na matumaini katika Kristo Mfufuka.
Mgombea urais Equador 20 Agosti 2023
Kuhusiana na Fernando Villavicencio, aliyekuwa mwandishi wa habari na mgombea wa kiti cha urais wa Ecuador, mwenye umri wa miaka 59 aliuawa mnamo tarehe 9 Agosti 2023, katika mji mkuu wa Equador Quito, mwishoni mwa mkutano wa kampeni ya uchaguzi. Mwanamume huyo, ambaye alipinga nguvu za magenge na makundi, ya kihalifu alipigwa risasi mara kadhaa. Mauaji hayo yalidaiwa na shirika la uhalifu la Los Lobos. Takriban watu tisa walijeruhiwa katika shambulio hilo akiwemo mgombea mwingine wa urais na maafisa wawili wa polisi. Waliojeruhiwa walikuwa wakihudhuria hafla iliyofanywa na Villavicencio katika eneo lenye watu wengi la Quito, ambapo mshambuliaji asiyejulikana alimfyatulia risasi mgombea urais wa nchi hiyo katika uchaguzi mkuu usiokuwa wa kawaida uliopangwa kufanyika Dominika tarehe 20 Agosti 2023.
Aliyemuua mgombea huyo naye alikufa
Mmoja wa watu wanaoshukiwa kumuua Villavicencio alikufa baada ya mapigano ya moto na maafisa wa usalama, watu sita walikamatwa. Guillermo Lasso, rais anayemaliza muda wake, alitangaza hali ya hatari nchini kote saa chache baada ya shambulio hilo. Ugombea wa Bwana Villavicencio ulijikita zaidi katika mapambano dhidi ya rushwa, alifafanu Alfredo Luis Somoza, rais wa Taasisi ya Kimataifa ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Milan, Italia akihojiwa na Radio Vatican - Vatican News
kwa mujibu wa mchambuzi huyo wa masuala ya kisiasa alisema: “Mwanasiasa huyo ndiye pekee ambaye hakukubali kulindwa na Polisi wa Taifa, kwa sababu hakuwaamini. Kwa hiyo shambulio ambalo alipoteza maisha, lina sifa zote za kuvizia hasa kutoka kwa waalifu wa biashara ya madawa ya kulevya. Bango la Ecuador kwa jina la Los Lobos, kiukweli, kwenye video lilidai kuhusika na mauaji hayo, likitoa maelezo, ambayo hata hivyo wachunguzi wanaona si ya kuaminika sana. Hakika, bango hilo linadai kwamba wanasiasa wafisadi wanaokubali pesa kutoka kwa walanguzi wa dawa za kulevya lazima waheshimu kauli yao.” Lakini inaonekana kwake kuwa ni vigumu sana kwamba Villavicencio, ambaye aliegemeza kampeni yake kwenye vita dhidi ya ufisadi, angekubali pesa zozote kutoka kwao. Hizi zote ni dhana ambazoitabidi zithibitishwe, alisisitiza. Na wakati huo huo, rais anayemaliza muda wake Guillermo Lasso alithibitisha kwamba uchaguzi wa urais mnamo tarehe 20 Agosti 2023 hautasitishwa, lakini hali ya hatari inaleta hali mbaya ya uchaguzi huu, ambao kwa upande wa mtaalamu huyo Somoza anasema - ulipaswa kukomesha kipindi cha zaidi ya miaka miwili ya machafuko ya kisiasa.”