Tafuta

2023.08.19 Kitabu cha Dorothy Day:Nilimjua Mungu kupitia maskini wake (LEV). 2023.08.19 Kitabu cha Dorothy Day:Nilimjua Mungu kupitia maskini wake (LEV). 

Papa Francisko:Dorothy Day,uzuri wa imani nilimpata Mungu kupitia maskini

Tunachapisha utangulizi wa Papa katika kitabu cha wasifu wa Dorothy Day:“Nilimpata Mungu kupitia maskini wake.Kutoka kumkana Mungu hadi imani:safari yangu ya ndani.”Dorothy Day(1897-1980),mwanzilishi wa Harakati ya Wafanyakazi Katoliki,alikuwa mwandishi wa habari wa Marekani na mpigania amani.

Francisko

Maisha ya Dorothy Day, kama yeye mwenyewe anavyotusimulia katika kurasa hizi ni moja ya uthibitisho unaowezekana wa yale ambayo,  Papa Benedikto XVI tayari aliyaunga mkono kwa nguvu na ambayo mimi mwenyewe nimeyakumbusha mara kadhaa kuwa: “Kanisa hukua kwa mvuto, sio kwa kugeuza watu imani.” Namna ambayo Dorothy Day anasimulia kufikia kwake  imani ya Kikristo inathibitisha ukweli kwamba si juhudi za kibinadamu au mikakati inayowaleta watu karibu na Mungu, bali ni neema inayobubujika kutoka katika upendo na uzuri unaobubujika kutokana na ushuhuda, upendo unaotokana na upendo ambao unakuwa ukweli. Historia nzima ya Dorothy Day, mwanamke huyu wa Marekani aliye jitolea maisha yake yote kwa ajili ya haki ya kijamii na haki za watu, hasa maskini, wafanyakazi walionyonywa, waliotengwa na jamii, aliyetangazwa kuwa Mtumishi wa Mungu mnamo mwaka 2000, ni ushuhuda wa kile ambacho mtume Mtakatifu Yakobo tayari alidai katika Barua yake kwamba: “Nioneshe imani yako bila matendo, nami nitakuonesha imani yangu kwa matendo yangu”(2:18).

Ningependa kumulika vipengele vitatu vinavyoibuka kutoka katika kurasa za wasifu wa Dorothy Day kama mafunzo muhimu kwa kila mtu katika wakati wetu ambayo ni: kutokuwa na utulivu, Kanisa na huduma. Dorothy ni mwanamke asiyetulia: alipoishi katika njia yake ya kufuata Ukristo, yeye alikuwa ni kijana, hata bado hajafikisha miaka thelathini, kwa muda mrefu sana alikuwa ameacha mazoezi ya kidini, ambayo yalionekana kwake, kama ndugu  aliyejikita na  kitabu hiki anaeleza kitu kama ugonjwa.  Badala yake, alipokua katika jitihada yake ya kiroho, alikuja kuzingatia imani na Mungu kuwa si kama “pengo la kuacha”, kwa kutumia ufafanuzi maarufu wa mtaalimungu wa Kilutheri, Dietrich Bonhoeffer, lakini kama vile inavyopaswa kuwa, yaani, utimilifu wa maisha na lengo la mtu kutafuta furaha. Dorothy Day anaandika: “Mara nyingi maono ya Mungu yalikuja nilipokuwa peke yangu. Wapinzani wangu hawawezi kusema kuwa ulikuwa  ni woga wa upweke na uchungu ambao ulinifanya nimgeukie Yeye. Ni katika miaka hii michache nikiwa peke yangu na furaha tele ndipo nilipompata. Hatimaye nilimpata kwa furaha na shukrani, si kwa maumivu.”

Hapa, ndipo Dorothy Day anatufundisha kwamba Mungu si chombo cha faraja tu au kutengwa kwa mwanadamu katika uchungu wa siku zake, lakini anajaza shauku  yetu ya furaha na utimilifu kwa wingi. Bwana anatamani mioyo isiyotulia, sio roho za kibepari ambazo zimeridhika na kile kilichopo. Na Mungu hachukui chochote kutoka kwa wanaume na wanawake wa nyakati zote, yeye hutoa mara mia tu! Yesu hakuja kutangaza kwamba wema wa Mungu ni mbadala wa kuwa mwanadamu, badala yake alituzawadia moto wa upendo wa kimungu ambao huzaa matunda yale yote yaliyo mazuri, ya kweli na ya haki yanayokaa ndani ya moyo wa kila mtu. Kusoma kurasa hizi za Dorothy Day na kufuata ratiba yake ya kidini linakuwa tukio ambalo ni zuri kwa moyo na ambalo linaweza kutufundisha mengi sana kuweka picha halisi  ya Mungu iliyo hai ndani yetu.

Dorothy Day katika nafasi ya pili, inahifadhi maneno mazuri katika Kanisa Katoliki, ambayo kwake, kutoka katika kumkana na kuingia  kwenye  ulimwengu wa kujitolea kwa vyama vya kijamii na wafanyakazi, mara nyingi ilionekana kuwa upande wa matajiri na wenye ardhi, hawakujali mahitaji ya haki hiyo ya kweli ya kijamii na usawa thabiti ambao katika muktadaha huo  unatukumbusha kwenye kurasa nyingi tajiri za Agano la Kale. Naam, kadiri ushikamanifu wake wa kweli wa imani ulivyoongezeka, ndivyo pia ufikirio wake kwa ajili ya asili ya kimungu wa Kanisa Katoliki uliongeza. Sio kwa mtazamo wa uaminifu usio na shaka, karibu  kusema kwamba ulinzi rasmi wa nyumba mpya ya kiroho, lakini kwa mtazamo wa uaminifu na mwanga, ambao ulijua jinsi ya kutambua katika maisha ya Kanisa kipengele cha kifungo kisichoweza kupunguzwa na siri, zaidi ya hayo, ya wengi na mara kwa mara kuanguka kwa wanachama wake.

Dorothy Day anabainisha kuwa: “Mashambulizi yenyewe yaliyoelekezwa dhidi ya Kanisa yamenionesha umungu wake. Ni taasisi ya kimungu pekee ambayo ingeweza kunusurika kusalitiwa kwa Yuda, kukanushwa kwa Petro, dhambi za wengi waliodai imani yake, ambao walipaswa kuwatunza maskini wake.” Na, katika kifungu kingine cha andiko hilo, anathibitisha: “Siku zote nimefikiri kwamba udhaifu wa kibinadamu, dhambi na ujinga wa wale wanaojikuta katika vyeo vya juu katika mchakato wa historia umedhihirisha tu kwamba Kanisa lazima liwe la kimungu ili kuendelea katika zama za karne. Nisingelaumu juu ya Kanisa kwa yale niliyoamini kuwa makosa ya makasisi.”

Ni jinsi gani ilivyo nzuri kusikia maneno ya namna hii kutoka katika ushuhuda mkuu wa imani, mapendo na matumaini katika karne ya ishirini, karne ambayo Kanisa lilikuwa kama lengo la kukosolewa, kuchukizwa na kuachwa! Mwanamke huru, Dorothy Day, asiyeweza kuficha yale ambayo haogopi kufafanua kama “makosa ya makasisi!”, lakini ambaye anakiri kwamba Kanisa lina uhusiano wa moja kwa moja na Mungu, kwa sababu ni lake, si letu, alilitaka yeye, sio sisi, ni chombo chake, na sio kitu ambacho tunaweza kutumia. Huu ndiyo wito na utambulisho wa Kanisa: ukweli wa kimungu, sio wa kibinadamu ambao unatupeleka kwa Mungu na ambao Mungu anaweza kutufikia.

Hatimaye, huduma. Dorothy Day ametumikia wengine maisha yake yote. Hata kabla ya kuwa na imani katika hali kamili. Na hii kufanya kupatikana, na kazi yake kama mwandishi wa habari na mwanaharakati, ikawa aina ya “barabara kuu” ambayo Mungu aligusa moyo wake. Na ni yeye mwenyewe anayemkumbusha msomaji jinsi mapambano ya haki yanawakilisha mojawapo ya njia ambazo, hata bila kujua, kila mtu anaweza kutambua ndoto ya Mungu ya ubinadamu uliopatanishwa, ambayo harufu ya upendo inatawala harufu ya kuchukiza na ubinafsi. Maneno ya Dorothy Day yanatia nuru zaidi kwa: “Upendo wa kibinadamu kwa ubora zaidi, usiovutia, unaong’aa, unaoangazia siku zetu, hutupatia taswira ya upendo wa Mungu kwa mwanadamu. Upendo ndiyo jambo bora zaidi tunalopewa kujua katika maisha haya.” Hii inatukumbusha jambo la kufundisha sana hata leo hii: waamini na wasioamini ni washirika katika kukuza hadhi ya utu wa kila mtu wakati wanampenda na kumtumikia mwanadamu aliyeachwa zaidi.

Wakati Dorothy Day anaandika kwamba kauli mbiu ya harakati za kijamii kwa wafanyakazi wa wakati wake ilikuwa “tatizo la mtu, shida ya kila mtu”, alinikumbusha kauli maarufu ambayo Padre Lorenzo Milani, kasisi wa Shirika la Barbiana ambaye mwaka huu anatimiza miaka 100 tangu kuzaliwa kwake, alimwambia Profesa mhusika mkuu wa mafunzo ya Fasihi akisema: “Nilijifunza kwamba shida ya wengine ni sawa na yangu. Kuzipanga zote kwa pamoja ni siasa. Kuziondoa pekee yako  ni ubadhirifu.” Kwa hiyo huduma lazima iwe siasa: yaani, uchaguzi madhubuti ili haki ipatikane na hadhi ya  kila mtu ilindwe. Dorothy Day, ambaye nilitaka kumkumbuka katika hotuba yangu kwa Bunge la Marekani wakati wa Ziara  yangu ya kitume mnamo mwaka 2015, ni kichocheo na kielelezo kwetu katika mchakato wa safari hii ngumu lakini ya kuvutia.

Anahitimisha Papa Francisko katika Utangulizi wa Kitabu cha Dorothy Day: "Nilimpata Mungu Kupitia Maskini."

Utangulizi wa Papa katika Kitabu cha Dorothy Day
20 August 2023, 13:14