Tafuta

2023.08.02 Papa akihutubia Serikali na Mamlaka ya kiraia na wanadiplomasia huko Ureno katika fursa ya ziara ya Siku ya vijana duniani 2023 Ureno. 2023.08.02 Papa akihutubia Serikali na Mamlaka ya kiraia na wanadiplomasia huko Ureno katika fursa ya ziara ya Siku ya vijana duniani 2023 Ureno.  (Vatican Media) Tahariri

Dira ya Ulaya na njia za ubunifu za amani

Katika hotuba yake kwa mamlaka ya Ureno, Francisko kwa mara nyingine tena anaomba Umoja wa Ulaya kuendeleza diplomasia ambayo inazima mizozo kwa kuanzia na ile ya Ukraine.

ANDREA TORNIELLI

Ikiwa vita vilivyozuka katika moyo wa Wakristo wa Ulaya na uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine vinaweza kutufanya tuwe tumechoka kuna mtu ambaye hachoki kamwe, akichanganya unabii na uhalisia, wa kuomba amani kwa kuita mataifa na watu  na hasa ' Ulaya  kwa majukumu yao. Hata mwanzoni mwa safari yake nchini Ureno ambako amewasili kwa ajili ya kujionea Siku ya Vijana Duniani, Papa Francisko alizungumzia jukumu la Bara la Kale, akitumaini kwamba halitasahau utambulisho wake bali litajua jinsi ya kupendekeza njia za ubunifu wa amani na suluhisho za kidiplomasia badala yake kukubali wazo la kutoweza kushindwa kwa vita na mbio za silaha

Mkutano wa Papa na mamlaka ya Taifa la Ureno

Mrithi wa Petro aliona jinsi ukosefu wa haki wa kimataifa, vita, majanga ya tabia nchi na uhamiaji yanavyoendesha haraka kuliko uwezo, na mara nyingi nia ya kukabiliana na changamoto hizi pamoja. Lakini aliongeza kuwa “Lisbon inaweza kupendekeza mabadiliko ya kasi, kwa kuzingatia kwamba mkataba wa mageuzi wa Umoja wa Ulaya ulitiwa saini hapo mnamo mwaka 2007, ambao unasema kwamba Umoja katika uhusiano wake na dunia nzima unachangia amani, usalama, uendelevu  wa maendeleo ya Dunia, mshikamano na kuheshimiana kati ya watu, biashara huria na ya haki, kutokomeza umaskini na ulinzi wa haki za binadamu”.


Papa Francisko alithibitisha kwamba “ulimwengu unahitaji Ulaya, Ulaya ya kweli: inahitaji jukumu lake kama daraja na mleta amani katika sehemu yake ya mashariki, katika Mediterania, Afrika na Mashariki ya Kati”. Ni kwa njia hiyo tu Ulaya itaweza kuleta, kwenye eneo la kimataifa, asili yake maalum, ambayo katika hali ya sasa ya kihistoria inajitahidi kujitokeza. Kuna haja ya kuendeleza diplomasia ya amani ambayo huzima migogoro na kupunguza mivutano, yenye uwezo wa kushika dalili dhaifu za utulivu na kusoma kati ya mistari potovu zaidi".


Tukiutazama uhalisia wa siku hizi bila vipofu vya kiitikadi, lazima tutambue kuwa haya hayafanyiki. Hii ndiyo sababu Papa anauliza maswali ya Ulaya: “Unasafiri kuelekea wapi, ikiwa hutoi njia za amani, njia za ubunifu za kukomesha vita nchini Ukraine na migogoro mingi inamwaga damu duniani? Na tena, kupanua uwanja: ni njia gani unayofuata, Magharibi? Teknolojia yako, ambayo imeashiria maendeleo na utandawazi wa dunia, haitoshi yenyewe; kidogo zaidi silaha za kisasa zaidi zinatosha, ambazo haziwakilishi uwekezaji kwa siku zijazo, lakini umaskini wa mtaji wa kweli wa kibinadamu, ule wa elimu, huduma za afya, hali ya ustawi. Inatia wasiwasi mtu anaposoma kwamba katika sehemu nyingi fedha huwekwa mara kwa mara katika silaha badala ya kukwekeza katika siku zijazo za watoto wao."

Mkutano wa Papa na viongozi wa Nchi ya Ureno
Mkutano wa Papa na viongozi wa Nchi ya Ureno

Ni nini kingine kinachohitajika kutokea ili Ulaya itikisike na kurejesha jukumu lake? Kulingana na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Ukraine, kufikia Februari 22, 2023, ilikuwa imbainisha kwamba uvamizi huo umegharimu maisha ya raia 9,655, walio tiwa ndani watoto 461; kujeruhiwa raia 12,829, ikiwa ni pamoja na watoto 926; na  tukio la vifo zaidi ya 68,000, zaidi ya uhalifu wa kivita na  ambapo 2,600 kati yao walifanyia dhidi ya watoto. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) linakadiria kuwa watu milioni 8.1 walilazimika kuyahama makazi yao barani Ulaya kufikia mwisho mwa Februari 2023. Kuna maeneo yote ya Ukraine yaliyoharibiwa, kuchafuliwa au kuchimbwa. Mkasa huu lazima umalizike, kwanza kwa mapatano na kisha kwa amani ya haki.

Lakini Papa Fransisko haachi kutazama siku zijazo kwa matumaini kwani anasema: “Nina ndoto ya Ulaya, moyo wa Magharibi ambao inaweka ustadi wake kwa matumizi mazuri ya kuzima milipuko ya vita na kuwasha taa za matumaini; Ulaya ambayo inajua jinsi ya kugundua upya nafsi yake ya ujana, inaota juu ya ukuu wa yote na kwenda zaidi ya mahitaji ya haraka; Ulaya ambayo inajumuisha watu na watu binafsi, bila kufuata nadharia na ukoloni wa kiitikadi”. Inastahili kusikilizwa kabla haijachelewa”.

Habari za Papa Francisko kuhusu ziara ya nchini Ureno.
02 August 2023, 16:53