Barua Pablo kwa Papa,kijana alifariki Julai 15:Sitokuwa WYD
Na Angella Rwezaula , - Vatican.
Pablo alijua kwamba hangeweza kwenda kuudhuria Siku ya vijana duniani (WYD) huko Lisbon 2023. Kutokana na ugonjwa wa saratani aina ya “Ewing's sarcoma”, ambao ni uvimbe unaokua katika umri wowote na katika sehemu yoyote ya mwili, haukuwa umempa matumaini. Hata hivyo, kijana Pablo hakujua kama katika siku ambazo Papa Francisko angekutana na maelfu ya vijana katika mji mkuu wa Ureno kwa ajili ya tukio la dunia, angekuwa bado hai au tayari yuko Mbinguni, karibu na Yule ambaye alimwita ‘Mpendwa'. "Yesu, ambaye alinipa sana, alinifariji sana, alinifurahisha sana!” Kijana Pablo mwenyewe kwa hiyo aliandika Barua yake, ambapo katika hiyo anasimulia kupanda na kushuka kwa ugonjwa wake na kushiriki ushuhuda wake wa imani, iliyokabidhiwa kwa Papa wakati akiwa kwenye ndege kuelekea Lisbon na mwandishi Eva Fernández wa Radio Cope. Barua hiyo inaeleza Papa kwamba: “Sijui kama ukipokea barua hii, nitaweza kuandamana nawe katika maombi, au ikiwa Mungu, kwa huruma yake isiyo na kikomo, tayari atakuwa ameniita. Katika hali hiyo, ninatumaini kwamba ataniruhusu kukupa mkono na bora zaidi kutoka Mbinguni, nikitengeneza 'hapo' na kusherehekea, kama unavyosema.”
Alikufa akiwa Mkarmeli
Pablo Alonso Maria de la Cruz Hidalgo, alifariki mnamo tarehe Julai 15 Julai 2023. Alikufa kama Mkarmeli, kwa kujiunga na Shirika ‘articulo mortis’, na akatamka viapo vyake vya nadhiri katika chumba chake cha Hospitali ya Salamanca. Jibu lilikuwa la kujiweka wakfu wa kitawa, kwa shauku ya imani ambayo alisema alihisi katika kila nyuzi za mwili wake na hata kudhoofika kwa ugonjwa huo kwa miaka sita. Historia yake ambayo kwa njia fulani inakumbuka ile ya kijana mwingine mwenye shauku juu ya Kristo, Carlo Acutis nayo sasa zinakimbizana hadi Lisbon mikononi mwa Papa, shukrani kwa Eva Fernández, mwandishi mashuhuri wa kituo cha utangazaji cha Hispania cha Radio Cope, ambaye katika kila safari ya kitume anatofautishwa na chaguo la kipekee la karama ya kuchagua jambo pekee la kumpatia Papa Fransisko.
Shauku ya kuudhuria WYD
Hii ni barua ya baada ya kifo kutoka kwa kijana ambaye hakuweza kufika kwenye Siku ya Vijana Duniani kwa sababu alikufa siku kumi na tano zilizopita. Ni barua ya kuvutia kwa sababu aliomba kujiunga na Wakarmeli Waliotengwa muda mfupi kabla ya kifo chake, Eva alimwambia Papa ambaye alijibu mara moja: “Ndiyo, ninamjua na ninajua historia.” Wakati huo barua ile iliyotolewa kwa Papa na mwandishi wa habari ni zaidi ya zawadi, ni ushuhuda wa maisha na imani ya mvulana aliyewekwa katika hali nyeusi na nyeupe na yeye mwenyewe kwa uwazi na utulivu. Ufasaha na utulivu uleule ambao Pablo alitengeneza kumbukumbu ya mazishi yake kwa msalaba wa maua yenye maandishi “Mti wa Uzima wa Milele, ishara ya matumaini kwa sababu mwandishi wa Uzima anakaa hapo.”
Kipindi cha majaribu
Pablo, aliyezaliwa mnamo tarehe 26 Julai 2001 huko Salamanca, aligunduliwa na ugonjwa wa "Ewing's sarcoma" akiwa na umri wa miaka 16 ambao ni saratani ya uvimbe unaokua taratibu. Kilikuwa ni kipindi cha majaribu magumu sana, ambapo, hata hivyo, mvulana huyo alisema alisikia mwito wa Mungu wa maisha yaliyowekwa wakfu na kwamba alianza kusali zaidi ya yote kwa ajili ya kuongoka kwa vijana: “Ili wapate kuujua upendo wa Mungu unaodhihirishwa ndani ya Yesu. Ekaristi, na kwa ajili ya umoja wa Kanisa”. Katika barua aliyomwandikia Papa, alisimulia miaka ya ugonjwa wake kwamba: “Ninafahamu kwamba kila jambo lina sababu katika mpango wa Mungu. Kati ya kupanda na kushuka, siku bora na mbaya zaidi, na utakaso mwingi kupitia ugonjwa, leo naangalia maisha yangu na ninaweza kukiri kwamba nilikuwa na nina furaha.” Nimegundua kwamba kiini cha maisha yangu sio ugonjwa, bali Kristo. Kama nilivyowaambia marafiki zangu, familia yangu, ndugu zangu Wakarmeli: 'Kupitia mateso katika ugonjwa nilikutana na Mungu, na kupitia kifo katika ugonjwa nitamwendea. Na kwa hili ninamshukuru.”
Mungu alimfariji kipindi cha ugonjwa
Katika sehemu nyingine ya barua iliyowasilishwa kwa Baba Mtakatifu kijana Pablo aliandika kwamba angependa "kushiriki katika siku ya Vijana WYD huko Lisbon na wewe na vijana wengi kutoka duniani kote. Ninajua kutokana na uzoefu kwamba hakuna mtu anayeweza kuzima moto wa ndani ambao kijana katika upendo na Yesu anaweza kuwa nao. Ninamwomba Bwana kwamba moto huu wa upendo wa Mungu uwake huko Lisbon, na jinsi ningependa vijana kumjua Yesu, Mpendwa wangu! Alinipa sana, alinifariji sana, alinifurahisha sana! Kimwili sina nguvu, lakini ushirika wa watakatifu utaniruhusu kushiriki nanyi kwa undani zaidi na kwa njia ya karibu zaidi.”