Tafuta

Wimbi kubwa la joto duniani kuanzia tarehe 18 Julai 2023 limeendelea kusababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao nchini Ugiriki. Wimbi kubwa la joto duniani kuanzia tarehe 18 Julai 2023 limeendelea kusababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao nchini Ugiriki.   (AFP or licensors)

Janga la Moto Nchini Ugiriki Lasababisha Maafa Makubwa

Zaidi ya watu 64, 000 wamehamishiwa kwenye maeneo salama, na kwamba, hii ni operesheni kubwa kuwahi kutoka nchini Ugiriki. Visiwa vya Rhodes, Corfu na Evia vimweathirika vibaya sana. Kiwango cha nyuzi joto kinatarajiwa kupanda hadi kufikia nyuzi joto kati ya 43 hadi 45, hatari sana kwa maisha ya viumbe hai. Baba Mtakatifu Francisko ameelezea kusikitishwa kwake na madhara yaliyosababishwa na janga la moto nchini Ugiriki katika siku za hivi karibuni.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Wimbi kubwa la joto duniani kuanzia tarehe 18 Julai 2023 limeendelea kusababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao nchini Ugiriki. Zaidi ya watu 64, 000 wamehamishiwa kwenye maeneo salama, na kwamba, hii ni operesheni kubwa kuwahi kutoka nchini Ugiriki. Visiwa vya Rhodes, Corfu na Evia vimweathirika vibaya sana. Kiwango cha nyuzi joto kinatarajiwa kupanda hadi kufikia nyuzi joto kati ya 43 hadi 45, hatari sana kwa maisha ya viumbe hai. Baba Mtakatifu Francisko ameelezea kusikitishwa kwake na madhara yaliyosababishwa na janga la moto nchini Ugiriki katika siku za hivi karibuni.

Ugiriki imekumbwa na janga la moto
Ugiriki imekumbwa na janga la moto

Baba Mtakatifu katika ujumbe ulioandikwa kwa niaba yake na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican kwenda Askofu Petros Stefànou, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Ugiriki anasema, anasikitishwa sana na madhara yanayosababiswa na janga la moto Ukanda wa Nchi za Ulaya. Baba Mtakatifu anapenda kuwahakikishia ukaribu wake kwa njia ya sala na sadaka yake. Mwenyezi Mungu apende kubariki jitihada zinazoendelea kufanywa na Kikosi cha Zima Moto na wadau wengine wa shughuli za uokoaji nchini Ugiriki, ili kudhibiti janga hili la moto linaloendelea kusababisha madhara makubwa. Ni matumaini makubwa ya Baba Mtakatifu Francisko kwamba, madhara makubwa yaliyosababishwa na janga hili la moto yataamsha ari na moyo mpya wa kuongeza juhudi za ulinzi na utunzaji wa mazingira nyumba ya wote, zawadi kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Papa Ugiriki

 

 

29 July 2023, 14:03