Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 24 Julai 2023, alikutana na kuzungumza kwa faragha na Bi Robinah Nabbanja, Waziri mkuu wa Uganda. Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 24 Julai 2023, alikutana na kuzungumza kwa faragha na Bi Robinah Nabbanja, Waziri mkuu wa Uganda.  (Vatican Media)

Papa Francisko Aguswa na Huduma Kwa Wakimbizi Uganda

Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 24 Julai 2023, alikutana na kuzungumza kwa faragha na Bi Robinah Nabbanja, Waziri mkuu wa Uganda na baadaye, Jumanne tarehe 25 Julai 2023 amekutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameambatana na Askofu mkuu Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa Mambo ya Nchi za Nje, Ushirikiano na Mashirika ya Kimataifa. Papa ameguswa sana na huduma kwa wakimbizi nchini Uganda.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 24 Julai 2023, alikutana na kuzungumza kwa faragha na Bi Robinah Nabbanja, Waziri mkuu wa Uganda na baadaye, Jumanne tarehe 25 Julai 2023 amekutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameambatana na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa Mambo ya Nchi za Nje, Ushirikiano na Mashirika ya Kimataifa. Katika mazungumzo kati ya Baba Mtakatifu Francisko na Waziri mkuu wa Uganda, kwa pamoja wamepongeza uhusiano mzuri wa kidiplomasia uliopo kati ya Vatican na Uganda.

Papa Francisko akutana na ujumbe wa Waziri mkuu wa Uganda
Papa Francisko akutana na ujumbe wa Waziri mkuu wa Uganda

Baba Mtakatifu Francisko ameguswa sana na huduma ya ukarimu inayotolewa na Serikali ya Uganda kwa wakimbizi na wahamiaji ndani na nje ya Bara la Afrika kwamba, huu ni mfano bora wa kuigwa na Jumuiya ya Kimataifa. Viongozi hawa wamepongeza mchango mkubwa unaotolewa na Kanisa katika ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu nchini Uganda. Huu umekuwa ni wakati muafaka kwa viongozi hawa kujadiliana tema mbalimbali za kikanda na Kimataifa.

Waziri mkuu Uganda
26 July 2023, 14:52