Tafuta

2023.07.22 Papa na mhamiaji  Bentelo wa Camerron. 2023.07.22 Papa na mhamiaji Bentelo wa Camerron.  (© Nello Scavo - Avvenire)

Papa na Bentolo,mhamiaji aliyenusurika katika ghasia na ajali za meli

Ijumaa Julai 21,ujumbe wa 'Mediterranea Saving Humans' ulipokelewa na Papa mjini Vatican.Na pia kijana mkimbizi wa Cameroon,mfungwa wa kambi za mateso za Libya aliyetoa faraja kwa wenzake waliokuwa wakifa kuwafanya wasali kupitia simu ya mkononi iliyopatikana kwa siri pamoja na Padre Mattia Ferrari.Bentolo alitimiza ndoto ya kukutana na Papa.

Salvatore Cernuzio & Angella Rwezaula, - Vatican.

“Inawezekanaje kwamba mtu muhimu zaidi duniani anataka kukutana nami, ambaye ni mtu ambaye hana hata karatasi kwa sasa?” Bentolo ni kijana wa Cameroon ambaye mnamo mwaka 2020 alijikuta akikabiliwa na mzozo katika nchi yake. Katika njia panda, kupigana au kukimbia, alichagua chaguo la pili la kutokubali mantiki ya chuki. Kutoroka kwake, kama ilivyo kwa maelfu ya wahamiaji wa Kiafrika, kulikuwa na vurugu, kifungo, na ajali za meli. Na kutokana na uchungu wa kuwaona wenzake wakiteswa.

Mkutano wa pamoja na ‘Mediterranea Saving Humans’

Kwa hiyo manmo Ijumaa, tarehe 21 Julai 2023, kijana Bentolo alipokelewa katika mkutano na Papa Francisko katika Nyumba ya Mtakatifu  Marta mjini Vatican akiwa pamoja na Ujumbe  Shirika moja lisilo la kiserikali NGO liitwalo Mediterranea Saving Humans, lililoanzishwa na Luca Casarini (aliyekuwepo kwenye kikao cha kusikilizwa) ambaye alihakikisha kwamba “kijana anaweza kuanza upya na maisha mapya. Maisha tofauti, maisha bora au maisha tu. Kile ambacho Sami na wakimbizi wengine waliosalia Libya hawana fursa ya kukipata leo”. Akiripoti juu ya Mkutano wa tarehe 21 Julai 2023  na kusimulia historia ya mhamiaji kijana na hisia zake kabla ya baraka za Papa, Padre Mattia Ferrari,  aliyeko kwenye Shirika hilo la kibindamu katika bahari ya Mediterranea, na  ambaye katika chapisho lake kwenye Facebook pia alichapisha picha ya kikundi akiwa na Baba Mtakatifu  Huko Mtakatifu Marta, miongoni mwao ni watu wanaomsindikiza kijana Bentolo, kama vile Kátia Lôbo Fitermann, Sr Adriana, mhusika wa utunzaji wa kikanisa cha  Spin Time Labs, na mwandishi wa habari wa Mediterranea kwa ajili ya  Mediterranea kwa habari za Gazeti la Avvenire la  Baraza la Maaskofu Italia Nello Scavo, ambaye Papa Francisko alimshukuru kwa kazi yake kama mwandishi wa habari katika maeneo nyeti zaidi duniani.

Njia ya Msalaba  ya Bentolo

Scavo  mwenyewe katika gazeti la CEI alifuatilia  tena Njia ya Msalaba  ya Bentolo nchini Libya, iliyekamatwa na wasafirishaji haramu na kuuzwa kwa walinzi wa serikali ambao walimpeleka kwenye kambi rasmi ya gereza huko Zawiyah, chini ya udhibiti wa wanamgambo wa al-Nasr na timu ya  walinzi wa pwani ya meja Abdurahman al-Milad na kisha Zuara. Katika moja ya vituo vya kizuizini, kijana wa Cameroon alikuta wakimbizi wengine Wakristo walio kusini mwa jangwa la Sahara, baadhi yao wakifa baada ya kuteswa kwa miezi kadhaa na kunyimwa haki zao.

Kuwa karibu na ndugu wanaokufa

Kutoka Libya, kijana huyo alifanikiwa kuwasiliana na baadhi ya wanaharakati wa haki za binadamu, ambao wanapatika kupitia simu ya mkononi ambayo wafungwa walikuwa wameificha. Na kupitia wanaharakati hao, waliwasiliana na Padre Mattia Ferrari, ambaye alimwomba neno la faraja kwa ndugu hao waliolikuwa wanakufa. Padre huyo aliweza kusali pamoja na vijana  wafungwa, akiwasindikiza na mmoja wao hadi kifo chake. Kwa njia hiyo Bentolo alikumbusha  katika gazeti la Avvenire  kuwa  Sami alikufa na faraja ya baraka na hii ilimpatia utulivu kabla ya kuwaacha. Habari zote baadaye za Bentolo zilipotea.  Kwa mujibu wa Padre Mattia Ferrari alisema: “Tulihofia kuwa amemezwa na mfumo wa uhalifu wa Libya au kwamba alifia baharini”. Kisha siku moja meli ya uokoaji ya shirika la kibinadamu ly Ujerumani Sea Watch iliingilia kati katika Mediterania ya Kati, na kuokoa makumi ya wakimbizi waliokuwa wameanguka ndani ya maji kutoka katik mashua. Miongoni mwao alikuwa Bentolo mwenyewe ambaye, mara alipotua Italia, alijaribu tena kumtafuta padre Ferrari. Kwa hiyo Sasa yeye ni mgeni katika kituo cha mapokezi.

Kuponywa kwa kukumbatiwa na Papa

Hata hivyo, Bentolo alisema  kuwa ameponywa kutokana na majeraha hayo yote alipojikuta katika kukumbatiwa na Papa Francisko , ambaye alikuwa amejulishwa katika majuma ya  hivi karibuni kuhusu historia chungu ya kijana huyo. “Nilikuwa nikisubiri kukutana naww. Ishara yako ilinisukuma,” kijana huyo alimwambia Papa. Na kumshika mkono, alihakikisha kuwa:  “Sasa nitawaita marafiki zangu ambao bado ni wafungwa huko Libya na nitawatumia baraka za Papa”. Padre Ferrari katika chapisho lake kwenye mtandao wa kijamii, Padre Ferrari aliandikwa kuwa: “Wakati zaidi ya mwaka mmoja uliopita Bentolo aliwasiliana nasi kutoka Libya, sikufikiri ningewahi kumuona”. Kwa kuongezea alisema “Watu wengi wamekuwa wakinifundisha kuwa unapopenda lazima upigane hadi mwisho na kwamba ikiwa tunafika mwisho au miujiza itatokea. Bentolo alipigana na hatimaye kufika Ulaya. Si kwamba yuko hapa tu, lakini leo hii ameona ndoto yake ya kukutana na Papa Francisko ikitimia. Ilionekana kama ndoto isiyowezekana na ni ukweli.”

Francisko alisikiliza kijana Bentolo

Papa Francisko kwa mujibu wa Padre Ferrari aliripoti kuwa hakutaka tu kukutana na kijana  huyo Mkameruni, lakini pia alimsikiliza sana, uzoefu wake, na shauku zake. Kilichomshangaza zaidi Papa ni ukweli kwamba Bentolo, aliendelea kupenda na kusimama na wenzake katika shida hata alipokuwa Libya, katika hali mbaya.” Alisisitiza Padre Ferrari.

Hali ya kinyama nchini Tunisia na Libya

Padre huyo aliripoti kwamba wakati wa Mkutano na Papa pia kulikuwa na mazungumzo juu ya hali ya kinyama ambayo wahamiaji wengine wengi nchini Tunisia na Libya wanapitia. Hali halisi  iliyowakilishwa na picha hiyo, ilisambazwa katika saa chache zilizopita kwenye tovuti, ya mwanamke akiwa na binti yake wa miaka 5 kando yake, ambaye alikufa jangwani kutokana na njaa, joto na kiu. Picha ambayo hata Papa aliweza kuiona na mbele yake alionesha uchungu wake.

24 Julai 2023, 14:49