Kardinali  Matteo Zuppi amemekuwa mjumbe tena wa Papa huko Washington Marekani kwa tarehe 17-19 Juali 2023. Kardinali Matteo Zuppi amemekuwa mjumbe tena wa Papa huko Washington Marekani kwa tarehe 17-19 Juali 2023. 

Kard.Matteo Maria Zuppi akutana na Rais Joe Biden

Katika barua iliyotolewa na Ikulu ya Marekani mwishoni mwa mazungumzo na mjumbe wa Papa yaliyochukua muda wa saa mbili,inabanisha kuwa Biden alitoa salamu za heri kwa kuendelea kwa huduma na uongozi wa kimataifa wa Papa Francisko na alikaribisha uteuzi wa hivi karibuni wa kardinali mpya,askofu mkuu wa Marekani.

Na Angella Rwezaula, -Vatican.

Kardinali Matteo Maria Zuppi, askofu mkuu wa Bologna na rais wa Baraza la Maaskofu wa Italia Rais (CEI) alikutana na Rais Joe Biden wa Marekani jioni tarehe 18 Julai 2023 kama mjumbe maalum wa Baba Mtakatifu Francisko. Katika barua iliyotolewa na Ikulu ya Marekani mwishoni mwa mazungumzo hayo ambayo yalichukua muda wa saa mbili, inaelezwa kuwa Rais Biden “alitoa salamu za heri kwa kuendelea kwa huduma na uongozi wa kimataifa wa Papa Francisko na “alikaribisha uteuzi wa hivi karibuni kama kardinali mmojawapo  wa askofu mkuu wa Marekani”. Katika  jitihada za Vatican katika kutoa misaada ya kibinadamu ili kukabiliana na mateso yaliyoenea yaliyosababishwa na uvamizi wa Urussi unaoendelea nchini Ukraine, pamoja na dhamira ya Vatican ya kuruhusu kurejea kwa watoto wa Ukraine waliopelekwa kwa  nguvu katika maeneo yaliyothibitiwa ya Urussi zilijadiliwa.

Kwa mujibu wa Serikali ya Ukraine inasemekana kwamba wanaweza kuwa ni zaidi ya watoto 19,000 au zaidi waliopelekwa huko, ambapo hiyo ni mada ambayo tayari Rais wa Ukrane Volodymir Zelensky alikuwa ameomba msaada Vatican wakati wa Mkutano aliokoutana na Baba Mtakatifu mjini Vatican mnamo mwezi Mei mwaka huu na ambayo Kardinali Zuppi mwenyewe alikabiliana nayo katika hatua za awali za utume wake huko, Kyiv mnamo  (Juni 5-6) na Moscow (Juni 28-29). Kwa namna ya pekee katika Urussi Kardinali  Zuppi alikuwa ameijadili na Yuri Ushakov, mshauri wa Vladimir Putin kwa ajili ya sera ya kigeni, na Maria Lvova-Belova, kamishna wa rais wa Shirikisho la Urussi kuhusu haki za watoto. Tovuti ya kamishna huyo pia ilithibitisha hilo, ikichapisha picha ya ziara ya Kadinali  Zuppi na kueleza kuwa katika mazungumzo hayo masuala ya kibinadamu yanayohusiana na “operesheni za kijeshi” na ulinzi wa haki za watoto yalijadiliwa.

Kwa sasa mwelekeo mpya umekuwa Washington, ambapo Zuppi alikwenda tangu Julai 17 na kuhitimisha Jumatano 19 Julai 2023, akifuatana na afisa wa Sekretarieti ya Vatican. Katika mji mkuu wa Marekani, Kadinali Zuppi askofu mkuu wa Bologna, kabla ya kwenda kumwona Biden, alitembelea Capitol Hill, makao ya Bunge kwa ajili ya mkutano na baadhi ya wabunge wa Marekani. Muda mfupi kabla ya mkutano huo balozi wa Vatican huko Marekani Askofu Mkuu Christophe Pierre, mmoja wa makadinali wa baadaye aliyechaguliwa na Baba Mtakatifu ambaye atasimikwa rasimu tarehe 30 Septemba, alitangaza kwenye baadhi ya vituo vya televisheni kwamba lengo la utume wa Kardinali Zuppi ni “kuzungumza, kusikiliza na kusikilizwa.”.                                                                                                                                             

Rais Joe Biden, aliongeza Kardinali mteule, “siku zote amekuwa na umakini mkubwa kwa Baba Mtakatifu.” Wazo la jumla ni “kuchangia amani, na haswa zaidi kuingia katika nyanja ya kibinadamu, haswa kuhusu watoto. Majadiliano yanahusu hili”, mjumbe huyo aliviambia vyombo vya habari, ikiwa ni pamoja na gazeti la Repubblica. “Hili ndilo dhumuni mahususi la kardinali, na ni dhahiri la Papa, pia kwa sababu ni thabiti. Ni wazi, hata hivyo, wazo ni kufikiria amani, katika mazingira magumu yaliyopo. Kardinali ana uhalisia sana, tujaribu kufanya kila linalowezekana.”

Mjumbe wa Papa huko Marekani Kardinali Zuppi,Rais wa CEI
19 July 2023, 15:30