Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Askofu msaidizi Michele Di Tolve kuwa ni Gambera wa Seminari kuu ya Kipapa ya Jimbo kuu la Roma. Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Askofu msaidizi Michele Di Tolve kuwa ni Gambera wa Seminari kuu ya Kipapa ya Jimbo kuu la Roma. 

Askofu Msaidizi Michele Di Tolve, Gambera Seminari Kuu ya Roma: Tamko la Papa Francisko

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 26 Mei 2023 akamteuwa Monsinyo Michele Di Tolve kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo kuu la Roma, na sasa anatamka kwamba, Askofu msaidizi Michele Di Tolve amekabidhiwa jukumu la kuimarisha mahusiano kati ya hali halisi ya malezi ya Kipadre eneo la Jimbo kuu la Roma sanjari na kuratibu shughuli zake kwa makubaliano na Askofu msaidizi Baldassarre Reina, Makamu Gambera. Hii ni sehemu ya Tamko la Papa Francisko!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Katika Tamko la Baba Mtakatifu Francisko kuhusu malezi ya Kipadre katika eneo la Jimbo kuu la Roma na uteuzi wa Gambera wa Seminari kuu ya Kipapa ya Jimbo kuu la Roma anasema, tarehe 6 Januari 2023 alitangaza Katiba ya Kitume ijulikanayo kama “In Ecclesiarum communione” yaani “Katika Ushirika wa Makanisa” kuhusu Vikarieti ya Jimbo kuu la Roma na kuwakabidhi Maaskofu wasaidizi maeneo na huduma za kichungaji, Jimbo kuu la Roma; na tarehe 26 Mei 2023 akamteuwa Monsinyo Michele Di Tolve kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo kuu la Roma.

Seminari kuu ya Kipapa ya Jimbo kuu la Roma
Seminari kuu ya Kipapa ya Jimbo kuu la Roma

Baba Mtakatifu anatamka kwamba, Askofu msaidizi Michele Di Tolve amekabidhiwa jukumu la kuimarisha mahusiano kati ya hali halisi ya malezi ya Kipadre eneo la Jimbo kuu la Roma sanjari na kuratibu shughuli zake kwa makubaliano na Askofu msaidizi Baldassarre Reina, Makamu Gambera. Ni katika muktadha huu, Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Askofu msaidizi Michele Di Tolve kuwa ni Gambera wa Seminari kuu ya Kipapa ya Jimbo kuu la Roma na kwamba, atatekeleza dhamana na wajibu wake kwa makubaliano na Baraza la Maaskofu. Kwa mambo muhimu na mazito, atafanya rejea moja kwa moja kwa Baba Mtakatifu mwenyewe. 

Papa Tamko

 

06 Julai 2023, 14:28