Tafuta

 Ilikuwa ni tarehe 22 Juni 1983, miaka 40 iliyopita, Emanuela Orlandi, raia wa mji wa Vatican alipotoweka katika mazingira ya kutatanisha. Ilikuwa ni tarehe 22 Juni 1983, miaka 40 iliyopita, Emanuela Orlandi, raia wa mji wa Vatican alipotoweka katika mazingira ya kutatanisha.  (ANSA)

Papa Francisko: Kumbukizi ya Miaka 40 Tangu Alipotoweka Emanuela Orlandi

Papa ametumia fursa hii, kuonesha uwepo wake wa karibu kwa familia ya Emanuela Orlandi katika kumbukizi ya miaka 40 tangu alipotoweka katika mazingira ya kutatanisha. Ukaribu huu ameuonesha hasa kwa Mama mzazi wa Emanuela Orlandi ambaye amemhakikishia sala na sadaka yake. Baba Mtakatifu ametumia pia fursa hii, kuwakumbuka na kuwaombea wale wote wanaoteseka kutokana na machungu ya kuondokewa na ndugu zao katika mazingira ya kutatanisha.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Ilikuwa ni tarehe 22 Juni 1983, miaka 40 iliyopita, Emanuela Orlandi, raia wa mji wa Vatican alipotoweka katika mazingira ya kutatanisha na hadi leo hii, juhudi za kumpata akiwa hai au masalia yake zimegonga mwamba. Baba Mtakatifu Francisko, Dominika tarehe 25 Juni 2023 mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican ametumia fursa hii, kuonesha uwepo wake wa karibu kwa familia ya Emanuela Orlandi katika kumbukizi ya miaka 40 tangu alipotoweka katika mazingira ya kutatanisha. Ukaribu huu ameuonesha hasa kwa Mama mzazi wa Emanuela Orlandi ambaye amemhakikishia sala na sadaka yake. Baba Mtakatifu ametumia pia fursa hii, kuwakumbuka na kuwaombea wale wote wanaoteseka kutokana na machungu ya kuondokewa na ndugu zao katika mazingira ya kutatanisha.

Watu 40 wamefariki dunia kutokana na ghasia ndani ya gereza.
Watu 40 wamefariki dunia kutokana na ghasia ndani ya gereza.

Wakati huo huo habari kutoka Honduras zinabainisha kwamba, tarehe 20 Juni 2023 ghasia kubwa zimezuka kwenye gereza la wanawake lililoko Támara, nchini Honduras. Wachunguzi wa mambo nchini Honduras wanasema kwamba, haya ni matokeo ya kinzani kati ya wanachama wa magenge ya “MS-13 na 18th Street.” Takwimu zinaonesha kwamba, watu 40 walipoteza maisha, wengi wao wamepoteza maisha kutokana na moto uliozuka wakati wa machafuko hayo. Vyombo vya ulinzi na usalama nchini Honduras vimeanza kufanya uchunguzi wa kina kuhusiana na mauaji haya. Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana, ameonesha masikitiko makubwa kutokana na mauaji yaliyofanyika kwenye Gereza la wanawake huko Támara, nchini Honduras. Baba Mtakatifu anawaombea marehemu msamaha, maisha na uzima wa milele. Bikira Maria wa Suyapa, Mama wa Honduras asaidie nyoyo za watu kufunguka kwa ajili ya upatanisho wa Kitaifa na hivyo kutengeneza mazingira yatakayowawezesha kuishi vyema na kidugu hata ndani magereza yenyewe.

Papa Orlandi
26 June 2023, 15:23