Papa Francisko:Kuna haja ya kuwa na uchumi fungamani kwa ajili ya wema wa wote
Na Angella Rwezaula, - Vatican
Baba Mtakatifu Francisko akikutana Jumatatu tarehe 5 Juni 2023 mjini Vatican na wanachama wa Taasisi ya Mfuko wa Centesimus Annus pro Pontifice, ambayo mwaka huu 2023 inaadhimisha miaka thelathini tangu kuanzishwa kwake kwa mkutano wa kimataifa ambao umeanza tarehe 5 Juni, unaoongozwa na kauli mbiu: ‘Kumbukumbu ya kujenga mustakabali: kufikiri na kutenda masharti ya jumuiya’. Kwa hiyo Papa amesema “Yote yalianza baada ya barua ya Mtakatifu Yohane Paulo II iliyoandikwa katika kumbukumbu ya miaka mia moja ya Waraka wa kitume wa Rerum novarum wa Papa Leo XIII. Papa ametaja barua zake za kitume za Laudato si' na Fratelli tutti, Wosia wake wa Evangelii Gaudium na pia rais wa zamani wa Mahakama ya Katiba Paolo Grossi na mshairi wa Milano Giampiero Neri, Papa Francisko, amethibitisha kuwa “hakuna kufanya uchumi ambao unaua na unazalisha taka”. Vile vile amekumbuka Injili na onyo “la Yesu la kutotumikia mabwana wawili kuepuka athari za uharibifu wa milki ya fedha: kulazimishwa kuhama, uhamiaji, biashara ya binadamu, madawa ya kulevya, vita, vurugu.” Katika hilo ndipo amezindua tena changamoto ya kujenga ulimwengu ambapo kila mtu anaweza kupata nafasi yake na Jumuiya inayojua kutoa sauti kwa wasio na sauti ndiyo tunayohitaji sote.”
Katika hotuba hiyo Papa Francisko mebainisha kwamba jitihada zao zimewekwa kwa usahihi kwenye njia hiyo, katika tamaduni. Kwa maneno mengine, kujitolea kusoma na kueneza mafundisho Jamii ya Kanisa, kujaribu kuonesha kwamba si nadharia tu, lakini inaweza kuwa maisha ya adili ambayo kwayo kukuza jamii zinazostahili mwanadamu. Katika hotuba yake, Papa Francisko kwa hiyo ameorodhesha mada kuu katika kitovu cha kazi ya msingi katika miongo hii mitatu: Kitovu cha mtu, manufaa ya wote, mshikamano na usaidizi. Changamoto zilibadilishwa kuwa vitendo madhubuti na kuzinduliwa tena na michango ambayo Papa Francisko, katika miaka yake kumi ya upapa, amejaribu kufanya kwa maendeleo ya mafundisho jamii ya Kanisa.
Mada ya uchumi, pia, ni msingi wa jitihada za Mfuko wa Centesimus Annus. Na, katika suala hilo, Papa amerejea Wosia wake wa kitume wa Evangelii gaudium kuonya juu ya hatari ya kuishi uchumi kwa njia isiyofaa. Uchumi huu unaua alisema mwaka 2013, huku akishutumu mfano wa kiuchumi unaozalisha taka na ambao unapendelea kile kinachoweza kufafanuliwa kama utandawazi wa kutojali. Hakuna mengi ambayo yamebadilika tangu wakati huo, kwa hivyo kujitolea sawa kunahitajika amesisitiza: “Wengi wenu mnafanya kazi katika uwanja wa uchumi: mnajua vyema jinsi njia ya kufikiria ukweli ambayo inamweka mtu kituoni, ambayo haimpunguzii mfanyakazi na ambayo unamsaidia ili kujaribu kuunda wema kwa wote.”
Mtazamo wa Baba Mtakatifu umehamia kwenye masuala ya mazingira. Waraka wa Laudato si' ambao ulimulika juu ya uharibifu uliosababishwa na dhana kuu ya kiteknolojia na kupendekeza mantiki ya ikolojia fungamani ambapo 'kila kitu kimeunganishwa', 'kila kitu kinahusiana' na suala la mazingira haliwezi kutenganishwa na suala la kijamii”. Kwa hiyo ni kutunza mazingira na makini na maskini kusimama au kuanguka pamoja. Baada ya yote, hakuna mtu anayejiokoa mwenyewe na ugunduzi upya wa udugu na urafiki wa kijamii ni uamuzi wa kutoanguka katika ubinafsi ambao humfanya mtu kupoteza furaha ya kuishi,” Papa amesisitiza
Papa Francisko akiendelea, amesisitiza kwamba kwa kufikiri na kutenda kulingana na jumuiya ambayo inatoa jina la mkutano wa Mfuko. Amenukuu kutoka kifungu cha 116 Waraka wa Fratelli tutti yaani Wote ni ndugu. Kiuhalisia,Papa Francisko anakumbusha, maneno hayo yanatoka kwenye hotuba kwa Harakati maarufu mwaka 2014 wakati Papa alipotoa ushauri wa "kupambana dhidi ya sababu za kimuundo za umaskini, ukosefu wa usawa, ukosefu wa kazi, ardhi na makazi, kunyimwa haki za kijamii na kazi. Akizungumzia juu ya fedha , Papa bila kusoma amenukuu kifungu cha Injili ambamo Yesu anatuambia kwamba mabwana wawili hawawezi kutumikiwa: ama unamtumikia Mungu, Bwana, au unamtumikia, (shetani) lakini hakusema shetani bali alisema fedha”. Kwa kurudia amesema “Ama unamtumikia Mungu, au unatumikia pesa. Mbaya kuliko shetani. Tunapaswa kuangalia Yesu anamaanisha nini kwetu katika hili, kuna ujumbe: ama unamtumikia Mungu au ni mtumishi wa pesa, hauko huru”.
Katika hotuba ya Papa, pia mawazo yake yamekwenda kwa mwanasheria mkuu wa Italia, Paolo Grossi ambaye alikuwa ni rais wa zamani wa Mahakama ya Katiba, ambaye alifariki mwaka 2022. “Jumuiya daima ni uokoaji kwa wanyonge na inatoa sauti hata kwa wale ambao hawana sauti kabisa”, aliandika katika Fasii ya Sheria. Pengine, ili jamii iwe kweli mahali ambapo wanyonge na wasio na sauti wanaweza kujisikia kukaribishwa na kusikilizwa, kila mtu anahitaji zoezi hilo ambalo tunaweza kuliita ‘kutengeneza nafasi. Kila mtu anaonesha “mimi) mwenyewe kidogo na hii inaruhusu nyingine kuwepo. Lakini ili kufanya hivyo, Papa Francisko amesema, “msingi wa jumuiya lazima uwe maadili ya zawadi na si ya kubadilishana.” Ametoa mkazo.
Papa amesisitiza kuwa ndivyo alivyokuwa anazungumza mshairi wa Milano, Giampiero Neri, ambaye aliaga dunia hivi karibuni akisema: “Inasemwa kuhusu baadhi ya watu ambao, wanapoingia kwenye chumba, hukimiliki chote kabisa. Ninapaswa kufikiria kwamba, wanapoondoka, wanaacha utupu mkubwa. Badala yake, nina mwelekeo wa kufikiria kuwa ni watu wanyenyekevu, wakimya ambao wanaacha utupu mkubwa, na ambao wanachukua nafasi ya lazima tu, wanaojifanya kupendwa.” Baba Mtakatifu kwa kuhitimisha amebainisha kuwa hitaji la kufikiri na kutenda kulingana na jumuiya maana yake ni kutoa nafasi kwa ajili ya wengine, maana yake ni kuwaza na kufanya kazi kwa ajili ya siku zijazo ambapo kila mtu anaweza kupata nafasi yake na kuwa na nafasi yake duniani. Kwa hiyo kuchangia mawazo na hatua inayopendelea ukuaji wa jumuiya ambayo itatembea pamoja kwenye njia ya amani.