Papa Francisko:bidii ya kitume haigeuzi kamwe watu inavutia
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Ikiwa ni mwendelezo wa ada kuhusu ari na juhudi za Utume, wa Uinjilishaji, katika katekesi ya Baba Mtakatifu, Jumatano tarehe 7 Juni 2023, katika uwanja wa Mtakatifu Petro kwa waamini na mahujaji waliofika, ameanza kwa kuwaonesha kuwa mbele yao kulikuwa na Sanduku la Masalia ya Mtakatifu Teresa wa Mtoto Yesu, Msimamizi wa Ulimwengu wa Utume wa kimisionari. “Ni vizuri kwamba hicho kikatendeka wakati tunatafakari juu ari kwa ajili ya uinjilishaji na bidii ya kitume.” Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu amesema siku hiyo kuacha kusaidiwa na ushuhuda wa Mtakatifu mdogo Teresa. Yeye alizaliwa miaka 150 iliyopita na katika mwaka huu, Papa ametangaza nia ya kuandika Barua ya kitume kuhusu yeye.
Ni msimamizi wa utume wa kimisionaria lakini hakuwahi kwenda kwenye utume. Je ni jinsi gani ya kueleza hilo? Papa ameuliza na kujibu. Yeye alikuwa ni mtawa mkarmeli na maisha yake yalikuwa yanafanywa na mambo madogo na udhaifu. Yeye mwenyewe alijifafanua kuwa “chembe ndogo ya mchanga”. Kwa afya mbaya, alikufa akiwa na umri wa miaka 24. Lakini ikiwa mwili wake ulikuwa mgonjwa, moyo wake ulikuwa mchangamfu, alikuwa mmisionari. Katika shajara yake anasema kwamba kuwa mmisionari ilikuwa shauku yake na kwamba alitaka kuwa mmoja si kwa miaka michache tu, bali kwa maisha yake yote, kiukweli hadi mwisho wa dunia. Teresa alikuwa dada wa kiroho wa wamisionari kadhaa: kutoka katika monasteri aliwasindikiza kwa barua zake, kwa sala na kwa kuwatolea sadaka za mfululizo. Bila kuonekana, aliombea wamisionari, kama injini ambayo, ikiwa imefichwa, huipatia gari nguvu ya kwenda mbele. Walakini, mara nyingi hakueleweka na dada zake watawa: alipokea kutoka kwao ‘miiba zaidi ya waridi’, lakini alikubali kila kitu kwa upendo, kwa uvumilivu, sadaka, pamoja na ugonjwa wake, pia hukumu na kutokuelewana.
Naye alifanya hivyo kwa furaha, na alifanya hivyo kwa ajili ya mahitaji ya Kanisa, ili, kama alivyosema, “mawaridi yatawanyike juu ya kila mtu,” hasa kwa walio mbali zaidi. "Lakini sasa, Papa alisema ninajiuliza, je, tunaweza kujiuliza, bidii hii yote, nguvu hii ya kimisionari na furaha hii ya maombezi inatoka wapi? Vipindi viwili vinatusaidia kuelewa hili, vipindi viwili vilivyotokea kabla ya Teresa kuingia kwenye monasteri. Jambo la kwanza lilihusu siku ambayo ilibadilisha maisha yake, siku moja maisha yake yalibadilika ambayo ilikuwa ni Siku ya Noeli ya 1886, wakati Mungu alipofanya muujiza moyoni mwake. Teresa alikuwa atimize miaka 14 muda mfupi baadaye. Akiwa mtoto mdogo, alibembelezwa na kila mtu ndani ya nyumba hiyo, lakini hakukomaa."
Baba yake akirudikutoka Misa ya usiku wa manane, amechoka sana, hata hivyo, hakuwa na hamu ya ufunguzi wa zawadi za binti yake na akasema: “Afadhali huu ni mwaka wa mwisho!” Kwa sababu miaka 15 tayari hawatoi tena zawadi. Teresa, mwenye tabia nyeti sana na mwenye tabia ya kutokwa na machozi, aliposika hivyo ajisikia vibaya, akaenda hadi chumbani kwake na kulia. Lakini alikandamiza machozi haraka, akashuka na, akiwa amejawa na furaha, ni yeye aliyemchangamsha baba yake. Nini kilikuwa kimetokea? Kwamba katika usiku ule, ambao Yesu alikuwa amedhoofika kwa sababu ya upendo, alikuwa amekuwa na nguvu katika roho muujiza wa kweli: katika dakika chache alikuwa ametoka katika gereza la ubinafsi wake na kujisikitikia; na akaanza kuhisi kwamba msaada uliingia moyoni mwake hivyo alijesemea, kwa haja ya kujisahau” (taz maandiko yake A, 133-134).
Tangu wakati huo na kuendelea alielekeza bidii yake kwa wengine, ili wapate kumpata Mungu na badala ya kujitafutia faraja aliazimia “kumfariji Yesu, ili kuzifanya roho zimpende”, kwa sababu Teresa alibainisha kwamba : Yesu anaumwa na ugonjwa wa upendo unaweza kuponywa tu kwa upendo”,(Barua kwa Marie Guérin, Julai 1890). Hili basi ndilo azimio la kila siku yake: “kumfanya Yesu apendwe” ( Barua kwa Céline, Oktoba 15, 1889), kuombea ili wengine wampende. Aliandika: “Ningependa kuokoa roho na kujisahau kwa ajili yao: Ningependa kuwaokoa hata baada ya kifo changu” (Barua kwa Padre Roullan, 19 Machi 1897). Mara kadhaa alisema: “Nitatumia mbingu yangu kufanya mema duniani”. Hiki ni kipindi cha kwanza ambacho kilibadilisha maisha yake akiwa na umri wa miaka 14.
Na bidii yake ilikuwa inawaelekeza hasa wadhambi na walio mbalu. Kipindi cha pili kinafichua. Inafurahisha: Teresa alisikia juu ya mhalifu aliyehukumiwa kifo kwa uhalifu wa kutisha, jina lake alikuwa Enrico Pranzini aliandika jina lake: kupatikana na hatia ya mauaji ya kikatili ya watu watatu, alikusudiwa kupigwa risasi, lakini hataki kupokea faraja za imani. Teresa alimchukua moyoni na kufanya kila awezalo na aliomba kwa kila njia kwa ajili ya uongofu wake, ili yule ambaye, kwa huruma ya kidugu, alimwita "mnyonge Pranzini, awe na ishara ndogo ya kuomba toba na kutoa nafasi kwa huruma ya Mungu, ambayo Teresa alikuwa akiamini kwa upofu.
Utekelezaji unafanyika. Siku iliyofuata Teresa alisoma kwenye gazeti kwamba Pranzini, kabla tu ya kuweka kichwa chake juu ya jukwaa la kuuliwa, ghafla, akiwa ameshikwa na msukumo wa ghafla, aligeuka, akachukua msalaba ambao kuhani aliwasilisha kwake na kubusu majeraha matakatifu mara tatu. Mtakatifu anatoa maoni kwamba “Kisha roho yake ikaenda kupokea hukumu ya huruma ya Yule aliyetangaza kwamba Mbinguni kutakuwa na furaha zaidi kwa mwenye dhambi mmoja anayetubu kuliko kwa watu tisini na tisa wenye haki ambao hawana haja ya kutubu!”(maandishi yake A, 135). Papa aliongeza kusema, hapa kuna nguvu ya maombezi inayoongozwa na upendo, hapa ni injini ya utume. Wamisionari, ambao Teresa ni msimamizi wao, si wale tu wanaosafiri safari ndefu, kujifunza lugha mpya, kufanya kazi nzuri na ni wazuri katika kutangaza; lakini pia , mmishonari ni mtu yeyote anayeishi, mahali popote alipo, kama chombo cha upendo wa Mungu; ndiye afanyaye yote ili, kwa ushuhuda wake, maombi yake, maombezi yake, Yesu apite.
“Na hii ni bidii ya kitume ambayo, tukumbuke daima, kamwe haifanyi kazi kwa ajili ya kugeuza watu imani, au kwa kulazimishwa! -, lakini kwa mvuto: imani huzaliwa na mvuto, mtu hawi Mkristo kwa kulazimishwa na mtu, hapana, lakini kwa sababu ameguswa na upendo. Kanisa, kabla ya njia nyingi, mbinu na miundo, ambayo wakati mwingine hukengeusha kutoka katika muhimu, inahitaji mioyo kama ya Teresa, mioyo inayovutia upendo na kutuleta karibu na Mungu”, Papa amehimiza. Papa ameomba tumuombe mtakatifu na ambapo masalia yake yalikuwa hapo katika Uwanja neema ya kushinda ubinafsi wetu na kuomba shauku ya kufanya maombezi, ili mvuto huu uwe mkubwa zaidi kwa watu na Yesu ajulikane na kupendwa, amehitimisha.
Nb: katika uwanja wa Mtakatifu Petro, pia kulikuwapo na masalia ya wazazi wa Mtakatifu mdogo Teresa wa Mtoto Yesu.