Tafuta

Papa:Kristo alipaa mbinguni kupeleka ubinadamu wetu kwa Mungu na kutuombea

Dominika 21 Mei ni siku ya Kupaa kwa Bwana ambayo imeadhimishwa nchini Italia na makanisa duniani ambapo,Papa amefafanua maswali mawili katika tafakari yake: kwa nini kusherehekea kuondoka kwa Yesu duniani?anafanya nini sasa mbinguni? Jibu alipeleka ubinadamu wetu mbele za Baba na kuwasilisha kwake majeraha ya wanadamu.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Dominika tarehe 21 Mei 2023, wakati mama Kanisa Mahalia anaadhimisha Siku kuu ya Kupaa kwa Bwana, sambamba na maadhimisho ya Siku ya 57 ya Upashanaji Habari Ulimwenguni, ametoa tafakari yake kwa waamini na mahujaji wote waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican. Akianza tafakari hiyo amesema. Leo nchini Italia na katika nchi nyingine nyingi Kupaa kwa Bwana kunaadhimishwa. Ni sherehe ambayo tunaijua vyema, lakini ambayo inaweza kuzua maswali, angalau mawili. Swali la kwanza: kwa nini kusherehekea kuondoka kwa Yesu duniani? Inaweza kuonekana kuwa kutengana kwake kungekuwa wakati wa kusikitisha, na kitu… kwa usahihi cha kufurahiya! Na kwa nini kusherehekea kuondoka? Swali la pili: Yesu anafanya nini sasa mbinguni? Na kwa nini kusherehekea?" Ni maswali ya Papa aliyorudia kuuliza.

Waamini katika uwanja wa Mtakatifu petro kusali sala na Papa
Waamini katika uwanja wa Mtakatifu petro kusali sala na Papa

Kwa nini tunasherehekea. Baba Mtakatifu amesema kwa sababu pamoja na Kupaa kitu kipya na kizuri kilitokea: Yesu alichukua ubinadamu wetu, mwili wetu hadi mbinguni, ni mara ya kwanza; yaani, aliupeleka mbele za Mungu. Huo ubinadamu, ambao alikuwa ameutwaa duniani, haukubaki hapa, baada ya Yesu Mfufuka hakuwa Roho, kiukweli alikuwa na mwili wa binadamu, nyama, mifupa, kila kitu; na atakuwa huko milele. Tunaweza kusema kwamba tangu siku ya Kupaa Mungu mwenyewe amebadilika" tangu wakati huo yeye si roho tena, lakini kadiri anavyotupenda anabeba ndani yake mwili wetu wenyewe, ubinadamu wetu! Kwa hivyo, mahali ambapo ni mali yetu imeoneshwa, hatima yetu iko hapo. Ndivyo alivyoandika Baba mmoja wa zamani katika imani: “Habari njema! Yeye aliyefanyika mtu kwa ajili yetu [...], ili kutufanya ndugu zake, anajionesha kama mwanadamu mbele za Baba, ili kuwaleta pamoja naye wote walio ndugu zake", (Hotuba ya Mtakatifu Gregori wa Nissa, juu ya ufufuko wa Kristo, 1)  na hii ndiyo tunayoadhimisha leo ushindi wa mbinguni: Yesu anayerudi kwa Baba, lakini pamoja na ubinadamu wetu. Na kwa hivyo mbingu  yetu kidogo, ni tayari. Yesu amefungua mlango na mwili wake huko pale.

Sala ya Malkia wa Mbingu
Sala ya Malkia wa Mbingu

Kuhusu swali la pil, Yesu anafanya nini mbinguni?  Baba Mtakatifu amesisitiza kwamba anasimama kwa ajili yetu mbele za Baba, daima anamwonesha ubinadamu wetu, anaonesha majeraha. Kwa kuongeza amesema “Ninapenda kufikiria kwamba Yesu, mbele ya Baba, anaomba hivi: akimuonesha majeraha yake ”. "Hivi ndivyo nilivyoteseka kwa ajili ya watu, fanya kitu! Anamuonesha gharama ya ukombozi. Baba anakuwa na hisia kali. Hili ni jambo ninalopenda kufikiria... lakini ni kufikiria kwamba  Yesu anaomba. Hajatuacha peke yetu. Hakika, kabla ya kupaa alituambia, kama  katika Injili ilivyo sema kuwa: Mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari” (Mt 28:20).

Sala la Malkia wa Mbingu
Sala la Malkia wa Mbingu

Yeye yuko pamoja nasi daima, anatutazama, “yu hai pamoja nasi sikuzote, ili kutuombea” (Eb 7:25 ). Kuonesha majeraha kwa Baba, kwa ajili yetu. Kwa neno moja, Yesu anaomba; yuko katika mahali bora zaidi, mbele ya Baba yake na baba yetu, ili kutuombea. Maombezi ni muhimu. Imani hii inatusaidia sisi pia: tusikate tamaa, tusivunjike moyo. Mbele za Baba kuna mtu anayemwonesha majeraha na maombezi. Malkia wa Mbinguni atusaidie kufanya maombezi kwa nguvu ya maombi, amehitimisha.

Tafakari ya Papa na wito kwa ajili ya Sudan na Ukraine
21 May 2023, 13:01