Tafuta

Vita nchini Sudan vinaendelea kuleta madhara kwa watu na tafia zima. Papa anaomba Jumuiya ya Mataifa kuingilia kati. Vita nchini Sudan vinaendelea kuleta madhara kwa watu na tafia zima. Papa anaomba Jumuiya ya Mataifa kuingilia kati.  (AFP or licensors)

Papa Francisko:wito kwa ajili ya Sudan na Ukraine:tusizoee vita!

Kwa mara nyingine tena mara baada ya sala ya Malkia wa Mbingu amekumbua hali ya nchini Sudan na pia kuonesha tena ukaribu na watu wa Ukraine waliouawa.Amekumbusha Siku ya Maadhimisho ya Mawasiliano duniani na Juma la Laudato Si.

Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Dominika tarehe 21 Mei 2023, mara baada ya Sala ya Malkia wa Mbingu kwa mahujaji na waamini waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu amesema: “Inasikitisha lakini, ni mwezi mmoja baada ya kuzuka kwa ghasia nchini Sudan, hali inaendelea kuwa mbaya. Katika kuhimiza makubaliano ya sehemu yaliyofikiwa hadi sasa, ninarudia ombi langu la dhati la kutaka silaha ziwekwe chini na ninaiomba jumuiya ya kimataifa isiache juhudi zozote za kufanya mazungumzo kutawala na kupunguza mateso ya watu. Tafadhali, tusizoee migogoro na vurugu. Tusizoee vita tafadhali. Na tunaendelea kuwa kidete  na watu wa Kiukraine waliouawa."

Siku ya upashanaji habari Duniani

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea amesema kuwa: “Leo ni Siku ya Hupashanaji habari Ulimwenguni  yenye kaulimbiu ya "Kuzungumza kutoka moyoni". Moyo ndio unaotusukuma kuelekea mawasiliano ya wazi na ya kukaribisha. Nawasalimu waandishi wa habari na waendesha mawasiliano waliopo hapa, ninawashukuru kwa kazi yao na ninatumaini kuwa watakuwa daima katika huduma ya ukweli na manufaa ya wote". Papa amependa kuwapongeza na kuomba umati  uwapigie  makofi waandishi wa habari wote...!

Juma la Laudato si

Baba Mtakatifu akiendelea amesema: “Leo linaanza Juma la Laudato Si'. Ninaishukuru Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu na asasi nyingi zinazofuata; na ninakaribisha kila mtu kushirikiana kwa ajili ya utunzaji wa nyumba yetu ya pamoja: kuna haja kubwa ya kuchanganya ujuzi na ubunifu! Maafa ya hivi karibunipia yanatukumbusha hilo, kama vile mafuriko ambayo yamekumba Emilia Romagna katika siku za hivi karibuni ambayo yamesababishwa kwa idadi ya watu wake ninapyaisha kwa moyo kuonesha ukaribu wangu.”

Vijitabu vya Laudato Si katika uwanja wa Mtakatifu Petro

Kuhusiana na suala la Juma la Laudato Si, aidha Papa Baba amesema:“ Vijitabu kuhusu Laudato si', ambavyo Baraza la Kipapa limetayarisha kwa ushirikiano na Taasisi ya Mazingira ya Stockholm, sasa vitasambazwa katika Uwanja” . Akiendelea amewasalimia mahujaji na waamini wote kuanzia na Warumi na mahujaji kutoka Italia na kutoka nchi nyingi, kwani ameona bendera nyingi  uwanjani, na kuwakaribisha wote. “Ninawasalimu hasa Masista Wafransiskani wa Mtakatifu Elizabeth kutoka Indonesia, ni kutoka mbali, waamini kutoka Malta, Mali, Argentina, kisiwa cha Karibea cha Curaçao na bendi ya muziki ya Puerto Rico. Ameongea “Tungependa kusikia mkicheza baadaye!”

Bendi kutoka Puerto Rico ilikuwa  Uwanja wa Mtakatifu  Petro.
Bendi kutoka Puerto Rico ilikuwa Uwanja wa Mtakatifu Petro.

Amewasalimia wanahija wa jimbo la Alexandria; vijana wa Kipaimara kutoka jimbo la  Genova ambao alikutana nao Jumamosi 20 Mei 2023. “Nilikutana nao jana na kofia nyekundu, huko, huko katika uwanja wa Mtakatifu Marta: mmefanya vizuri”, amewapongeza. Akiendelea amewataja vikundi vya parokia ya Molise, Scandicci, Grotte na Grumo Nevano; vyama vinavyojitolea kulinda maisha ya binadamu; kwaya ya Vijana ya ‘Emil Komel’ ya Gorizia; shule za “Caterina wa Mtakatifu Rosa” na Mtakatifu 'Orsola huko Roma na watoto wa  Mama msafi wa Moyo. Kwa kuhitimiksha amewatakia Dominika njema na ameomba wasisahau kumwombea.

Tafakari ya Siku ya Kupaa kwa Bwana na wito wa Papa kwa Sudan na Ukraine
21 May 2023, 13:00