Tafuta

2023.05.21 Kitabu "Il miracolo della vita" Muujiza wa Maisha na utangulizi wa Papa  Francisko. 2023.05.21 Kitabu "Il miracolo della vita" Muujiza wa Maisha na utangulizi wa Papa Francisko. 

Papa Francisko:tusikilize sauti ya mtoto ambaye hajazaliwa kupitia sayansi

Baba Mtakatifu ametia saini katika utangulizi wa kitabu 'Muujiza wa maisha'(Piemme) kilichohaririwa na Arnoldo Mosca Mondadori pamoja na mwanasayansi Gabriele Semperbon na mwandishi Luca Crippa,kwa nia ya kujadili zaidi ya uzio wa kiitikadi.Maandishi hayo yalitolewa ndondoo na gazeti la‘Corriere della Sera’

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Katika utangulizi wa kitabu kilichotiwa saini na Baba Mtakatifu  Francisko, chenye kichwa cha habari ‘Muujiza wa maisha’ na ambapo kilihaririwa na Arnoldo Mosca Mondadori pamoja na mwanasayansi Gabriele Semperbon na mwandishi Luca Crippa, kwa nia ya kujadili zaidi ya uzio wa kiitikadi, ndondoo zake zilitolea na Gazeti la kila siku jioni liitwalo ‘Corriere della Sera.’ Katika utangulizi huo Baba Mtakatifu anaandika kuwa Kitabu hiki kinalenga kumrejesha msomaji kwenye mshangao na furaha ya kuja katika ulimwengu wa kila mmoja wetu. Inapendekeza uzuri wa kuangalia maisha machanga kama mwenye haki ya juu ambayo kila mtu anayo: ile iliyopo ya Uzuri, na ndiyo kwa sababu tamasha la asili linalofuata mkondo wake huamsha mshangao na kuomba utunzaji, ulinzi na kukubalika.

Na zaidi ya yote  katika kiini cha  mada ya kitabu hicho Baba Mtakatifu anaandika kuwa “ nimealika ulimwengu kutekeleza tafakari ya utungaji  mimba sio tu kutoka kwa yaliyomo kwenye mila moja au nyingine ya imani au mawazo, lakini pia na mchango uliohitimu wa sayansi. Ni wito thabiti lakini tulivu wa kuchochea majadiliano na ndugu zangu, ambao ninashiriki nao ubinadamu wetu mkubwa, adhimu na wenye sura nyingi.” Baba Mtakatifu anabainisha kwamba “umuhimu wa kitabu hiki ni mchango wa mwanasayansi, mtaalam wa mambo ya utungaji mimba (embryology) na kushiriki kikamilifu katika kamati za pamoja za bioethics (yaani, katika mazungumzo na madaktari na wanasayansi walei). Pamoja na waandishi wengine alikubali mwaliko wangu: kurejea kuzungumza juu ya mada ya utoaji mimba ‘kusikiliza’ sauti ya kiinitete, kijihoji juu ya asili yake, umoja wake, jinsi inavyoshughulika nayo, ikiongozwa na michakato ya asili na imeendelea katika milenia ya mageuzi, kila tishio ambalo linasimama kati yake na kuwepo kwake mwenyewe.”

Kwa hiyo Baba Mtakatifu anatoa mwaliko na kupendekeza waandishi katika utangulizi huo kwamba “Ebu turudi kushangaa kuzaliwa”. Katika suala hilo, ninarudia tena wito wangu kwa wale wote ambao, wanakabiliwa na maisha ambayo hawajazaliwa, wasiache na wasikate tamaa juu ya suluhisho la kushangaza na la uhakika, kama vile kutoa mimba, lakini wanaona kuwa wanaweza kumpa mtoto ambaye hajazaliwa na mama msaada wa jamii ambayo hatimaye imejitolea kutetea utu wa wote, kuanzia na wale walionyimwa zaidi ulinzi”.

Akiendelea na hilo Baba Mtakatifu anakazia kusema kwamba “Kwa kifupi, jamii inayokataa  na iliyogubikwa na utamaduni wa kutupa katika kila nyanja na katika kila hatua ya uwepo: katika udhaifu wa mtoto ambaye hajazaliwa, katika upweke wa wazee, katika taabu ya aibu ya watu wengi maskini ambao wamenyimwa mambo muhimu na ukosefu wa matarajio ya maendeleo, katika mateso ya wale ambao ni waathiriwa wa vita, uhamiaji wa kukata tamaa, mateso katika kila sehemu ya dunia. Kwa jina la wahanga wengi wasio na hatia, Mungu awabariki wale wote wanaokubali kujadili na kutafakari kwa pamoja juu ya muujiza huu ambao ni maisha”.

22 May 2023, 17:05