Tafuta

2023.05.22 Wanahitaja wa Familia ya Miito ya Kimungu wamekutana na Papa Francisko. 2023.05.22 Wanahitaja wa Familia ya Miito ya Kimungu wamekutana na Papa Francisko.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa Francisko:panda,andaa,kuza na sindikiza miito

Kuna hitaji kubwa leo hii la utunzaji wa miito.Amesema hayo Papa alipokutana na washiriki wa hija ya Familia ya Shirika la Miito ya Kimungu,mmoja baada ya kutangazwa Mtakatifu Justin Maria Russolillo,mtume wa miito na mwanzilishi wa Shirika hilo la Miito.“Tunzeni miito,pandeni,andaeni na kufanya kukua,pamoja na kuwasindikiza”ameaalika Papa.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Jumatatu tarehe 22 Mei 2023, Baba Mtakatifu Papa Fracisko akikutana na Jumuiya ya Shirika la Miito ya Kimungu(S.D.V., ambayo pia inajulikana kama Vocationists, ambalo lilianzishwa nchini Italia mnamo tarehe 18 Oktoba 1920, amewashukuru kwa ujio wao na kuonesha furaha kuwakaribisha mwaka mmoja baada ya kutangazwa kwa  Mtakatifu Justin Maria Russolillo, mtume wa miito na mwanzilishi wa Shirika la Familia yao ya Waalimu wa Miito. “Kwetu sisi, kusherehekea kumbukumbu ya miaka kama hii haimaanishi tu kukumbuka kwa shukrani zawadi za Mungu na safari iliyokamilishwa, lakini pia kujiuliza ni nini tunapaswa kujiuliza, ni mwanga gani tunaweza kupokea kwa sasa na ni urithi gani tunaitwa kukubali kwa siku zijazo, kutoka katika ushuhuda wa Mtakatifu Justin. Kwa maneno mengine: ni ujumbe gani anatuachia ili kufanya kwa upya ufuasi wetu wa Bwana. Na kila mmoja wetu lazima ajiulize swali hilo ndani na kujiuliza hivy,” amesisitiza Papa.

Papa Francisko alikutana na Familia ya Shirika la Miito  ya kimungu
Papa Francisko alikutana na Familia ya Shirika la Miito ya kimungu

Baba Mtakatifu akinuu katika maandishi ya mwanzilishi wao amesema kwamba “wito wao ni kutoa huduma kwa  ajili ya miito yote. Karama hiyo inatokana na shauku ya kijana Giustin ambaye, akiwa bado mseminari,  badala ya kusoma alifanya mambo hayo, yaani akiwa bado ni mseminari alihisi msukumo mkubwa moyoni mwake wa kutunza miito, hasa ile ya ukasisi, ya wakfu na maisha  ya watawa. Papa kwa kuongeza: “Kuna haja kubwa ya hii hata leo ya kutunza miito. Na ninawaomba, tafadhali: tunzeni miito. Pandeni, itayarisheni na muwafanye wakue na kuwasindikiza.” Na jinsi ya kufanya? Baba Mtakatifu ameuliza. Kwa kutazam Mtakatifu Giustin, amependa  kuwaonesha “njia tatu ambazo ni sala, tangazo, utume” na kusizafafanua.

Familia ya Shirika la  Miito Mitakatifu
Familia ya Shirika la Miito Mitakatifu

Kwanza, sala.  Kila mtu ajibu mwenyewe ndani, kwa swali hili ambalo ninaliuza ... si kwa sauti, lakini ndani ya moyo: je, ninaombea miito? Au ninasema tu Baba Yetu au Salamu Maria, kwa kukimbia kidogo… Je, ninaleta maombi mazito kwa ajili ya miito? Maombi ni mzizi wa shughuli zetu zote na utume wote. Ukuu si wa kazi zetu, wa miundo yetu na wa mashirika yetu, lakini wa maombi. Ni ukuu. Na kwa sababu hiyo ndio maana ya  swali la kwanza: je, ninaombea miito? Kwa sababu tunapoingia katika roho ya kutafakari na kuabudu, Bwana hutubadilisha na tunaweza kuwa kielelezo cha upendo wa Baba kwa wale tunaokutana nao njiani, kuwa watu wapya, waangavu, wa kukaribisha na wenye furaha.”

Tunapokuwa hivyo, tunatoa huduma ya kwanza kwa miito, kwa sababu wale tunaokutana nao, hasa vijana, wanavutiwa na namna yetu ya maisha na chaguo la maisha tulilofanya: tunaweza kuona nuru ya Mungu ikiakisiwa juu ya nyuso zetu, huruma yake na upendo wake katika ishara zetu, furaha yake katika mioyo ya wale ambao wamejitoa na kujitoa kabisa kwake,  kwa kuhani au mtawa fulani anayeonesha ubinadamu mzuri, amani ya moyo, furaha isiyoshindika, hulka ya upendo na ukaribishaji. Na ni maombi ambayo yanatufanya kuwa hivyo.  Kwa hiyo papa amekazia kusema “Tusipuuze! Ombea miito kwa bidii”.

Familia kubwa ya Jumuiya ya Miito kimungu na Papa Francisko
Familia kubwa ya Jumuiya ya Miito kimungu na Papa Francisko

Katika utume wao basi, umuhimu wa kutangaza haupaswi kusahaulika. Mtangazeni Bwana. Mtakatifu Justin alizungumza juu ya wajibu wa mahubiri ya kila siku na utafiti wa daima na utamaduni wa miito (Kanuni na Katiba, I, 75, art. 802), hasa kupendekeza mafundisho ya katekisimu. Ni ishara inayohifadhi umuhimu wake na kuifanya uzuri wao kuwa wa mada. Katika muktadha wa kiutamaduni wa leo hii, kiukweli, Papa amekazia kusema wakati hisia ya uwepo wa Mungu inatoweka na imani inadhoofika, inaweza kutokea kwamba watu, hasa vijana, wanashindwa kuelewa maana na mwelekeo wa maisha yao, na labda kuridhika kuishi kutoka kwao. siku hadi siku, au kupanga bila kuhoji njia yao ni ipi, Bwana ana ndoto gani kwa ajili yao. Na ndipo tunaona haja ya kurudi kwenye uinjilishaji: kutangaza Neno, kuwasilisha yaliyomo ndani ya imani kwa njia rahisi na ya shauku, na kuandamana na watu katika utambuzi wao. Kuna haja ya hili katika Kanisa: kwamba nguvu za utume wetu zielekezwe zaidi ya yote kukutana na kusikiliza, kusindikiza katika utambuzi. Ninapendekeza hili kwenu: mfikie kila mtu kwa furaha ya Injili, wasaidie watu katika utambuzi wao wa kiroho, wajitumie wenyewe katika uinjilishaji!

Baba Mtakatifu kwa hiyo ameakumbusha kuwa daima wasitawishe  na kufanya upya roho ya umisionari. Mtaalamu wa wito, anasema Mtakatifu Justin, ni mtume, ni mmisionari, ni shahidi wa Injili, na Shirika lote la Miito ya Kimungu lazima liwe la kimisionari mashuhuri”.  Ni suala la kuweka katika mzunguko, katika maisha ya Kanisa lakini pia katika maeneo mbalimbali ya jamii ambayo wanafanya kazi, yote ambayo yanafaa kwa kuwasilisha furaha ya Injili, kwa mazungumzo na vijana, kwa kuonesha ukaribu kwa familia, kwa wanadamu, hasa zile zinazofanyika katika uwanja wa elimu. Huu ni utume ambao huduma ya walei wengi wanaoshiriki karama ya Mtakatifu Justin ni ya lazima na ya thamani.

Kila mmoja anataka amguse Papa
Kila mmoja anataka amguse Papa

Pamoja na hayo yote, Papa amependa kuongezea nyingine kwamba “Justin alipendekeza kwamba kila jumuia ya wafundi stadi wanapaswa kuwa majira ya kidini; nyumba ya makasisi; karamu kuu ya  miito; ofisi ya watu; zahanati ya mwanga na faraja; moyo wa parokia na jumuiya ya kijimbo.” Pia kwa njia hii utume unafanywa mbele: kuwa na uwezo wa kukaribisha, kusikiliza, ukaribu. Papa Francisko amewatakia kila wakati kuwa nafasi wazi ya kukaribisha watu na kutunza miito; kuwa na mahali pa sala na utambuzi kwa wale wanaotafuta; mahali pa faraja kwa waliojeruhiwa; kwa mananie mengine  kuwa “Karakana ya Roho” ambapo yeyote anayeingia anaweza kupata uzoefu wa kutengenezwa na fundi wa kimungu ambaye ni Roho Mtakatifu. “Na msivunjika moyo katika shida na misuko suko: Bwana yuko karibu nanyi na Mtakatifu Justin anawaombea!  Na kwa ujasiri nendeni mbele”. Papa amewabariki na kuwaomba wawombee.

22 May 2023, 16:11