Tafuta

2023.05.24 Katekesi ya Papa 2023.05.24 Katekesi ya Papa  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Fransisko:bidii ya kitume ni ujasiri wa mtu kuinuka anapoanguka!

Katika Katekesi ya Baba Mtakatifu ameendeleza mzunguko wa bidii ya kitume,mbapo ametoa mfano kwa waamini wa Mtakatifu Andrew Kim Tae-gon, mfiadini na padre wa kwanza wa Korea:ushuhuda wa Injili unaotolewa wakati wa mateso unaweza kuzaa matunda mengi kwa ajili ya imani.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 24 Mei 2023, katika katekesi yake kwa waamini na mahujaji waliofika katika uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican amesema kuwa “katika mzunguko huu wa katekesi tutakao kuwa nao, tujikita katika shule ya baadhi ya watakatifu wa kiume na wa kike ambao, kama mashahidi wa mfano, wanatufundisha bidii ya kitume. Kwa kuongeza amekazia “Kumbuka kwamba tunazungumza juu ya bidii ya kitume, ambayo lazima tuwe nayo kutangaza Injili”. Mfano mzuri wa Mtakatifu wa shauku ya uinjilishaji leo hii tunakwenda kumpata katika nchi ya mbali sana au katika Kanisa la Korea. Tunamtazama mfiadini na Padre wa kwanza wa Korea Mtakatifu Andrew Kim Tae-gon. “Lakini, je kwa Padrewa kwanza wa Kikorea: mnajua nini? Ni kwamba uinjilishaji wa Korea ulifanywa na walei! Ilikuwa ni walei waliobatizwa ambao walipitisha imani, hapakuwa na makuhani, kwa sababu hawakuwa nao. Kisha, baadaye ... lakini uinjilishaji wa kwanza ulifanywa na walei. Je, tungeweza kufanya jambo kama hilo? Hebu tufikirie kuhusu hilo kwani, ni jambo la kuvutia. Na huyu ni mmoja wa makuhani wa kwanza, Mtakatifu Andrew.”, Papa amekazia.  Maisha yake yalikuwa na yanabaki kuwa ushuhuda fasaha wa utangazaji wa Injili, bidii kwa ajili yake.

Baba Mtakatifu Francisko ameeleza kuwa takriban miaka 200 iliyopita, nchi ya Korea ilikuwa eneo la mateso makali sana: Wakristo waliteswa na kuangamizwa. Kumwamini Yesu Kristo, katika Korea wakati huo, kulimaanisha kuwa tayari kutoa ushahidi hadi kifo. Hasa, tunaweza kupata mfano wa Mtakatifu Andrew Kim kutoka katika nyanja mbili halisi za maisha yake. Ya kwanza ni njia ambayo alipaswa kuitumia kukutana na waamini. Kwa kuzingatia mazingira ya kutisha sana, Mtakatifu alilazimika kuwaendea Wakristo kwa njia isiyo ya dhahiri, na daima mbele ya watu wengine, kana kwamba walikuwa wamezungumza kwa muda fulani. Halafu, ili kutambua kitambulisho cha Mkristo cha mpatanishi wake, Mtakatifu Andrew alitumia njia hizi: kwanza kabisa, kulikuwa na ishara iliyokubaliwa hapo awali ya kutambuliwa: “utakutana na Mkristo huyu na atakuwa na ishara kama hii katika tabia yake au katika mkono; baada ya hapo, aliuliza swali kwa siri,  lakini kwa kunong'ona, kila kitu: “Je, wewe ni mfuasi wa Yesu?” Watu wengine walipohudhuria mazungumzo, Mtakatifu ilimbidi azungumze kwa sauti ya chini, akitamka maneno machache tu, yale muhimu zaidi. Kwa hiyo, kwa  upande wa Andrea Kim, usemi ambao ulifanya muhtasari wa utambulisho wote wa Mkristo ulikuwa “mwanafunzi wa Kristo”: “Je! wewe ni mfuasi wa Kristo?”, lakini kwa sauti ya chini kwa sababu ilikuwa hatari. Ilikuwa ni marufuku kuwa Mkristo huko.”, Papa amebainisha.

Kwa hakika, kuwa mfuasi wa Bwana maana yake ni kumfuata yeye, kufuata njia yake. Na Mkristo kwa asili ni mtu anayehubiri na kumshuhudia Yesu. Kila jumuiya ya Kikristo inapokea utambulisho huu kutoka katika Roho Mtakatifu, na Kanisa lote pia hupokea utambulisho huu kutoka kwa Roho Mtakatifu, ya siku ya Pentekoste (Ad Gentes,2). Na kutoka katika Roho hii tunayopokea shauku huzaliwa, shauku ya uinjilishaji, ari hii kuu ya kitume: ni zawadi ya Roho ambayo kila mtu anapewa. Na hata ikiwa muktadha unaozunguka sio mzuri, kama ule wa Andrea Kim huko Korea, haubadilika, badala yake, unapata dhamana kubwa zaidi. Mtakatifu Andrew Kim na waamini wengine wa Korea wameonesha kwamba, ushuhuda wa Injili unaotolewa wakati wa mateso unaweza kuzaa matunda mengi kwa imani. Papa ameongeza mfano wa pili halisi kwamba Mtakatifu Andrea alipokuwa bado mseminari, alilazimika kutafuta njia ya kuwakaribisha kwa siri wamisionari kutoka nje ya nchi. Hii haikuwa kazi rahisi, kwani serikali ya wakati huo ilikataza kabisa wageni wote kuingia katika eneo hilo. “Kwa sababu hii kabla ya hili ilikuwa ni vigumu sana kupata padre ambaye angekwenda kufanya utume: walei walifanya utume”.  Papa amewaomba waamini na mahujaji wafikirie kile ambacho Mtakatifu Andrea alifanya, siku moja alikuwa akitembea kwenye theluji, bila kula, kwa muda mrefu na kwamba akaanguka chini amechoka, akihatarisha kupoteza fahamu na kubaki amegandamana huko. Wakati huo, ghafla alisikia sauti ikisema: “Simama, tembea!” Kwa kusikia sauti hiyo, Andrea aliamka, akaona kama  kivuli cha mtu ambaye alikuwa akimuongoza.

Katekesi ya Papa 24 Mei

Uzoefu huu wa ushuhuda mkuu wa Kikorea unatufanya kuelewa kipengele muhimu sana cha bidii ya kitume. Yaani ujasiri wa kuinuka unapoanguka. Baba Mtakatifu ameuliza:  “Lakini je, watakatifu huanguka? Jibu, Ndiyo! Lakini tangu nyakati za kwanza kwa mfano  fikiria Mtakatifu Petro, alifanya  dhambi kubwa  Lakini alitiwa nguvu katika huruma za Mungu na akasimama tena. Na huko Mtakatifu Andrea tunaona nguvu hiyo, kwamba  alikuwa ameanguka kimwili lakini alikuwa na nguvu za kwenda, kupeleka ujumbe mbele”. Ingawa hali inaweza kuwa ngumu kiasi gani, Baba Mtakatifu amesisitiza kwa hakika

nyakati fulani inapoonekana kuwa haitoi nafasi kwa ujumbe wa kiinjili, hatupaswi kukata tamaa na tusikate tamaa katika kuendeleza kile ambacho ni muhimu katika maisha yetu ya Kikristo, huo ni uinjilishaji. “Hii ndiyo njia. Na kila mmoja wetu anaweza kufikiria: Je ninawezaje kuinjilisha?”  Papa ameomba kutazama hayo makubwa kufikiri katika walio wadogo, kufikiria udogo wetu: kuinjilisha familia, kuinjilisha marafiki, kuzungumza juu ya Yesu na kuinjilisha kwa moyo uliojaa furaha, uliojaa nguvu. Na hii inatolewa na Roho Mtakatifu. Tujiandae kumpokea Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste inayokuja na kumwomba neema hiyo, neema ya ujasiri wa kitume, neema ya kuinjilisha, kuendeleza daima ujumbe wa Yesu, amehimisha Papa.

Baada ya katekesi
24 May 2023, 16:41