Yaliyojiri katika siku ya II ya ziara ya Papa nchini Hungaria
Papa Francisko akiwa huko Budapest nchini Hungaria, siku yake ya pili iliyoanza 28 Aprili imehitimishwa, mara baada ya kuwa na siku iliyokuwa na ratibia kuanzia na kukutana: kwa faragha na Watoto wa Tasisi ya Mwenyeheri László Batthyány-Strattmann saa 2.45 hivi, ambayo inawatunza watoto walemavu na pia vipofu. Baadaye alikutana na maskini, wahamiaji na wakimbizi katika Kanisa la Mtakatifu Elizabeth wa Hungaria. Mara baada ya kusikiliza shuhuda kadhaa alitoa hotuba yake ikiwa ni ya Tatu tangu amefika katika Ziara yake ya kitume huko Budapest, kwa kuonesha furaha ya kuwa katikati yao na kushukuru, maneno ya makaribisho na shukrani ambapo imekumbusha huduma ya ukarimu ambayo Kanisa la Hungaria linatekeleza kwa ajili ya maskini.
Ratiba yake kama ilivyokuwa imepangwa, mara tu baada ya kukutana na maskini katika Kanisa la Mtakatifu Elizabeth wa Hungaria, alitembelea pia Jumuiya ya Kigiriki - katoliki “ La Ulinzi wa Mama Maria". Katika fursa hiyo baada ya masomo yaliyo somwa, walisali kwa pamoja na kuwabariki. Papa vile vile alikutana na Hilarion Mhusika wa zamani wa mahusiano ya Upatriaki, Moscow kwa miaka 13 na ambaye kwa sasa amekuwa mkuu wa kiorthodox, tangu mwaka 2022 Budapest na Hungaria. Mkutano kwa sauti ya upole ulifanyika katika Ubalozi wa Vatican kwa dakika 20 hivi. Papa alimkaribisha kwa kumkumbatia na kubusu msalaba kifuani. Hilarion alimzawadia vitabu vikubwa Papa.
Hata hivyo katika ratiba kulikuwa na mapumziko hadi alasiri ambapo Baba Mtakatifu alikwenda katika uwanja mkubwa zaidi wa michezo “Papp László Budapest, ndani mji mkuu wa nchi na kukutana na vijana. Baada ya ngoma ya utamaduni na shuhuda Papa alitoa hotuba ya kusisimua kwa vijana. Na hatimaye kama ratiba ilivyokuwa imepangwa, alikutana kwa faragha na Jumuiya ya Shirika la Kijesuit(JI).
Ikumbukwe Baba Mtakatifu Francisko anatarajia kurudi jioni Dominika tarehe 30 Aprili 2023, bada ya kukaa kwa siku tatu za kina katika nchi hiyo katika moyo wa Ulaya.