Papa:Ziara ya kwenda Hungaria 28-30 Aprili
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Mara baada ya Tafakari na sala ya Malkia wa Mbingu, kwa waamini na mahujaji wengi waliofika katika uwanja wa Mtakatifu Petro, mjini Vatican, Dominika tarehe 23 Aprili 2023, Baba Mtakatifu ameanza kusema kwamba: “Jana, mjini Paris, Enrico Planchat, Padre wa Shirika la Mtakatifu Vincent de Pauli, Ladislao Radigue na mapadre wenzake watatu wa Shirika la Mioyo Mitakatifu ya Yesu na Maria walitangazwa kuwa wenyeheri,.Wachungaji waliohuishwa na ari ya kitume, walishiriki ushuhuda wa imani hadi kifo cha kishahidi, ambacho waliteseka huko Paris mnamo 1871, wakati wa kile kiitwacho “Wilaya ya Kiparis”. Kwa kumalizia amesema “ tuwapigie makofi wenyeheri wapya”....
Siku ya Kimataifa ya Mama Sayari dunia 2023
Baba Mtatifu vile vile amesema: “Jana ilikuwa Siku ya kimataifa ya Mama Sayari dunia. Nimatumaini yangu kwamba dhamira ya kutunza kazi ya uumbaji daima itaunganishwa na mshikamano mzuri na maskini zaidi.”
Wito kwa ajili ya kuombea Sudan
Papa Francisko akiendelea amesema: “Kwa bahati mbaya, hali nchini Sudan bado ni mbaya, kwa hivyo ninarudia wito wangu kwa ajili ya kukomesha ghasia haraka iwezekanavyo na njia ya mazungumzo ianzishwe tena. Ninawaalika kila mtu kuwaombea kaka na dada zetu wa Sudan.”
Siku ya Chuo Kikuu Katoliki cha Moyo Mtakatifu
Katika fursa ya chuo kikuu katoliki Italia, Papa Francisko vile vile amesema: “Leo ni Siku ya 99 ya Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Moyo Mtakatifu, kwa kuongoza na kaulimbiu ya “Kupenda maarifa. Changamoto za ubinadamu mpya”. Ninawatakia Chuo kikuu kikubwa zaidi cha Kikatoliki cha Italia kikabiliane na changamoto hizo kwa moyo wa waanzilishi, hasa kijana Armida Barelli, aliyetangazwa kuwa Mwenyeheri mwaka mmoja uliopita”.
Ziara ya Budapest Hungaria
Ijumaa ijayo nitasafiri kwa siku tatu hadi Budapest, Hungaria, nikikamilisha safari niliyofanya mnamo 2021 katika Kongamano la Kimataifa la Ekaristi. Itakuwa fursa ya kulikumbatia tena Kanisa na watu wapendwa sana. Pia itakuwa ni safari ya kuelekea katikati mwa Ulaya, ambapo pepo za barafu za vita zinaendelea kuvuma, huku mienendo ya watu wengi ikiweka masuala ya dharura ya kibinadamu kwenye ajenda. Lakini sasa ninapenda kuzungumza nanyi kwa upendo, ndugu wa Hungaria, nikitazamia kuwatembelea ninyi kama mhujaji, rafiki na ndugu wa wote, na kukutana, miongoni mwa wengine, Mamlaka zenu, Maaskofu, mapadre na watu waliowekwa wakfu, vijana, wanafunzi wa vyuo vikuu na maskini. Ninajua kwamba mnatayarisha ujio wangu kwa juhudi nyingi: Ninawashukuru kutoka moyo wangu kwa hilo. Na ninaomba kila mtu anisindikize katika maombi ya safari hii”.
Sala kwa ajili ya Ukraine
Kama kawaida Baba Mtakatifu “Na tusiwasahau kaka na dada zetu wa Ukraie, ambao bado wanateswa na vita hivi”.
Salamu kwa mahujaji
Hatimaye aeelekza salamu kwa wote warumi na mahujaji kutoka Italia na kutoka nchi nyingi ambao aliona bendera nyingi kutoka nchi nyingi hasa zile za Salamanca na wanafunzi wa Albacete na vile vile kikundi cha Veneto-Trentino, Kikosi cha Msaada cha Malta. Amewasalimu waamini kutoka Ferrara, Palermo na Grumello ya Monte; jumuiya ya Shule ya Jimo la Lodi; vijana kutoka miji mbalimbali ya majimbo ya Alba, Bergamo, Brescia, Como na Milano; Vijana wa Kipaimara kutoka parokia nyingi za Italia; wanafunzi wa Taasisi ya Moyo Mtakatifu ya Cadoneghe; ushirika wa "Volœntieri" wa Casoli na kikundi cha Waendesha pikipiki cha Agna. Amewatakia mlo mwema na kuwaomba wasisahau kusali kwa ajili yake.