Tafuta

2023.04.15 Papa alikutana na wajumbe wa Chama cha (Fundacio'n Madre de la Esperanza de Talavera de la Reina) wa Toledo Hispania. 2023.04.15 Papa alikutana na wajumbe wa Chama cha (Fundacio'n Madre de la Esperanza de Talavera de la Reina) wa Toledo Hispania.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa:Tuwe na unyenyekevu kwani peke yetu hatuwezi kufanya lolote

Fransisko amekutana na wanachama wa Shirika la Kihispania “Madre de la Esperanza de Talavera de la Reina”ambalo linasaidia watu wenye ulemavu wa akili.Katika hotuba yake:“Msaidiane kwa unyenyekevu wa kutambua kwa sababu peke yetu hatuwezi.Na katika udogo wetu sisi ni wamisionari wa upendo.Mpeleke Yesu kwa wengine,kwa ishara,nyimbo na maombi.hata kama humtambui.”

Na Angella Rwezaula,- Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi tarehe 15 Aprili 2023, amekutana mjini Vatican na wanachama wa Shirika la Kihispania liitwalo “Madre de la Esperanza de Talavera de la Reina” ambalo linasaidia watu wenye ulemavu wa akili kutoka Toledo nchini Hispania. Amefurahi uwepo wao mjini Vatican ili kushirikishana nao siku kuu ya kufufuka Bwana. Siku kuu ambayo imerefushwa na hata sasa inadhimishwa katika mkesha wa Dominika ya Huruma ya Mungu. Papa ameelezea jinsi ambavyo pia sababu nyingine ya kusheherekea miaka hamsini kwa ajili ya kuungana pamoja kufanya kazi na kukua pamoja. Hili ni jambo jema. Safari ya maisha iko hivyo kupitia msalaba ambayo wanapanga kila mwaka ili kumsindikiza Yesu wa Nazareti. Kwa upande mmoja inatakiwa kuandaa vitu vingi, kusikiliza, kujifunza, kufanya uzoefu na  hatimaye, kusaidiana, mara nyingi sana tukiwa na unyenyekevu wa kutambua kwamba hatuwezi kufanya hivyo peke yetu.

Papa alikutana na wajumbe wa chama cha Mama wa Matumaini kutoka Hispania
Papa alikutana na wajumbe wa chama cha Mama wa Matumaini kutoka Hispania   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Kisha tunapaswa kumwomba Bwana kwa ujasiri wa kwenda njiani, kubeba sura yake ili kila mtu aweze kuitafakari. Na hivyo unampelekea Yesu kwa wengine, hata kama hutambui, lakini kwa ishara zao, kwa nyimbo zao, kwa maombi yao. Je, wanaona jinsi inavyopendeza, katika udogo wao, kuwa mashahidi wa Yesu, wamisionari wa huruma yake? Baba Mtakatifu Francisko amesema kwamba katika maisha, kama katika hili kupitia msalaba, sote tuna kazi. Yesu anatutazama na kufurahia juhudi zetu na upendo ambao tunaweza kuupitisha. Baadhi yao alisema  ni wasanii, wanafanya kazi halisi za sanaa, ambazo zinauzwa. Kuwa na uwezo wa kujikimu ni muhimu, kwa sababu kila mfanyakazi anastahili mshahara, lakini papa anaamini kwamba faida ya kazi yao ni kubwa zaidi kwa wale wanaopokea vitu hivyo vidogo, labda kama zawadi, na kuona upendo wote ambao umewezeshwa kuweka katika kuzitengeneza.

Papa katikati ya wajumbe wa chama cha Mama wa matumaini kutoka Hispania
Papa katikati ya wajumbe wa chama cha Mama wa matumaini kutoka Hispania   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Kwa njia hiyo Papa ameshauri kwamba ingekuwa muhimu kama nini kwamba katika kazi ya kila mtu waweze kuona nia yote ya kujifunza, uvumilivu wa walimu wao katika kufundisha, kazi ya pamoja ambayo ina uwezo wa kuhakikisha kwamba uwezo tofauti wa kila mtu unakutana katika matokeo ya mwisho ambayo ni mali kwa kila mtu. Na upendo huu wote katika kitu kidogo sana .... Jambo hili linaonekana ajabu, alisisitiza Papa. Akiendelea Papa alisema  alivyoona picha ambayo katika njia ya Msalaba  wanatembea wakiwa wamembeba Yesu mfungwa. Katika picha hiyo Yesu amefungwa mikono yake na msalaba umepambwa kwa scapulara ndogo. Yesu alivaa hivyo ili kwamba  tutambue kuwa kaka na dada wengi walio karibu nasi hawajisikii kuwa na uwezo wa kufanya mambo kama wengine, na wanaamini kwamba mikono yao imefungwa. Lakini si kweli,pamoja na Yesu, tunaweza kufanya mambo mengi mazuri. Kwa njia hiyo Papa amesema wao ni mikono ya Yesu, wanapofanya kazi pamoja. Wao pia ni miguu yake, sauti yake, Moyo wake, wanapotaka kushiriki furaha ya kukutana naye na wengine. Kwa jinsi gani? Papa ameuliza.

Papa amekutana na wajumbe Toledo Hispania
Papa amekutana na wajumbe Toledo Hispania   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Kwa kutoa shukrani kwa Mungu kwa ajili ya wazazi wao, kwa ajili ya ndugu zao, kwa ajili ya walimu wao, kwa ajili ya makuhani wao, na kwa ajili ya watu wote wanaowapenda. Kwa hiyo Msalaba uliopambwa kwa rangi unatoa mwaliko wa ndoto ya ufufuko. Yesu alikuja ulimwenguni ili kutuonesha njia ya mbinguni, kutufungulia milango yake, na hii ndiyo furaha kuu tunayosherehekea katika ufufuko kwamba tuko huru kutenda mema, kutembea pamoja kuelekea lengo hili. Na msalaba wetu yaani, jitihada, uvumilivu, huleta kazi nzuri ya sanaa, iliyojaa rangi na matumaini, ambayo, inaangaza ndani ya mioyo yetu, inatupatia nguvu na inatuhimiza kwenda mbele. Mapendekezo yao yawe angalau kwa miaka hamsini ijayo ya kufanya kazi pamoja na kushukuru wakiwa wamejaa furaha, kwa sababu Yesu amewachagua kwa ajili ya utume mkubwa. Bwana Yesu anawabariki na Bikira Maria Mama wa Tumaini awalinde daima daima.

17 Aprili 2023, 10:22