Tafuta

Papa:tutembelee wamonaki wana nguvu ya sala isiyoonekana kusaidia Kanisa na utume wake

Papa katika katekesi yake ya mwendelezo wa ari ya ushuhuda wa kitume ameshauri kutembea monsteri za kitawa kwa sababu ya kuunganisha sala na kazi ya kila siku na kutoa mfano wa Mtakatifu Teresa wa Mtoto Yesu ambaye ni msimamizi wa utume wa kisimionari.Maisha yao ni moyo ambao ni kama antena wanajua kila kitu kinachotokea ulimwenguni

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko katika tafakari yake ya Katekesi, Jumatano tarehe 26 Aprili 2023 kwa waamini na mahujaji waliounganika katika uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, kwa mwendelezo mada ya ushuhuda wa ari ya Kitume, amesema walianzia na Mtakatifu Paulo ambao katekesi iliyopitia walitaazama ushahidi ambao unatangaza Yesu na maisha  hadi kujitoa kwa ajili yake na kwa ajili ya Injili. Lakini kuna ushuhuda mwingine mkubwa ambao unapitia historia ya imani, ule wa wamonaki wa kike na kiume, kaka na dada ambao watangaza na kujikatalia ulimwengu kwa ajili ya kumuiga Yesu katika njia ya umaskini, ya usafi wa moyo na uti ina kwa ajili ya kuwaombea wote.   Maisha yao yanajizungumza, lakini sisi tunaweza kujiuliza,Je inawzekanaje watu ambao wanaishi katika Monastri wanasaidia kutangaza Injili?

Papa amewabariki mama wajawazito
Papa amewabariki mama wajawazito

Je isingekuwa vema kujijita nguvu zao sote katika utume? Kwa kutoka ndani ya Monastri na kuhubiri nje, Injili… nje ya Monasteri? Ni swali la Papa ambapo amesema kwamba. Kiukweli, wamonaki ni moyo unaodunda kutoka tangazo. Ni ajabu hili kuwa moyo unaodunda. Sala zao   ni Oksijeno kwa ajili ya viungo vya Mwili wa Kristo, sala zao ni nguvu isioonekana ambayo inasaidia utume. Si kwa bahati mbaya msimamizi wa utume wa kimisionari  ni mmonaki, Mtakatifu Teresa wa Mtoto Yesu. Tsikilize  alivyogunda wito wake, na aliandika hivi: “ Nilielewa kwamba Kanisa lina moyo, moyo unaochomwa na upendo. Nilielewa kwamba upendo pekee ndio unaowasukuma washiriki wa Kanisa kutenda na kwamba, kama upendo huu ungezimwa, mitume hawangetangaza tena Injili, wafia imani hawangemwaga tena damu yao. Nilielewa na kujua kwamba upendo unakumbatia miito yote (....).Kisha kwa furaha kuu na msisimko wa nafsi nikalia: Ee Yesu, mpenzi wangu, hatimaye nimepata wito wangu. Wito wangu ni upendo. […] Katika moyo wa Kanisa, mama yangu, nitakuwa upendo” (Maandiko yake 8 Septemba,1896). Watawa wa ndani, wamonaki kike na kiume ni  watu wanaosali, wanaofanya kazi, kwa ukimya, kwa ajili ya Kanisa zima. Na huu ndio upendo: ni upendo unaooneshwa kwa kuombea Kanisa, kufanya kazi kwa ajili ya Kanisa, katika nyumba za watawa”, Papa Francisko ameongeza.

Papa akibariki wenye ndoa wapya
Papa akibariki wenye ndoa wapya

Upendo huo kwa wote huhuisha maisha ya watawa na kutafsiri katika maombi yao ya maombezi. Katika suala hili Baba Mtakatifu amependa  kutoa  kama mfano Mtakatifu Gregory wa Narek, Mwalimu wa Kanisa. Yeye ni mtawa wa Kiarmenia, aliyeishi karibu miaka ya  1000, ambaye alituachia kitabu cha maombi, ambamo imani ya watu wa Armenia, wa kwanza hukumbatia Ukristo, ilimiminwa; watu ambao, wakiwa wameshikamana na msalaba wa Kristo, wameteseka sana katika historia. Na Mtakatifu Gregory aliishi karibu maisha yake yote katika monasteri ya Narek. Huko alijifunza kuchunguza kwa kina cha nafsi ya mwanadamu na, akichanganya pamoja mashairi na sala, aliweka alama ya kilele cha fasihi ya Kiarmenia na kiroho. Kipengele cha kuvutia zaidi kwake ni mshikamano wa ulimwengu wote ambao yeye ni mkalimani. “Na miongoni mwa watawa wa kike na kiume kuna mshikamano wa kiulimwengu: chochote kinachotokea duniani, kinapata nafasi katika moyo mwao, na wanasali na kuomba. Moyo wa watawa wa kike na kiume  ni moyo ambao huchukua kama antena, huchukua kile kinachotokea ulimwenguni na kuomba na kuombea. Na hivyo wanaishi katika muungano na Bwana na watu wote”.

Kukutana na Papa na kumsalimia ni baraka
Kukutana na Papa na kumsalimia ni baraka

Na mmoja wao alisema “Nilijitwika kwa hiari yangu makosa yote, kuanzia yale ya baba wa kwanza hadi ya mwisho wa kizazi chake. “Na kama Yesu alivyofanya: wanajitwika matatizo ya ulimwengu, magumu, magonjwa, mambo mengi na wanayaombea. Na hawa ndio waeneza-injili wakuu. Monasteri ni hivyo …. lakini je ni kwa nini wanaishi wamefungwa na wanainjilisha? Ni kweli…kwa sababu kwa neno, mfano, maombezi na kazi ya kila siku, wao  ni daraja la maombezi kwa watu wote na dhambi. Pia wanalia kwa machozi, wanalia kwa ajili ya dhambi zao  na kisha  kwa ajili ya wote wenye dhambi na pia wanalia kwa ajili ya dhambi za ulimwengu, na wanaomba na kuomba kwa mikono na mioyo yao iliyoinuliwa juu.

Papa amekutana kwaya  ya watoto
Papa amekutana kwaya ya watoto

Kwa njia hiyo, Baba Mtakatifu Francisko ameshauri kufikira kidogo juu ya hilo amejiruhusu kusema neno la -"hifadhi" tuliyo nayo katika Kanisa: wao ni nguvu halisi, nguvu halisi inayowapeleka mbele watu wa Mungu na kutoka hapo inakuja tabia ambayo watu wanayo  watu wa Mungu. Kwa hiyo amesema watu wanaokutana na watu waliowakw wakfu, waombe ili wawaombee kwa sababu wanajua  kwamba kuna maombi ya maombezi yao . Aidha iyawafaa kwa kadiri wawezavyo kutembelea monasteri fulani, kwa sababu huko wanasali na kufanya kazi. Kila mtu ana kanuni yake mwenyewe, lakini kuna mikono yao daima ambayo ina fanya  kazi,  na maombi. Bwana atupe monasteri mpya, atupe watawa na watawa wanaopeleka Kanisa mbele kwa maombezi yao.

Katekesi ya Papa 26 Aprili 2023
26 April 2023, 17:44