Papa na Waoblati,Milano:Ushuhuda wa furaha ya kuwa ndugu!
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Ndugu wa Oblati wa Jimbo la Milano, Ijumaa tarehe 14 Aprili 2023. Katika Hotuba yake aliyowakabidhi Papa Francisko anawashukuru ujio wao na salamu kutoka kwa mkuu kwa niaba yako. Kwake yeye ni fursa kubwa kukutana na ndugu waliowekwa wakfu, kwa sababu ni ushuhuda wa thamani ya uwepo wa Kanisa na ambao unastahili kugunduliwa. Kwa njia hiyo amewashukuru na kuwatia moyo kwa sababu wao ni ishara ndogo lakini muhimu na inayohitajika, ni kama vipande vizuri vya mapambo ya miito ya Kanisa.
Kwanza kabisa, wao ni ishara ya udugu kulingana na Injili. Wao wako sawa kabisa na kuwa kwao ndugu: si kwa mambo wanayofanya, pamoja na shirika, shughuli... Mambo haya yote ni mazuri na yanahitajika, lakini udugu unajengwa kwa namna halisi ya maisha. Mtindo thabiti, ambayo kila mmoja wenu hupata uzoefu wa kawaida kwa njia tofauti, na utu wako mwenyewe na zawadi zako na pia mapungufu yako; lakini sifa ya kawaida na inayostahiki ni udugu huu. Papa anatumaini kwamba hii ni sababu ya furaha ya ndani kwao, kwa sababu ni njia yao ya kufanana na Yesu, ambaye aliishi mwelekeo huu wa kuwa ndugu kwa kila mtu, ndugu wa ulimwengu wote. Ni kipengele sahihi cha fumbo la Umwilisho. Hili ndilo jambo la kwanza ambalo ametaka kuwatakia “furaha ya kuwa ndugu”.
Wao ni ndugu wa Oblati na ndicho kipengele cha pili ambacho ni cha kujitoa sadaka, yaani karama binafsi katika huduma. Yesu, kutoka katika umbo la Mungu, alitwaa umbo la mtumishi; lakini wanapaswa kuwa waangalifu na sio moja ya ripoti hizo ambazo kila mtu anasema kwamba jinsi ilivyo nzuri! ripoti ya kupongezwa, na hiyo hufanya habari. Kinyume chake ni utumishi uliofichwa, mnyenyekevu, wakati mwingine hata wa kufedhehesha. Hiyo tunajua ndiyo njia ya kufuata kwa kila Mkristo. Lakini ambayo ni karama ya kwanza ambayo ni sadaka. Na hapa pia, kwa wale wanaoishi hivyo, Roho Mtakatifu huwapatia furaha ya ndani. Mama Teresa mara nyingi alizungumzia juu yake: furaha ya kutumikia. Maria alipokwenda kumsaidia Elizabeth, hakukuwa na wapiga picha waliokuwa wakimsubiri, hakukuwa na waandishi wa habari. Hakuna aliyejua. Na hapo ndipo furaha ilipo, kwamba Bwana pekee ndiye anayejua! Furaha ya huduma. Hii ni hamu yangu ya pili, Papa amesisitiza
Na ya jambo la mwisho Baba Mtakatifu amebainisha kwamba linahusishwa na ukweli kwamba wao ni wa jimbo. Ndugu wa Jimbo wa Oblati. Huu pia ni mwelekeo wa Umwilisho wa kuwa mwaminifu kwa nchi, kwa watu, kwa jimbo. Wakati mwingine tunatamani kuokoa ulimwengu! “Lakini Mungu anakuambia: uwe mwaminifu kwa huduma hiyo, kwa watu hao, kwa kazi hiyo... Yesu aliokoa ulimwengu kwa kutoa maisha yake kwa ajili ya kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli, na hivyo akatimiza uaminifu wa Baba; aliwapenda mpaka mwisho wale ambao Baba alimpa, alimwaga damu yake kwa ajili yao, na hivyo aliimwaga kwa ajili ya wote. Hii ndiyo sheria ya upendo: huwezi kupenda ubinadamu kwa uwazi, unampenda mtu huyo, watu hao. Uaminifu ni jambo adimu! Zaburi moja tayari ilisema hivi: “Uaminifu umepita kati ya wanadamu” (Zab 12:2). Huduma ya kijimbo ni shule ya uaminifu, na ndugu huo wanafanya kuwa hivyo, Udugu, obalati, wa kijimbo, Ni mpango wa maisha, Bwana awasindikize daima katika njia hi ina Mama awalinda katika furaha na katika imani”.