Papa kwa shirika la Ndege Italia:Ni mbawa za Papa!
Na Angella Rwezaula; – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko tarehe 14 Aprili 2023 amekutana mjini Vatican na wakuu na wafanyakazi wa Shirika la Ndege la Italia. Ameshukuru na kusema wametua Vatican. Ni furaha yake kuwapokea na kwa namba nyingine wao kama wawakilishi wa “mabawa ya Papa ambayo yamaruhusu kuruka hadi miisho ya dunia ili kupeleka Injili ya tumaini na amani. Papa amesema wakati mwingin anafikiri ikiwa Mtakatifu Paulo angepata uwezekano wa kusafiri kwa ndege, ni kitu gani kingetokea? Na kiukweli hayo yalitokea kwa Papa ambaye alikuwa anapeleka kwa niaba yake. Mnamo tarehe 4 Januari 1964 Mtakatifu Paulo VI alipanda ndege aina ya DC8 ya Italia, ile DC8 ambao wamestaafu sasa, kwa mara ya kwanza Papa wa historia alisafiri kwa ndege kwenda hija ya kitume. Papa Montini alikuwa anatamani sana kwenda Nchi Takatifu, fupi lakini ya kina, Alikuwa ameitangaza kwa shauku na ihisi za Mababa wa Mtaguso, mwishoni mwa sehemu ya pili ya Mtaguso. Ndege hiyo kwa kuanzia Fiumicino Roma na kufika Amani alizindua safari za kipapa katika ulimwengu, mtindo moya wa kutekeleza huduma yak e ya kichungaji ya Papa ambayo iliruhusu Askofu wa Roma kufikia watu wengine ambapo kuna wengine ambao hawana uwezo wa kutimiza hija hiyo Roma.
Baba Mtakatifu ameeleza kuwa, baada ya zafari ya kwanza, Mtakatifu Paulo VI alitimiza safari nyingine nane kwa kugusa mabara yote. Mtakatifu Yohane Paulo II aliyejitahidi kwa miaka 27 ya upapa wake alitimiza ziara 104 za kimataifa, katika mtindo huu wa utuma umegeuka kuwa sehemu fungamani ya upapa. Na hivyo alisafiri mfuasi wake Benedikito XVI; na hivyo pia ameendelea yeye Papa: ambapo majuma mawili Mungu akipenda, atasafiri kwa ziara yake ya 41 kwenye hija ya kutembelea nchini Hungaria. Baadaye kutakuwa na ile ya Marsiglia na baadaye Mongoria… mambo yote hayo yapo katika orodha ya kusubiri”, Papa amesisitiza. Shirika la “bendera ya Italia ambayo wao walikuwa wanawakilisha, Papa amesema kwa kawaida wanamsindikiza Mfuasi wa Petro na wasindikizaji wake katika safari ya kwanza na baadhi katika muktadha, wanafanya katika kurudi na kuzungukia ndani, au katika Nchi nyingine kwa muktasha wa safari hiyo hiyo. Ni huduma ya thamani sana, ambayo inahitaji umairi, utunzaji na umakini kwa walio wengi, ikiwa na magumu ya kuandaa ambayo sio rahisi; anajua vizuri Papa kwa sababu kama walivyoona yeye ana matatizo ya kutembea, lakini shukrani kwa msaada wao, anaendelea kusafiri. Kwa hiyo Papa amewapongeza.
Kwake yeye ni muhimu sana kukutana na watu,kukutana jumuiya , waamini na waamini wa dini nyingine, wanawake, na wanaume wenye mapenzi mema… Kukutana ana kwa ana, kuzungumza na mtu ni kitu tofauti ambacho kianeleza uwepo na ujumbe, labda kwa njia ya video. Siyo sawa... Kwa hiyo Papa amethibtisha kwamba anasafiri ili kuthibitisha imani ndugu, kuwa nao karibu na wale wanaoteseka, kwa ajili ya kuwasaidia wale ambao wanajikita katika muktaadah wa amani. Papa kwa hkuhitimisha amesema hiyo yote inawezekana hata kwa sababu ya wao. Ka njia hiyo amewashukuru na Mungu akipenda wanataendelea kupaana pamoja. Amewatakia kazi njema na kuwashukuru sana kwa ziara na Mama Maria anawasindikize. Amewabariki kwa moyo wote na familia zao. Tafadhali wasisahau kusalia kwa ajili yao.