Papa:jitafakari dhamiri kila siku&kumfungulia Yesu moyo
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Kabla ya sala ya Malkia wa Mbingu, Baba Mtakatifu Francisko kwa kuongozwa na Injili ya Dominika ya Tatu ya Pasaka kwa waamini na mahujaji wengi waliojaa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro tarehe 23 Aprili 2023 amesema kwamba “Katika Dominika ya tatu ya Pasaka, Injili inasimulia mkutano wa Yesu Mfufuka na mitume wa Emmau. (Lk 24,13-35). Hawa ni wafuasi wawili ambao walikata tamaa kwa sababu ya kifo cha Mwalimu na siku ya Pasaka wakaamua kuacha Yerusalemu na kurudi nyumbani. Labda walikuwa kidogo na shaka kwa sababu walisika wanawake waliotoka kwenye kaburi wakisema kwamba Bwana alikuwa hivi, na wakaenda. Na wakati wakitembea kwa huzuni huku wakizungumza kile kiichotokea, Yesu akawa karibu nao, lakini hawakutambua. Baadaye Yeye akawauliza kwa nini wana huzuni hivyo na wao wakamwambia: “Lakini je ni wewe tu ambaye ni mgeni Yerusalemu! Hujui kile ambacho kilitokea kwa siku hizi (Lk 24, 18). Yeye aliwajibu Ni nini? (Lk 24,19). Na walimsimulia historia yote.
Papa amesema kuwa baadaye wakati wakitembea aliwasaidia kusoma juu matukio kwa namna tofauti, yaani katika mwanga wa unabii na wa Neno la Mungu, kwa yale yote yaliyotangazwa kwa watu wa Usraeli. Suala la kusoma ni kile ambacho Yesu anawafanyia wao na anawasaidia kusoma. Baba Mtakatifu Francisko kwa njia hiyo akiwaelekea waamini ameomba kujikita na mantiki hiyo. Kwa upande wake amesema “Hata sisi kiukweli ni muhimu kusoma historia yetu pamoja na Yesu, Historia ya maisha yetu, kwa kipindi fulani, katika siku zetu, pamoja na kukata tamaa na matumaini.
Hata sisi inatokea, tunaweza kujikuta tunahangaika mbele ya matuko fulani, tukiwa peke yetu, na wenye mashaka, kuwa na maswali mengi na wasiwasi. Injili ya leo hii inatualika kusimulia yote kwa Yesu, kuwa wazi kabisa , bila kuogopa kumsumbua, bila woga wa kusema mambo yaliyokosewa, bila aibu ya ugumu wetu wa kuelewa. Bwana anafurahi tunapojifungulia kwake: ni kwa mtindo huo tu, anaweza kutushika mkono, kutusindikiza na kurudi kuwaka moyo (Lk 24,32). Kwa hiyo hata sisi, kama wafuasi wa Emmau, tunaalikwa kumsihi abaki na sisi, inapokuwa usiku, ili Yeye abaki na sisi (Lk 24,29).
Baba Mtakatifu amesema kuwa kuna namna nzuri ya kufanya hivyo ambayo amependekeza. Kwanza kabisa njia hiyo ni kutafuta muda kila jioni, kwa muda mfupi kufanya mazoefu ya kutathimini dhamiri: Je ni kitu gani kimetokea ndani mwangu leo hii? Hilo ni swali. Hiyo ni kusoma kila siku, siku na Yesu, kusoma siku yangu, kumfungulia moyo na kumpelekea Yesu mtu, chaguzi, hofu, maanguko, na matumaini, mambo yote ambayo yametokea, ili kwenda kwake kujifunza taratibu kutazama mambo kwa mtazamo tofauti, kwa mtazamo wake na sio wa kwetu. Tunaweza kufanya hivyo kwa kuishi uzoefu ule wa wanafunzi wawili.
Mbele ya upendo wa Mungu, hata kile ambacho utafikiri ni kigumu na kushindwa kinaweza kuonekana chini ya nuru nyingine: msalaba mgumu wa kukumbatia uchaguzi wa msamaha mbele kosa, kisasi kilichokosa, ugumu wa kazi, ukweli unaogharimu, majaribu ya maisha ya familia ambayo yanaweza kutufanya kuonekana chini ya nuru mpya, wa Msalaba Mfufuka, ambaye anajua kufanya kila anguko katika hatua ya mbele. Lakini ili kufanya hivyo ni muhimu kutoa nafasi: kuacha muda na nafasi kwa ajili ya Yesu na usimfiche kitu, mpelekee madhaifu, humiza ukweli wake na kuacha moyo utingishwe na pulizo la Neno lake.
Baba Mtakatifu amesisitiza kuwa, tunaweza kuanza hata leo hii, kwa kujikita na uzoefu huo, usiku na wakati wa sala kwa kujiuliza je! Siku yangu imekuwaje? Je ni furaha zipi, huzuni gani, uchovu gani na ilikuwa namna gani? Zilikuwa ni lulu gani za siku ambazo labda zimejificha, ambazo ninapaswa kuzishukuru? Je kumekuwa na upendo kwa kile ambacho nimefanya? Ni maanguko yapi, huzuni, mashaka na hofu vya kupeleka kwa Yesu ili anifungulie njia mpya, anipe faraja na kunitia moyo? Kwa kuhitimisha Papa amesema “Bikira Maria wa hekima atusaidie kujua Yesu ambaye anatembe pamoja nasi na kusoma neno, na kulirudia kusoma mbele yake kila siku ya maisha yetu”.