Tafuta

2023.04.15Wanahija kutoka Jimbo la Crema ( Italia ) 2023.04.15Wanahija kutoka Jimbo la Crema ( Italia )  (Vatican Media)

Papa Francisko:wito kwa ajili ya kuomba amani nchini Myanmar

Papa amekutana na mahujaji kutoka Jimbo kuu la Crema katika ukumbi wa Paulo VI. Katika hotuba yake ametoa mwaliko wa kuombea nchi ya Myanmar nchi aliyouawa shahidi Mwenyeheri Alfredo Cremonesi:“Alidhihirisha utauwa wake thabiti,kazi ya ukarimu,maisha rahisi na ari ya kimisionari,fadhila thabiti za nchi yake.”

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi tarehe 15 Aprili 2023, amekutana na washiriki wa hija ya Jimbo kuu la Crema Italia. Katika hotuba yake ameanza kumshukuru Askofu Daniele Gianotti kwa maneno ya hotuba yake lakini pia hata Askofu Rosolino Bianchetti, Askofu Quiché, nchini Guatemala, Mkuu wa Shirika la Taasisi ya Kipapa  kwa ajili ya Utume wa nje, waseminari, wa Jimbo  la Taungngu, nchini  Myanmar, mapadre, na wamisionari waliokuwapo,  pia Mkuu wa Wilaya ya Cremona na Mameya wa mji huo. Salamu zaidi kwa wote waliofika kwa idadi kubwa kama hiyo na kuwashukuru kwa mshangao kwa ziara yao.  Mkutano wao huo ulipangwa kitambo, baada ya kutangazwa Mwenyeheri Padre Alfredo Cremonesi, mzaliwa wa Cremona, na mmisionari na mfia imani yake huko Birmania, ambayo sasa ni Myanmar. Kama wanavyojua,  Papa Francisko amesema hiyo  ni nchi yenye matatizo ambayo amesisitiza kuwa anaibeba moyoni mwake na amewaalika kuiombea, wakimwomba Mungu zawadi ya amani. Kwa hiyo janga la Uviko lililazimisha kuahirisha mkutano wao  hadi siku. Hata hivyo, huu pia ni mwaka wa pekee: kiukweli, ni miezi hii ambayo inaadhimisha mwaka wa sabini wa kuuawa kwa Mwenyeheri Alfredo, ambayo ilifanyika mnamo tarehe 7 Februari 1953 huko Donoku.

Papa Francisko alikutana na wanahija kutoka Crema
Papa Francisko alikutana na wanahija kutoka Crema

Padre Cremonesi alifanya kazi katika kijiji hicho cha mlima kwa muda mrefu wa maisha yake, na alirudi huko mara kadhaa, licha ya shida na hatari elfu, alikuwa karibu na watu wake na kujenga kwa kupyaisha kile ambacho vita na vurugu viliendelea kuharibu. Mtu anavutiwa na ushupavu wa Padre Alfredo alioutumia utumishi wake, akijitoa bila hesabu na bila kujiwekea akiba kwa ajili ya manufaa ya watu aliokabidhiwa, waamini na wasioamini, Wakatoliki na wasio Wakatoliki. Mtu wa ulimwengu wote, kwa kila mtu. Hivyo kwa hakika alijumuisha, kwa namna ya kuwa mfano, fadhila dhabiti za eneo lake la Crema: uchaji Mungu thabiti, kazi ya ukarimu, maisha sahihi na ari ya kimisionari. Alipanda umoja, akijua jinsi ya kuzoea ulimwengu mpya kabisa kwake na kuufanya kuwa wake mwenyewe, kwa upendo. Alitumia upendo hasa kwa wahitaji, akajikuta mara kadhaa akiwa hana kitu, akilazimika kuomba mwenyewe. Alijishughulisha na elimu ya vijana na hakujiruhusu kutishwa au kukatishwa tamaa na kutoelewana na upinzani mkali, hadi mlipuko wa bunduki zilizomuua. Lakini hata ukatili huu uliokithiri haukuzuia roho yake na haukunyamazisha sauti yake.

Furaha ya wanahija kutoka Crema ya kukutana na Papa
Furaha ya wanahija kutoka Crema ya kukutana na Papa

Kwa hakika, Baba Mtakatifu amesisitiza kuwa aliendelea kusema kupitia kwa wale ambao wamefuata nyayo zake: miongoni mwa wamisionari hao ni  Padre Andrea Mandonico ambaye bado yupo japokuwa  hakuweza kuwa hapo pamoja nao, tusimsahau Padre Pierluigi Maccalli, mfungwa wa miaka miwili nchini Niger na Mali, ambaye waliomba sana  kwa ajili ya ukombozi wake! Sauti ya mmisionari ya Padre Alfredo, hata hivyo, haijakabidhiwa kwao tu: imekabidhiwa kwa wote,  na zaidi wao , kwa maneno yao na zaidi ya yote kwa uzoefu wao kama jumuiya ya Kikristo.

Baba Mtakatifu Francisko amebainisha kwamba katika maandishi yaliyoachwa na Padre Alfredo kuna sentensi nzuri sana juu ya roho ya umisionari. Yeye anasema hivi: “Sisi wamisionari si kitu kiukweli. Yetu ni kazi ya ajabu na ya ajabu sana ambayo inatolewa kwa mwanadamu, sio kuifanya, lakini kuiona: kuona roho zikiongoka ni muujiza mkuu zaidi kuliko muujiza wowote.”  Papa ameongeza kusema kwamba “Maneno haya yanafupisha baadhi ya sifa muhimu za umisionari”, ambazo Papa amewaalika kuzitafakari na ambazo amewaalia wao wenyewe kufanya uzoefu wa utambuzi wa unyenyekevu wa kuwa chombo kidogo katika mikono mikuu ya Mungu; furaha ya kufanya “kazi ya ajabu” kwa kuwaleta kaka na dada pamoja na Yesu; kushangazwa na yale ambayo Bwana mwenyewe hufanya kwa wale wanaokutana nao  na kumkaribisha. Unyenyekevu, furaha na mshangao: sifa tatu nzuri za utume wetu, katika kila hali na hali ya maisha.

Papa na wanahija wa Crema
Papa na wanahija wa Crema

Papa Francisko amesema kwamba kiukweli ni zawadi kuwa nao hapa: jumuiya ya rangi ya kila umri na hali. Kwa kufafanua na Mtakatifu Laurenti, shemasi na shahidi wa Kanisa la Roma, wanaweza kusema kwamba hii ndiyo hazina ya Kanisa: na wao wote  ni maskini wote mbele za Mungu na wote matajiri katika upendo wake usio na mwisho, ambayo inaakisiwa kwa njia ya pekee machoni pa kila mmoja, na ambayo sisi ni mashahidi na wamisionari wayo. Hii ndiyo sababu ninataka kukuhimiza uendelee na safari yako ya jumuiya kwa kujitolea na shauku, katika nyanja zake zote. Ninawasihi msitawishe ushirika, kati ya watu na kati ya jumuiya, katika kusaidiana, kwa ushirikiano, pia katika kufungua njia mpya, katika ulimwengu unaobadilika kwa kasi zaidi. Wasiogope kutafsiri maadili ya kale katika lugha za kisasa, ili waweze kufikia kila mtu, na ili kila mtu aweze kuonja na kufurahia manufaa yao. Wajaribu daima kuwa wakaribishaji na mjumuisho na wale wanaobisha mlangoni kwako; kutunza hasa elimu ya vijana, kuwasaidia kujitolea  bora zaidi wao wenyewe na kupata mpango wa Mungu katika maisha yao, na kuifanya utume, kwa shauku.

Kushangazwa na watu wengi wa hija kutoka Crema
Kushangazwa na watu wengi wa hija kutoka Crema

Papa amewahimiza wasisahau wazee, wanyonge, hasa maskini na wagonjwa; Amewaalika kuwasikiliza, kwa sababu kuna mengi ya kujifunza kutoka kwa wale wanaojua maisha, uchovu na mateso ni nini. Hatimaye, katika nchi tajiri na nzuri kama yao wawe vielelezo vya utunzaji wa heshima kwa viumbe, wa kiasi katika kutumia matunda yao na ukarimu katika kuwagawia wengine. Papa amewashukuru tena kufika kwao na amewakabidhi kwa maombezi ya Bikira Maria na Mtakatifu  Pantaleone. Amewabariki kwa moyo wote na jumuiya nzima ya kijimbo. Amewaomba wasisahau kusali kwa ajili yake.

17 April 2023, 09:35