Tafuta

Papa Francisko asikitishwa na shutuma dhidi ya Mtakatifu Yohane Paulo II ambaye kwa siku za hivi karibuni, amezushiwa shutuma nzito dhidi ya utu wake, heshima na utakatifu wake. Papa Francisko asikitishwa na shutuma dhidi ya Mtakatifu Yohane Paulo II ambaye kwa siku za hivi karibuni, amezushiwa shutuma nzito dhidi ya utu wake, heshima na utakatifu wake. 

Papa Francisko Asikitishwa na Shutuma Dhidi ya Mtakatifu Yohane Paulo II: Hazina Ukweli

Baba Mtakatifu Francisko asikitishwa na shutuma dhidi ya Mtakatifu Yohane Paulo II ambaye kwa siku za hivi karibuni, amezushiwa shutuma nzito dhidi ya utu wake, heshima na utakatifu wake, mambo ambayo hayana msingi wala ukweli wowote. Baba Mtakatifu anawataka waamini kuwa ni vyombo na mashuhuda wa Kristo Yesu na Kanisa lake, kwa njia ya imani tendaji iliyopyaishwa, ili kusaidia kunogesha mng’ao wa Kristo Yesu mfufuka ulimwenguni kote. Utu na Heshima!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Mtakatifu Adalbert wa Prague, Mfiadini, Mlinzi na Mwombezi wa Poland anajulikana sana katika Jamhuri ya watu wa  Czech, Poland na Slovakia. Alipozaliwa wazazi wake wakamwita Vojtěch. Alikuwa Askofu wa Jimbo la Prague na mmisionar hodari nchini: Hungaria, Poland na Prussia. Aliuwawa kikatili kutokana na ushuhuda wa imani yake kwa Kristo Yesu na Kanisa lake. Mtakatifu Adalbert alijitahidi kuwaongoa watu kwa ushuhuda wake, lakini akakumbana na kifo, kiasi cha kuleta mvuto mkubwa kwa watu wa Mungu nchini Poland. Alizaliwa mwaka 956 na kufariki dunia mwaka 997. Mama Kanisa anamwadhimisha kila mwaka ifikapo tarehe 23 Aprili. Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Katekesi yake, Jumatano tarehe 19 Aprili 2023 amewaalika waamini, lakini zaidi watu wa Mungu kutoka Poland, kumkimbilia kwa sala zao, ili aweze kuwaombea ujasiri wa kutangaza na kushuhudia imani yao kwa Kristo Yesu na Kanisa lake. Kazi ya Kristo ya Ukombozi hudhihirika katika Sakramenti Takatifu, na Liturujia ya Dominika ya Pili ya Pasaka inayozungumzia Sakramenti hizo katika mapana yake yaani: Ubatizo, Kitubio na Ekaristi Takatifu. Hivi ni visima vya huruma, msamaha na upendo wa Mungu visivyokauka. Kanisa huviongoza vizazi vyote vya dunia nzima kuelekea katika visima hivi vya: utakatifu, neema, baraka na matumaini.

Sherehe ya Huruma ya Mungu: Sakramenti, Toba Na Ushuhuda
Sherehe ya Huruma ya Mungu: Sakramenti, Toba Na Ushuhuda

Lakini kwa namna ya pekee kabisa kwa njia ya Sr. Maria Faustina Kowalska kwake tumepata kuifahamu ibada ya Huruma ya Mungu kwa njia mbalimbali. Kwa njia ya Picha ya Yesu wa Huruma inayomwonesha Yesu akibariki na miale miwili ikitoka katika ubavu wake uliochomwa kwa mkuki na chini imeandikwa Yesu Nakutumainia, ikimwalika mwanadamu kuitumainia daima Huruma kuu ya Mungu katika maisha yake. Njia ya Rosari ya Huruma ya Mungu inayomwalika mwanadamu kutakafakari Mateso makali ya Yesu aliyoyapata kwa ajili ya kumkomboa Mwanadamu kutoka katika lindi la dhambi na mauti na hivyo kumwalika kumtolea Baba wa milele kwa ajili ya dunia nzima. Njia ya Saa ya Huruma, yaani kujizamisha katika Huruma ya Mungu saa ya huruma kuu, saa 9 alasiri ambapo Kristo Yesu alidhihirisha upeo wa Huruma yake na kujitoa sadaka kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu. Njia ya Sherehe ya Huruma ya Mungu inayoadhimishwa Dominika ya Pili ya Kipindi cha Pasaka ambapo Kristo alitaka picha yake Ibarikiwe kwa ibada na waamini wapokee Sakramenti ya Kitubio na Ekaristi wapate maondoleo ya dhambi na adhabu zake.

Shutuma dhidi ya Mtakatifu Yohane Paulo II hazina msingi wowote
Shutuma dhidi ya Mtakatifu Yohane Paulo II hazina msingi wowote

Baba Mtakatifu Francisko katika maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 100 tangu kuzaliwa kwa Mtakatifu Yohane Paulo II, tarehe 18 Mei 2020 alisema kwamba, Mtakatifu Yohane Paulo II, kwa njia ya ushuhuda wa maisha yake, amejitahidi kuwafunulia watu, huruma na upendo wa Mungu, kama Kristo Yesu alivyomfunulia Mtakatifu Sr. Maria Faustina Kowalska wa Shirika la Masista wa Mama wa Mungu wa Huruma. Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Maadhimisho ya Sherehe ya Huruma ya Mungu, Dominika tarehe 16 Aprili 2023 aliyaelekeza macho na hisia zake kwa Mtakatifu Yohane Paulo II ambaye kwa siku za hivi karibuni, amezushiwa shutuma nzito dhidi ya utu wake, heshima na utakatifu wake, mambo ambayo hayana msingi wala ukweli wowote. Nalo Baraza la Maaskofu Katoliki Italia, limeungana na Baba Mtakatifu Francisko kuelezea kusikitishwa kwake na shutuma zinazotolewa dhidi ya Mtakatifu Yohane Paulo II, likisema, “kila mwanadamu ana thamani kubwa machoni pa Mwenyezi Mungu na kwa kila mmoja wao, Kristo Yesu ameyamimina maisha yake kwa ajili ya wokovu wao na Baba wa milele anawapatia wote zawadi ya Roho Mtakatifu, ili waweze kuunganika kwa dhati kabisa na Fumbo la Utatu Mtakatifu.”

Mtakatifu Yohane Paulo II: Ibada ya Huruma ya Mungu
Mtakatifu Yohane Paulo II: Ibada ya Huruma ya Mungu

Wakati huo huo, Baraza la Maaskofu Katoliki Poland tarehe 14 Machi 2023 limetangaza kuunda “Kikosi Kazi Maalum” ambacho kimepewa dhamana ya kuchunguza kwa kina shutuma za nyanyaso za kijinsia dhidi ya watoto wadogo zilizofanywa ndani ya Kanisa wakati Mtakatifu Yohane Paulo II alipokuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Krakow kuanzia mwaka 1964 hadi mwaka 1978 alipochaguliwa kuwa Papa. Kikosi Kazi kitachunguza nyaraka za Kanisa na Serikali ili kutafuta ukweli, kwa kuzingatia hali halisi ya wakati ule kisheria, kisiasa na kitamaduni.

Shutuma Dhidi ya JPII
19 April 2023, 15:04