Papa kwa Chuo Kikuu Péter Pázmány:epuka itikadi za kisasa dhidi ya maisha

Papa katika hotuba yake ya mwisho nchini Hungaria,akikutana na ulimwengu wa vyuo na utamaduni,katika Chuo Kikuu katoliki cha Péter Pázmány amezungumzia juu ya maarifa ambayo hayapaswi kuwekewa mipaka ya kiufundi yenye tabia ya utamaduni wa jikomboe mwenyewe.Onyo ni kuepuka matumizi fulani ya uharaka unaodhoofisha mwanadamu.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko katika hotuba yake ya mwisho ya ziara yake ya 41 ya kitume akizungumza na ulimwengu wa kiutamaduni na wanachuo katika Chuo Kikuu Katoliki cha Péter Pázmány amegusia  mada ya ujuzi, maendeleo ya kiufundi, kiburi cha kujiona uwezo, hadi kufika hatari ambayo mwanadamu anajiruhusu kunyongwa na mashine, akipoteza mguso wa ukweli na uwezo wa kukuza roho. Na katika hilo maneno yake pia yamekumbusha hatari za itikadi hizo ambazo zina wazo potofu la uhuru na yale ambayo nchi ya Hungaria imepitia. Baba Mtakatifu Francisko kwa hiyo  Dominika 30 Aprili 2023 jioni katika hotuba yake ameeleza kuwa nchi ya Hungaria imeona mfuatano wa itikadi ambazo zilijiweka kama ukweli, lakini hazikutoa uhuru. Na hata leo hii hatari hizo haijatoweka:kwa sababu amefikiria juu ya mpito kutoka katika ukomunisti kwenda  kwenye matumizi ya hovyo. Kile ambacho itikadi mbili zinafanana na ni wazo potofu la uhuru. Kwa sababu ukomunisti ulikuwa ni uhuru wa kulazimishwa, uliopunguzwa kutoka nje, ulioamuliwa na mtu mwingine, wakati matumizi ya hovyo ni uhuru,  ambao unawafanya watu kuwa watumwa wa matumizi na vitu.

Papa na ulimwengu wa Chuo Kikuu Katoliki nchini Hungaria
Papa na ulimwengu wa Chuo Kikuu Katoliki nchini Hungaria

Na ikiwa ni rahisi kupita kutoka katika mipaka iliyowekwa juu ya kufikiria, kama katika ukomunisti, hadi kufikiria bila mipaka, kama ile ya matumizi ya hovyo  na kutoka katika  uhuru uliozuiliwa hadi uhuru usio zuilika, Papa amesema, Yesu anafundisha kwamba kile kinachomweka mtu huru kutokana na utaratibu wake na kufungwa kwake, ufunguo wa kupata ukweli huo ni ujuzi ambao haujatenganishwa kamwe na upendo, uhusiano, unyenyekevu na uwazi, thabiti na jamii, ujasiri na kujenga. Papa kwa hiyo amefafanua mawazo yake juu ya ujuzi, huku akikumbuka sura ya Romano Guardini, ambaye alitofautisha wanyenyekevu na uhusiano, kwamba kuumba kulingana na asili, ambayo haipiti mipaka iliyowekwa na kwamba kuchambua na kushika mambo ambayo huleta pamoja nguvu na vitu ambapo mwisho  wake ni mmoja ambao ni mashine.

Ushuhuda wa Mwanafunzi wa Chuo Kikuu
Ushuhuda wa Mwanafunzi wa Chuo Kikuu

Kwa hiyo katika hilo Guardini hapitishi teknolojia, ambayo inatuwezesha kuishi vizuri zaidi, kuwasiliana na kuwa na faida nyingi, lakini anaonya juu ya hatari kwamba inawezakana kutawala maisha na kusababisha mwanadamu kupoteza mahusiano yote ya ndani ambayo yanampatia maana ya kipimo cha ndani  na namna za kujieleza kwa upatanisho na maumbile, kuweka kiholela malengo yake na kuyatekeleza katika kutawala na kulazimisha nguvu za asili. Mbele ya kukabiliana na haya yote, kama vile msomi mkuu na mtu wa imani, Papa Francisko ametoa mwaliko wa kujiuliza kama maisha yanaweza kubaki hai na kusisitiza swali kwa Chuo Kikuu kilichomkaribisha, ambacha sayansi ya kompyuta na sayansi ya biolojia inachunguzwa.

Wanafunzi wa Chuo Kikuu Katoliki Hungaria wakisikiliza Papa
Wanafunzi wa Chuo Kikuu Katoliki Hungaria wakisikiliza Papa

Mawazo ya Baba Mtakatifu yamekwenda kwenye mzozo wa kiikolojia, huku asili ikiguswa na matumizi fungamani ambayo mwanadamu anafanya; “kwa kukosa mipaka; katika mantiki ya "inaweza kufanywa, kwa hivyo inaruhusiwa"; kwa "hamu ya kuweka katikati ya kila kitu na sio mtu na uhusiano wake, lakini mtu mwenye pupa ya kupata na anayetamani kurarua  ukweli". Kwa namna ya pekee lakini kumomonyoka kwa mahusiano ya jamii,  Papa ametoa mwaliko kuwa " tuangalie, upweke na woga ambao kutoka katika hali ya uwepo unaonekana kugeuka kuwa hali ya kijamii". Kwa hili ameuliza swali "  Ni watu wangapi waliojitenga, wa kijamii sana na sio wa kijamii sana, wanaamua, kama katika duara mbaya, kwa faraja ya teknolojia ili kujaza utupu wanaohisi, wakiendesha kwa njia ya kichefuchefu zaidi huku, wakishindwa na ubepari wa kishenzi, wanahisi udhaifu wao wenye uchungu zaidi, katika jamii ambapo kasi ya nje inaendana na udhaifu wa ndani.

Papa Francisko amezungumza na ulimwengu wa chuo kikuu
Papa Francisko amezungumza na ulimwengu wa chuo kikuu

Baba Mtakatifu Francisko aidha amesema kuna kiburi cha kuwa nacho ambacho katika mtazamo wa kiteknolojia unazidisha, kwa matumizi fulani ya uharaka ambao unaweza na kutaja liwaya yenye kichwa: “Mkubwa wa ulimwengu”, cha mtunzi Robert Benson, ambaye tayari ametajwa katika hotuba kadhaa. Papa Francisko amekifafanua kama kitabu cha kinabii, ambacho kinaelezea mustakhbali unaotawaliwa na teknolojia mahali ambamo kila kitu, kwa jina la maendeleo, kimefutwa ambapo tofauti zinabatilishwa, maisha ya watu yamezuiliwa na dini na itikadi zinazopingana kukomeshwa hukutana katika upatanisho unaotawala kiitikadi” na ambapo “mwanadamu, akigusana na mashine, husawazisha zaidi na zaidi”. Katika hali kama hiyo, Papa  Francisko amesema, ni jambo ambalo kila mtu anaonekana kufa ganzi na kukosa usingizi,  na inaonekana wazi kuwatupa wagonjwa na kutumia euthanasia, na pia kufuta lugha na tamaduni za kitaifa ili kufikia amani ya ulimwengu, ambayo kwa kiukweli inabadilika kuwa mateso kwa kuzingatia uwekaji wa ridhaa.

Mbele ya kukabiliwa  na hali kama hiyo, Papa amekumbuka majukumu ya utamaduni na Chuo Kikuu, akibainisha kwamba Chuo Kikuu ni mahali ambapo mawazo yanazaliwa, hukua na kukomaa, ya uwazi na ya maelewano,  hekalu ambalo ujuzi huitwa kuwa huru, kutoka katika mipaka finyu ya kuwa na kumiliki ili kuwa utamaduni”, katika mahusiano hayo ambayo mwanadamu husitawisha na wapitao maumbile, na jamii, na historia, na uumbaji.  Hii ni kuonesha kiasi kwamba Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican, katika Gaudium et Spes, unathibitisha kuwa: “utamaduni lazima ulenge ukamilifu kamili wa mwanadamu, kwa manufaa ya jumuiya na jamii yote ya binadamu” na kwa ajili hiyo ni muhimu “kukuza roho  na uwezo wa kupongezwa, angavu, kutafakari, na kuwa na uwezo wa kuunda uamuzi wa kibinafsi na kukuza hisia za kidini, kiadili na kijamii.

Baraka kwa chuo Kikuu
Baraka kwa chuo Kikuu

Katika hilo pia Papa amesisitiza kuwa tunahitaji kutumia sayansi kuelewa na kufanya maamuzi sahihi, na kwa hilo tunahitaji unyenyekevu. Papa amesema wasomi wakuu, kiukweli ni wanyenyekevu. Siri ya maisha, kwa upande mwingine, inafunuliwa kwa wale wanaojua jinsi ya kuingia katika vitu vidogo. Inaeleweka kwa njia hiyo, utamaduni unawakilisha kweli ulinzi wa ubinadamu. Unazama katika kutafakari na kuunda watu ambao hawako katika mitindo ya wakati huu, lakini wamejikita vyema katika uhalisia wa mambo. Na ambao, wanafunzi wanyenyekevu wa maarifa, wanahisi lazima wawe wazi na wawasilianaji ambao kamwe sio  wagumu na wala wagomvi.

Kwa kifupi, wale wanaopenda utamaduni huleta ndani mwao hali ya kutotulia yenye afya.  Papa amesisitiza kuwa Mwenye kutafiti, hujiuliza, hujihatarisha na kuchunguza; na anajua jinsi ya kutoka nje ya uhakika wake mwenyewe ili kujitosa katika unyenyekevu wa fumbo la maisha ambalo kwa upande wake hujifungulia tamaduni nyingine na kuhisi hitaji la kubadilishana maarifa. Na hii ndiyo roho ya Chuo Kikuu, amesisitiza Papa, huku akibainisha kwamba Chuo Kikuu Katoliki cha Hungaria kinaishi kupitia programu za pamoja za utafiti na pia kwa kuwakaribisha wanafunzi kutoka maeneo mengine ya dunia, kama vile Mashariki ya Kati hasa kutoka Siria inayoteswa.

Papa akiaga wanachuo
Papa akiaga wanachuo

Askofu wa Roma amezidi kusisitiza kuwa utamaduni unatusindikiza kujijua sisi wenyewe. Tunatukumbushwa  na mawazo ya kiutamaduni, ambayo hayapaswi kamwe kuzama. Maneno maarufu ya simulizi za Delphi ambazo zimemjia akilini kwamba: “jitambue”. Kwa hiyo Papa Francisko amesema kwamba kujijua inamaanisha kuwa na uwezo wa kutambua mipaka ya mtu na kwa hiyo, kuzuia dhana ya mtu ya kujitosheleza na kwamba, ni kwa  kujitambua  tu kuwa viumbe ndipo tunaweza kuwa wabunifu, tukijikita katika ulimwengu, badala ya kutawaliwa nao. Aidha   Baba Mtakatifu amesisitiza kuwa  tunahitaji kutafakari juu ya ukweli kwamba mawazo ya kiteknolojia hufuata maendeleo ambayo hayakubali kikomo, na badala yake mwanadamu halisi pia ameundwa na udhaifu, na mara nyingi ni pale ambapo anaelewa kuwa anamtegemea Mungu na kushikamana na wengine na kazi ya uumbaji. Kwa hivyo kujijua kunamaanisha kuzingatia, fadhila msingi ya udhaifu na ukuu wa mwanadamu.

Na ikiwa ni rahisi kuhama kutoka katika mipaka iliyowekwa juu ya kufikiria, kama ya kutoka ukomunisti, kwenda kufikiria bila mipaka,  na ile ya utumiaji hovyo, na kutoka katika uhuru uliozuiliwa hadi uhuru bila kizuizi, Papa amesema Yesu anafundisha kwamba "ukweli hutuweka huru, na kwamba ukweli ni kile kinachomkomboa mwanadamu kutoka katika kujitosheleza na kufungwa kwake", kwa hiyo "ufunguo wa kupata ukweli huu"  kwa mujibu wa Papa  "ndiyo  ujuzi ambao haujafunguliwa kamwe kutoka katika upendo, uhusiano, unyenyekevu na uwazi, thabiti na jamii, ujasiri na wenye kujenga". Vyuo vikuu,  kwa hiyo vinaalikwa kuhamasisha njia hiyo  ya kujua, wakati imani inapaswa kumwilisha! Na matumaini  yake kwa Chuo Kikuu katoliki cha Hungaria na kwa kila chuo kikuu ni "kuwa kitovu cha ulimwengu wote na uhuru, kama shamba kubwa lenye matunda ya ujenzi wa ubinadamu na maabara ya matumaini", Papa Francisko amehitimisha.

Hotuba ya Papa kwa chuo Kikuu na ulimwengu wa utamaduni
30 April 2023, 17:00