Tafuta

2023.04.26 Kardinali Blase Joseph Cupich, Askofu Mkuu wa Chicago, na wawakilishi wa "Catholic Extension Society" 2023.04.26 Kardinali Blase Joseph Cupich, Askofu Mkuu wa Chicago, na wawakilishi wa "Catholic Extension Society"  (Vatican Media)

Papa Francisko:kusaidia maskini huboresha maisha ya jamii

Papa amekutana na wawakilishi wa Jumuiya ya chama katoliki cha jamii iliyopanuka,chombo cha Marekani kinachofanya kazi kwa ajili ya kuleta misaada katika maeneo maskini zaidi ya nchi.Papa amewaeleza kuwa Mtindo wa Mungu kamwe sio kujitenga na watu bali ni ukaribu,huruma na upole.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Chama cha Upanuzi Kikatoliki hufanya kazi kwa mshikamano na watu ili kujenga jumuiya za imani Kikatoliki zenye nguvu na mageuzi kati ya maskini katika maeneo maskini zaidi ya Marekani. Kwa hiyo Baba Mtakatifu  Francisko amewasalimia wawakilishi wa Chama hicho Jumatano tarehe 26 Aprili 2023 ambapo wamewakaribisha kwamba wamefika katika mkutano jijini Roma. Uwepo wao, umempatia fursa ya kuelezea hisia zake za shukrani katika jitihada za kusaidia majimbo ya kimisionari kwa namna ya pekee Marekani na kusaidia mahitaji ya maskini na watu walioa katika mazingia magumu.  

Papa na chama cha kusaidia maskini na watu walio katika mazingira magumu
Papa na chama cha kusaidia maskini na watu walio katika mazingira magumu

Baba Mtakatifu aidha amesema kwamba wao katika muktadha wa kujenga Mwili wa Kristo, na  Kanisa (Ef 4,12) na kutoa sauti kwa wale ambao mara nyingi hawana  sauti, wanashuhudia hadhi iliyotolewa na Mungu kwa kila mtu. Yaani kwa namna ya pekee leo hii wakati Kanisa zima linajitahidi kuwa katika mchakato wa  kisinodi. Kishirikiana na kujumuisha uzoefu na matarajio ya wengi, hasa wale ambao wanajikuta pembezoni mwa jamiii unatajirisha maisha na huduma ya kikanisa, kwa sababu Kanisa ni kama kitambaa kikubwa kichotengenezwa kwa uzi mmoja moja mahali wanapokuwa watu, lugha na tamaduni tofauti lakini zilizounganishwa na umoja wa Roho Mtakatifu,

Papa amekutana na wawakilishi kutoka Marekani wanaosaidia maskini
Papa amekutana na wawakilishi kutoka Marekani wanaosaidia maskini

Hakika, Roho huunda umoja kwa kuoanisha wingi wa viungo vya Mwili wa Kristo na utofauti wa karama zao. Katika suala hili, amefurahia uharaka wao wa kuweka katikati  utendaji wa kichungaji wa Kanisa wale ambao mara nyingi ni waathirika wa “utamaduni wa kutupwa leo hii, hivyo basi sauti yao inaweza kusikika na jamii kwa ujumla kunufaika. “Papa anawatia moyo waendelee kueleza “mtindo wa Mungu” katika kazi wanayofanya. Mtindo wa Mungu kamwe hauko mbali, kutengwa, au kutojali. Kinyume chake, ni mtindo wa ukaribu, huruma na upole. Huo ndio mtindo wa upole (cercanía, compasión y ternura. Dios va así, eso es lo estilo que tiene. Auspico che il vostro servizio rispecchi sempre queste qualità, vicinanza, compassione e tenerezza – cercanía, compasión y ternura), kwa kuonesha kwamba Bwana hukaribia maisha yetu, kwamba anachochewa na huruma kwa wale walio katika hali ngumu, kwamba upendo wake hutuita tujihusishe naye na kumwona jirani yetu kuwa kaka au dada wa kweli. Kwa hiyo, Kanisa linashukuru kwa kila onesho la mapendo ya kidugu na kujali wale wanaohitaji, ili huruma ya Mungu ionekane na muundo wa jamii ujiimarishe na kujipyaisha. Papa Francisko amependa kuonesha uwtambua a juhudi zao katika Kanisa na amewatakia kila ufanisi wa kazi yao. Juu yao na familia zao na wale ambao wanawahudumia ameomba Bwana na ili awabariki kwa hikia yake na nguvu zake. Amewaomba wasali kwa ajili yake.

Hotuba ya wawakilishi wa chama cha Catholic Extension Society
26 Aprili 2023, 17:00